Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Jana tu tumetoka kuliongea hili ila Viongozi wetu wakahisi hela za utalii ni bora kuliko uhai. Poor country, poor mind , bad leadership
TAARIFA ZA HIVI PUNDE.
MTALII MMOJA RAIA WA CHINA AMEWEKWA CHINI YA UANGALIZI MAALUM KWENYE HOTEL YA RIVER TREE ILIYOPO USA RIVER ARUSHA, BAADA YA KUWA NA DALILI ZOTE ZA UGONJWA WA CORONA. MADAKTARI KUTOKA HOSPITALI YA WILAYA TENGERU NA HOSPITALI YA MKOA YA MOUNT MERU WAMESHAFIKA KWENYE HOTEL YA RIVER TREE MUDA HUU.
Jamani Tumuombe Mungu waTanzania tutakwusha

C&P

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Korea Kusini

Visa vipya 219 vimeripotiwa nchini humo pamoja na kifo kipya kimoja (1) na kufikisha jumla ya visa 3,150 nchi nzima huku idadi ya vifo ikifikia 17 hadi sasa.

Pamoja na ripoti ya awali, Korea Kusini imeripoti visa vipya vipatavyo 813 ndani ya siku moja.
 
UPDATE: Iran

Visa vipya 205 pamoja na vifo vipya tisa (9) vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 593 na vifo 43 hadi sasa.

Mpaka sasa Iran ni nchi ya pili baada ya China kwa kuripoti vifo vingi zaidi duniani vinavyohusishwa na virusi vya COVID-19.
 
UPDATE: Visa vya kwanza

Kisa cha kwanza kimeripotiwa Qatar huku nchi nyingine ya Ecuador ikiripoti kisa chake cha kwanza kabisa cha COVID-19 nchini humo.
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya vitatu (3) vimeripotiwa katika jimbo la North Rhine-Westphalia nchini humo.

Mojawapo ya visa hivyo ni mwanamke ambaye amekuwa akitibiwa mjini Aachen kwa sababu nyinginezo.

Visa vingine viwili ni mama na mtoto wake wa kiume walioko Würselen mjini Aachen.
 
UPDATE: Kisa kipya kimeripotiwa nchini Denmark. Mtu huyo alirejea nchini humo hivi karibuni akitokea Munich nchini Ujerumani.
 
UPDATE: Italia

Visa vipya 239 vimeripotiwa nchini humo sambamba na vifo vipya nane (8).

Mpaka sasa idadi ya visa vyote nchini humo imeongezeka mpaka kufikia 1,128 huku idadi ya vifo ikifikia 29 nchi nzima hadi sasa.

Pia, imeelezwa kuwa wagonjwa wapatao 105 wako katika hali mbaya zaidi na wamewekwa katika vyumba maalumu kwaajili ya wagonjwa mahututi (ICU).
 
corona imeingia italy kwa fujo gia namba 4 mixer kustunt kwa sana😀😀😀😀😀😀😀
 
UPDATE: Marekani imethibitisha kifo cha kwanza nchini humo kinachohusishwa na virusi vya Corona katika jimbo la Washington.

Kifo hicho ni miongoni mwa visa vipya kadhaa vilivyoripotiwa hivi karibuni katika jimbo hilo, maafisa wameeleza.
 
UPDATE: Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump ameeleza kuwa mtu huyo aliyeripotiwa kufariki dunia alikuwa na umri wa miaka ya hamsini (50s), mwanamke aliyekuwa na matatizo mengine ya kiafya.

Trump ameongeza pia, watu wengine wanne wako katika "hali mbaya zaidi".

Pia, Gavana wa jimbo la Washington, Jay Inslee, ametangaza hali ya hatari kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona katika jimbo hilo.
 
NEWS ALERT: White House gives details on first coronavirus death. (VIDEO)

NEWS ALERT: The Trump administration Saturday announced additional travel restrictions affecting Iran, Italy and South Korea in response to the coronavirus outbreak, following the first death from the virus in the United States. [WaPo]
 
UPDATE: Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump ameeleza kuwa mtu huyo aliyeripotiwa kufariki dunia alikuwa na umri wa miaka ya hamsini (50s), mwanamke aliyekuwa na matatizo mengine ya kiafya.

Trump ameongeza pia, watu wengine wanne wako katika "hali mbaya zaidi".

Pia, Gavana wa jimbo la Washington, Jay Inslee, ametangaza hali ya hatari kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona katika jimbo hilo.
UPDATE: Marekani imethibitisha kifo cha kwanza nchini humo kinachohusishwa na virusi vya Corona katika jimbo la Washington.

Kifo hicho ni miongoni mwa visa vipya kadhaa vilivyoripotiwa hivi karibuni katika jimbo hilo, maafisa wameeleza.
hapa sasa tutaanza kuelewana nadhani watu sasa watapata kuamini ni janga la dunia mana wengi mawazo yao marekani ndo amesambaza hivi virusi ila kufikia hapa bira ushirikiano tutaangamia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Visa vya kwanza vya COVID-19
  • Kisa cha kwanza kimeripotiwa nchini Luxembourg
  • Kisa cha kwanza kimeripotiwa nchini Ireland
 
UPDATE: Visa vipya vya COVID-19
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Mexico na kufikisha jumla ya visa vitatu (3) nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Thailand na kufikisha jumla ya visa 42 nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Norway na kufikisha jumla ya visa saba (7) nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Uswidi na kufikisha jumla ya visa 12 nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Georgia na kufikisha jumla ya visa vitatu (3) nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Croatia na kufikisha jumla ya visa sita (6) nchini humo
 
Back
Top Bottom