Huu ugonjwa huko China haujaanza jana wala juzi, hadi China inautangazia ulimwengu kuwa kuna tatizo la Corona, ni dhahiri kabisa ni baada ya kulemewa na kuanza kusambaa kwa taarifa mitandaoni ndio wakaamua sasa kusema,muda wanaongea huenda tatizo limeshazunguka dunia nzima.
Ni kwamba nilikuwa China mwezi Septemba jimbo moja la Kunming, wakati naondoka Airport ya Bejing Kwenda jimbo la Kunming ndani ya ndege nilishuhudia hali mbaya sana ya afya za abiria wa kichina,walikuwa wakikohoa na makohozi hadi najisikia vibaya,nikishindwa hata kupata breakfast humo,hali hy niliikuta pia kwenye flight to Kunming kwenda Gasa...nikajua ni homa ya mapafu na koo labda kwa vile wachina wanavuta sigara sana.
Niliporudi hapa bongo niliugua sana madonda ya kooni na homa kali baada ya wiki moja mke wangu akaugua na wanangu wawili kwa pamoja,japo wote walipona homa ileile....sasa baada ya ugonjwa ule kutajwa nilipoangalia dalili,ni zilezile.....CORONA...
Ugonjwa humu nchini upo,sema tu huenda kweli waafrika tupo tolerant na ugonjwa huo,ugonjwa huu utakuwa umesambaa dunia nzima.
Sent using
Jamii Forums mobile app