Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Uholanzi imeripoti kisa chake cha kwanza kabisa cha COVID-19.

Kisa hicho kimeripotiwa katika mji wa Tilburg, mji ambao upo karibu na mpaka wake (Uholanzi) na nchi ya Ubelgiji.

Imeelezwa kuwa, mtu huyo alirejea nchini humo hivi karibuni akitokea nchini Italia.
 
Ningekuwa Mello ningekuwa naakulipa kiasi kwa kazi nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Kisa kipya cha COVID-19 kimeripotiwa barani Afrika nchini Nigeria

Wizara ya afya ya Nigeria imethibitisha kisa cha kwanza kabisa cha virusi vya Corona nchini humo mnamo Februari 27.

1582852280380.png
 
UPDATE: Nigeria

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Waziri wa afya, Osagie Ehanire, kisa kilichoripotiwa nchini humo ni raia wa kigeni ambaye tayari amekwishawekwa katika uangalizi maalumu nchini humo huku taratibu za kufuatilia taarifa zake kamili zikiendelea.

Taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa hapo baadaye.
 
Mungu atusaidie. Hii Corona inasambaa kwa Kasi Sana, Na ubaya unaweza ambukiza mtu hata kabla wewe mwenyewe kuanza kuonesha dalili zake hiyo ndio hatari zaidi.

Hata Ebola outbreak haikuenea kwa Kasi hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
Haikuweza kuenea kwa Kasi sababu ilikuwa Ni ya papo kwa papo. Tofauti na Corona mtu anaweza kusafiri nayo umbali mrefu.

Ebola yenyewe ilikuwa Haina muamana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa walikataa kabisa kufunga mpaka na Italy
UPDATE: Ufaransa imeripoti visa vipya 20 nchini humo.

Mpaka sasa, Ufaransa ni nchi ya tatu kwa kuwa na visa vingi zaidi barani Ulaya baada ya Italia na Ujerumani.

Ufaransa imeripoti jumla ya visa 38 vikiwemo vifo viwili (2) huku wagonjwa wapatao 11 wakiripotiwa kupata ahueni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom