Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Taarifa ni kutoka katika vyanzo mbalimbali vya kuaminika;
  • Vyombo mbalimbali vya habari duniani (News Media).
  • Mamlaka za nchi husika (Taasisi/Wizara za afya n.k. kupitia tovuti)
  • Taasisi za kimataifa. WHO n.k.
  • Vyanzo vingine
Takwimu ama ripoti zote ninazozileta humu zenye utangulizi "BREAKING", "UPDATE" au mara nyingine "NEW/MPYA" mwanzoni mwa taarifa hizo, ni rasmi na zimethibitishwa na mamlaka za sehemu husika ama taasisi zenye dhamana.

Taarifa zenye utangulizi "NEWS ALERT" ni kutoka katika media ama vyombo mbalimbali vya habari vya kuaminika.
Thx mkuu unaongeza hadhi ya JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuna blacks aliyekufa kwa Corona duniani??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi sasa hakuna mwafrika alieumwa isipokuwa yule jamaa wa Cameron kule China lakini alipona haraka saana na kuwa discharged hospitalini.

Hapo ndipo tafiti zikakiri kwamba waafrika Wako more immuned na Corona virus. Na hii inaweza kuwa kweli coz hakuna mwafrika anaekufa kutokana na mafua and technically Corona Ni mafua pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali Ni mbaya tofauti na tunavyodhani. Imetokea Leo hii.
tapatalk_1582836324721.jpeg
tapatalk_1582836142831.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 14 vimeripotiwa katika jimbo la North Rhine-Westphalia magharibi mwa Ujerumani.

Pia, visa vipya vinne (4) vimeripotiwa katika jimbo la Baden-Württemberg kusini magharibi mwa nchi hiyo huku pia jimbo jingine la Bavaria likiripoti kisa chake cha kwanza cha COVID-19.

Hadi hivi sasa, Ujerumani imeripoti jumla ya visa 45, wagonjwa takribani 16 wameripotiwa kupata ahueni huku wagonjwa wawili (2) wakiwa katika hali mbaya zaidi.
 
UPDATE: Uswidi imeripoti visa vipya vitano (5) nchini humo. Mpaka sasa, nchi hiyo imekwisharipoti visa vipatavyo saba (7).
 
UPDATE: Ufaransa imeripoti visa vipya 20 nchini humo.

Mpaka sasa, Ufaransa ni nchi ya tatu kwa kuwa na visa vingi zaidi barani Ulaya baada ya Italia na Ujerumani.

Ufaransa imeripoti jumla ya visa 38 vikiwemo vifo viwili (2) huku wagonjwa wapatao 11 wakiripotiwa kupata ahueni.
 
Back
Top Bottom