UPDATE: Barani Afrika
1. Misri imeripoti visa vipya 13 nchini humo pamoja na kifo kipya kimoja (1). Idadi ya visa vyote nchini humo imefikia 80 hadi sasa.
2. Ivory Coast imeripoti kisa cha kwanza nchini humo. Raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 45 ambaye alisafiri kuelekea nchini Italia hivi karibuni.
3. Gabon imeripoti kisa cha kwanza nchini humo. Kisa hicho ni raia wa Gabon mwenye miaka 27 aliyerejea nchini humo mnamo Machi 8 akitokea nchini Ufaransa.
4.Ghana imeripoti visa vya kwanza viwili (2) nchini humo. Wawili hao walirejea nchini humo wakitokea katika mataifa ya Norway na Uturuki.
Hadi saa nchi zipatazo kumi (10) za kusini mwa jangwa la Sahara zimekwisha ripoti visa vya COVID-19 katika nchi zao; Ivory Coast, Nigeria, Senegal, Cameroon, Togo, Afrika Kusini, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Gabon pamoja na Ghana.