Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Mkuu nikitulia ntalipitia hili gaazeti maaana naliona lina mafacts hapa ndani.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FAHAMU: Visa vya COVID-19 hadi sasa barani Afrika.

Nchi zipatazo nane (8) zimethibitisha visa vya COVID-19 barani Afrika hadi hivi sasa huku nchi nne (4) kati ya hizo ni zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).

Nchi hizo ni; Algeria, Senegal, Misri, Morocco, Cameroon, Nigeria, Tunisia pamoja na Afrika Kusini.

Idadi ya visa barani humo ni kama ifuatavyo;

1. Algeria: Visa 17 hadi sasa vimeripotiwa nchini humo.

2. Senegal: Nchi ya pili kwa kuripoti visa vingi zaidi barani Afrika. Hadi sasa imeripoti visa vinne (4).

3. Misri: Visa vitatu (3) vimeripotiwa nchini humo huku mmoja akithibitika kupata ahueni.

4. Morocco: Visa viwili (2) vimeripotiwa nchini humo hadi sasa.

5. Cameroon: Visa vya kwanza viwili (2) ambavyo ni raia wa kigeni (Ufaransa).

6. Nigeria: Kisa kimoja (1) tu kimeripotiwa nchini humo hadi sasa huku watu wengine kadhaa wakihofiwa kuwa na maambukizi.

7. Tunisia: Kisa kimoja (1) kimeripotiwa nchini humo hadi sasa.

8. Afrika Kusini: Kisa kimoja (1) tu hadi sasa kimeripotiwa nchini humo.

Taarifa zaidi zitafuata!

Cc: YOUNGBLOOD
 
Mkuu vipi kuhusu Nigeria? Sikuona update yake muda kidogo.
Kuhusu Nigeria; Idadi ya visa ni kile kile kimoja (1) kilichoripotiwa awali ingawa kuna watu kadhaa wanahofiwa kuwa na maambukizi ya COVID-19.

Updates zozote zitakazotoka hapo baadaye, nitazileta humu.
 
Asante sana mkuu,kazi nzuri.
 
Miongoni mwa visa hivi yupo mtu mweusi?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hadi sasa kuna mtu mweusi yeyote ameshafariki kwa hivyo virusi?
 

swali la ufahamu tu je kuna any reported and confirmed case ya mtu mweusi kufariki kutoka na huyo virus?!
 
UPDATE: Visa viwili (2) vya kwanza vilivyoripotiwa hapo awali nchini Cameroon ni raia wa Ufaransa huku kisa cha pili kikiwa ni raia wa nchini Cameroon.

Visa vyote viwili vinahusiana ambapo imeripotiwa kuwa, Mfaransa huyo aliingia nchini Cameroon mnamo mwezi Februari ambapo alikutana na raia huyo wa Cameroon.

Wote wawili wamekwisha tengwa katika sehemu maalumu katika hospitali moja mjini Yaounde, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya afya ya Cameroon.
 

nawasiwasi na huyo Mkameruni huenda ni Mkameruni mwenye asili ya Kifaransa.

ukupata kisa cha mtu mweusi (black skin) kufariki tafadhali nitag.
 
NEWS ALERT: Pope Francis will deliver Sunday's Angelus Prayer by livestream instead of in person out of concern over spreading the new coronavirus, the Vatican says. [AFP]
 
naiwe hivyo hivyo uthibitisho usipatikane kwa mtu mweusi...
maana mtu mweusi na mizigo mingi sana na ndio imemkomaza hata kuhimili baadhi ya infection ya virusi.
ha ha ha mkuu umenichekesha eti naiwe hivyo usipatikane
dah ! sema tuombe hilo janga iwe kweli halimuathili black people mana km ni kusema joto nchi zenye joto zisharepotiwa tayari kuwa na maambukizi
hvyo tuombe uwe ugonjwa wa wanaojiweza hao weupe
we fikilia hongkong tu imegawa zaidi ya mln 1 na ushehe kwa kila mwananchi wake zakujikimu
wkt ITARY yeye katenga zaidi ya trilion 17 kupambana kuhakikisha wananchi wake wanabaki salama
wkt hapa bongodasilamu likitokea tetemeko tu yeye hajaleta tetemeko na pesa za rambirambi zinaliwa
sasa ikija hiyo COVID-19 maiti si zitagaa mtaani tu mana tutakimbiana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NEWS ALERT: Kiongozi wa chama cha siasa cha Democratic cha nchini Italia ametangaza kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Nicola Zingaretti, ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho, ameyasema hayo baada ya kufanyiwa vipimo ambapo kwa sasa amejitenga.

 
NEWS ALERT: Italy recruits retired doctors to battle coronavirus crisis as deaths rise to 197. [Daily Mail]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…