Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Iran imeripoti kifo kipya kinachomhusu kiongozi mwingine wa ngazi za juu nchini humo.

Hossein Sheikholeslam, mshauri wa waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif ambaye pia aliwahi kuwa balozi wa nchi hiyo nchini Syria, ameripotiwa kufariki dunia mnamo Machi 5 kutokana na ugonjwa ya virusi vya Corona (COVID-19), janga ambalo limeambukiza maelfu nchini Iran.

1583461950171.png
 
UPDATE: Italia

Visa vipatavyo 3,858 vimekwisha ripotiwa nchini humo hadi sasa ambapo wagonjwa wapatao 351 wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 414 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini Italia imefikia 148 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Marekani

Hadi hivi sasa, Marekani imeripoti visa 210 nchini humo ambapo wagonjwa wapatao nane (8) wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine tisa (9) wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 12 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Hong Kong

Hadi sasa, visa vipatavyo 105 vimeripotiwa Hong Kong wakiwemo wagonjwa sita (6) walioko katika hali mbaya zaidi huku wengine 36 wakiripotiwa kupata nafuu.

Hong Kong imeripoti vifo viwili (2) kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Iran

Visa vipatavyo 3,513 vimeripotiwa nchini humi hadi hivi sasa ambapo wagonjwa wapatao 552 wameripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 108 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Barani Afrika

1. Afrika Kusini imeripoti kisa cha kwanza (1) cha COVID-19 nchini humo.

2. Misri imeripoti kisa kipya kimoja (1) nchini humo na kufikisha jumla ya visa vitatu (3) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Ufaransa

Visa vipatavyo 423 vimeripotiwa nchini Ufaransa hadi hivi sasa wakiwemo wagonjwa wapatao 23 ambao wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 12 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia saba (7) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Japan

Japan imethibitisha jumla ya visa 350 nchini humo hadi hivi sasa wakiwemo wagonjwa wapatao 29 ambao wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 10 wakipata ahueni.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) vilivyothibitika nchini Japan imefikia sita (6) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Duniani

Mpaka sasa, visa vipatavyo 98,101 vimethibitishwa duniani kote huku idadi ya vifo vyote vilivyotokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) ikifikia 3,386 ulimwenguni hadi hivi sasa kulingana na takwimu rasmi.
 
Ni vile tu nimechoka kuandika ila kukusaidia kuanzia leo hii tambua ya kua HAKUNA KIRUSI CHOCHOTE KILE CHENYE DAWA , CHOCHOTE KILE

jua hilo kuanzia leo hii, mengine utaongezea mwenyewe kwa kusoma

Sent using Jamii Forums mobile app

Baada ya kutambua kwamba hakuna kirusi chochote chenye dawa,then jiulize hiyo asilimia 98 ya walioambukizwa wanaponaje.

Itendee haki akili yako.Just take few minutes to think,usikimbilie kunijibu kwanza,just think about that.
 
Acha ujinga ww, ukitaka kupiga hesabu vzr piga death toll over recovered, kama wenye ugonjwa wote asilimia kubwa wamepata leo je???
Then kibaya ni kuwa hapa bado haujamutate unaua watu hivi
Usiongee kama mtoto wa darasa la pili, ongea kama mtu mzimaView attachment 1378298

Sent using Jamii Forums mobile app
Tutakutana tena baada ya drama hii kuisha,nakuhakikishia utajiona mjinga sana.
 
Baada ya kutambua kwamba hakuna kirusi chochote chenye dawa,then jiulize hiyo asilimia 98 ya walioambukizwa wanaponaje.

Itendee haki akili yako.Just take few minutes to think,usikimbilie kunijibu kwanza,just think about that.
Ina maana kirusi chochote ina dawa na tiba zake kutegemea na aina ya ugonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kutambua kwamba hakuna kirusi chochote chenye dawa,then jiulize hiyo asilimia 98 ya walioambukizwa wanaponaje.

Itendee haki akili yako.Just take few minutes to think,usikimbilie kunijibu kwanza,just think about that.
sio hiyo 98% tu .. jiulize ni magonjwa mangapi ya virus yaliyoko dunian ? tena mengine ni deadly kweli kweli ... Hakuna tiba hakuna nini lakini watu wanapona

home work, nenda kasome , utajua n kwa namna gani wataalamu wanakabiliana nayo , na pia utajua ni kwann hakuna dawa ya kirusi chochote kile

Hao waliopona wameponaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Duniani

Mpaka sasa, visa vipatavyo 98,101 vimethibitishwa duniani kote huku idadi ya vifo vyote vilivyotokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) ikifikia 3,386 ulimwenguni hadi hivi sasa kulingana na takwimu rasmi.
Mkuu FRANC unaweza ukatupa update nzima ya Africa kwa mataifa yote yaliyokumbwa na COVID-19
 
UPDATE: Barani Afrika

1. Afrika Kusini imeripoti kisa cha kwanza (1) cha COVID-19 nchini humo.

2. Misri imeripoti kisa kipya kimoja (1) nchini humo na kufikisha jumla ya visa vitatu (3) hadi hivi sasa.

Mkuu vipi kuhusu Nigeria? Sikuona update yake muda kidogo.
 
Back
Top Bottom