Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Thx mkuu unaongeza hadhi ya JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuna blacks aliyekufa kwa Corona duniani??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi sasa hakuna mwafrika alieumwa isipokuwa yule jamaa wa Cameron kule China lakini alipona haraka saana na kuwa discharged hospitalini.

Hapo ndipo tafiti zikakiri kwamba waafrika Wako more immuned na Corona virus. Na hii inaweza kuwa kweli coz hakuna mwafrika anaekufa kutokana na mafua and technically Corona Ni mafua pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 14 vimeripotiwa katika jimbo la North Rhine-Westphalia magharibi mwa Ujerumani.

Pia, visa vipya vinne (4) vimeripotiwa katika jimbo la Baden-Württemberg kusini magharibi mwa nchi hiyo huku pia jimbo jingine la Bavaria likiripoti kisa chake cha kwanza cha COVID-19.

Hadi hivi sasa, Ujerumani imeripoti jumla ya visa 45, wagonjwa takribani 16 wameripotiwa kupata ahueni huku wagonjwa wawili (2) wakiwa katika hali mbaya zaidi.
 
UPDATE: Uswidi imeripoti visa vipya vitano (5) nchini humo. Mpaka sasa, nchi hiyo imekwisharipoti visa vipatavyo saba (7).
 
UPDATE: Ufaransa imeripoti visa vipya 20 nchini humo.

Mpaka sasa, Ufaransa ni nchi ya tatu kwa kuwa na visa vingi zaidi barani Ulaya baada ya Italia na Ujerumani.

Ufaransa imeripoti jumla ya visa 38 vikiwemo vifo viwili (2) huku wagonjwa wapatao 11 wakiripotiwa kupata ahueni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…