Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 96 nchini humo sanjari na vifo vipya 28 nchi nzima huku visa 74 kati ya hivyo vikiripotiwa Hubei pekee.
 
UPDATE: Mainland China
  • 80,651 confirmed cases so far
  • 3,070 deaths so far
  • 5,489 in serious condition
  • 55,404 recoveries
 
UPDATE: Korea Kusini imeripoti visa vipya 174 pamoja na vifo vipya viwili (2) nchini humo na kufikisha jumla ya visa 6,767 pamoja na vifo 44 nchi nzima.
 
UPDATE: South Korea
  • 6,767 confirmed cases so far
  • 44 deaths so far
  • 52 in serious/critical condition
  • 108 recoveries
 
UPDATE: Norway imeripoti visa vipya 26 nchini humo na kufikisha jumla ya visa 127 nchi nzima.

Hadi hivi sasa, Norway haijaripoti kifo chochote kinachohusishwa na COVID-19 nchini humo.
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 31 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 670 ambapo wagonjwa wapatao wawili (2), wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 17 wakiripotiwa kupata ahueni.

Mpaka sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kile kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 28 vimeripotiwa nchini Uhispania na kufikisha jumla ya visa 402 huku wagonjwa wapatao saba (7) wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine wawili (2) wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia tano (5) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Barani Afrika

Visa viwili (2) vya kwanza vimeripotiwa nchini Cameroon.

Visa viwili vya Cameroon ni raia wa kigeni kutoka nchini Ufaransa.
 
UPDATE: Iran

Visa vipya 1,234 pamoja na vifo vipya 16 vimeripotiwa nchini Iran hivyo kufikisha jumla ya visa 4,747 huku wagonjwa wapatao 913 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 124 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Visa vya kwanza vya COVID-19
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa nchini Bhutan
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa nchini Serbia
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa jijini Vatican
  • Kisa cha kwanza (1) kimeripotiwa nchini Colombia
 
UPDATE: Italia

Visa vya COVID-19 vipatavyo 4,636 vimekwisha ripotiwa nchini Italia hadi sasa ambapo wagonjwa wapatao 462 wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 523 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 197 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Marekani

Idadi ya visa vyote nchini Marekani imefikia 329 hadi sasa ambapo wagonjwa wapatao nane (8) wako katika hali mbaya zaidi huku wengine tisa (9) wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 16 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Japan

Idadi ya visa vyote nchini humo imefikia 350 hadi sasa huku wagonjwa wapatao 29 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 10 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) vilivyothibitika nchini Japan imefikia sita (6) hadi hivi sasa.
 
Hakuna kitu kizuri kama ukiamua jifunza mkuu , upeo wako wa kufikiri usidhani dunia ndio imeishia hapo , siko kwenye mood ya kuandika ila nitaandika summary kwa uchache sana zikufungue kidogo , na ukitoka hapa ukasome

Kwamba hatuna dawa wala kinga ila mtu anaponaje ponaje , leo ukiugua ugonjwa wowote unaosababishwa na parasites, bakteria au worms au fangasi , unapata dawa hakuna shida .. ila upande wa virusi hua inatokea nini ??

naomba ieleweke kwanza hii ni virusi wote sio korona pekee ,sio jamii moja , virusii wote hakuna dawa, na hii husabishwa na sifa yao kuu , wanaishi mazingira yote , mfu na hai , lakn pia wana uwezo mkubwa sana wa kutengeneza resistance na mambo mengine kadhaa wa kadhaa (ukasome)

HUA KINAFANYIKA NINI SASA ENDAPO MWILI WAKO UKIVAMIWA NA VIRUSI

hua kuna counter measure zinatumika ..mfano , virusi kwa asilimia kubwa hua wanashambulia mifumo mbali mbali ya mwili , ambayo mwsho wa siku husababisha hiyo mifumo ifeli au wewe kupata magonjwa nyemelezi , so hua wanafanya nini
- Kwenye seli zako za mwili , ili ziweze pokea kitu chochote, iwe kirusi au bakteria lazima kuwepo mlango wa kuingia , milango hii huitwa receptors au protein, na kama unavyo faham , virusi hua vinafanya kazi vikiwa ndani ya seli , ..wataalamu wanacho fanya hapa , hua wanaua hizo receptors , ili kirusi kisiendelee kuvamia seli , so hapo seli zako tayari ziko salama, immune system yako inasalimika

pia , dawa ya kuwaua hatuna ila tunaweza wazuia wasiendelee ongezeka ndani ya mwili ...hatua nyingine hiyo

kuwaua hawawezi ila wanaweza wafubaza hivyo unawapunguzia uwezo wao wa kutenda kazi na kulela madhara

pia , vinanyimwa uwezo wa kuendelea kufanya madhara endapo wakitoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine

..wanatibu magonjwa nyemelezi ambayo mara nyingi ndio yanayo ua watu kwasababu kirusi kishamaliza mfumo wa ulinzi wa mwili, na mambo mengine mengi mengi... preventive measure kibao huko nje


sehemu kubwa ya vita dhidi ya kirusi inategemea wewe mwenyewe immune system yako ikoje , kama ni imara , wakafanya counter measures hizo unapona

na mambo mengine mengi mengi tuuu , nadhan kwa kias fulan nimekufungua macho ni namna gani wana dili na ebola , corona na the likes na inakuaje watu wanapona , na hata kwa vile virusi vilisivyo pona , wanapambana kuvinyamazisha kwa mifumo hii hii , hadi vitulia tulii , unaishi miaka 20 unavyo .

anyway..endelea kuungana na huyo jamaa, mnadhani upeo wenu wa kufikiri ulipo ishia basi na dunia imeishia hapo hapo , muwe na siku njema

Sent using Jamii Forums mobile app
thnkx kwa kutufumbua macho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom