Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Hello
Nitangulize samahani kwenu maana nitatumia uzi huu kuomba ushauri kwa sababu ndio wapo member wenye fully update za corona na hali ya kiuchumi ya dunia kwa sasa so sina budi. Tafadhari usinitukane nijibu na km nitakuwa nimekuudhi narudia samahani sana.
Nipo mbioni kufungua biashara ya mtaji km mil 5 hv lakin nategemea bidhaa tokea china, sasa je kwa hali ya huu ugonjwa kwasasa maoni yako yapoje nifungue hautoniathiri maana pia najaribu kuwaza labda nishafungua alafu yanatokea km yale ya china wote tunafungiwa ndani then pesa ushanunua bidhaa na kukodi fremu hii mbona km itanigharimu, kwa hiyo hapa nipo dilemma
Naomba msaada wako wa kimawazo tafadhari.


Sent using Jamii Forums mobile app
kwa sasa nakushauri subiri kwanza mpk ufike mwezi wa 6 hivi sikilizia upepo wa corona
7bu nchi nyingi si china tu pekee wamefunga biashara zao mashure maofisi hata public issue nk
na kuna hata baadhi ya matukio yamesitishwa kwa mfano HOLLYWOOD wamesitisha kulaunch movie nyingi tu wamepostpone mpk swala la corona lieleweke
hvyo kwa sasa hifadhi pesa yako mkuu au izungushe kwenye biashara za hapahapa hasa zinazohusu biashara za vyakura ndo deal now na hata ugonjwa ukifika lazima watu wale
kwa sasa hv watu wengi hawatumii pesa hovyo kwa vitu vya anasa au visivyo na lazima wanaficha pesa kuhofia corona ikiingia
mfn ni mm matumizi nimepunguza ya siku toka elf 20 25 mpk elf 10 to 15 na kila siku najibana nahifadhi elf 10 au 15 ambapo hapo awali sikuweza kabisa
lkn nikiangalia familia naona kuna kitu nifanye na nafanya hivi hata likivoromoka hilo gonjwa nijue cha kufanya mana kusema ninnuue vyakura vya miezi 3 nihifadhi ndani uwezo huo sina
nadhani umewasikia wenye mamlaka kuwa hawana uwezo
hivyo matumizi ya vitu visivyo na ulazima nimeacha hivyo si mm tu hata watu wengi ambao ili tupate pesa lazima tutoke kila siku tumekuwa makini na matumizi ya pesa
hvyo ushauri wangu tulia kwanza uangalie upepo unavyokwenda 7bu hata kuagiza mzigo kuupata itakuchukua muda au usiupate kabisa
kazi ni kwako mkuu
 
Imekaa vizuri hii asante
kwa sasa nakushauri subiri kwanza mpk ufike mwezi wa 6 hivi sikilizia upepo 7bu nchi nyingi si china wamefunga biashara zao mashure maofisi hata public issue nk
na kuna hata baadhi ya matukio yamesitishwa kwa mfano HOLLYWOOD wamesitisha kulaunch movie nyingi tu wamepostpone mpk swala la corona lieleweke
hvyo kwa sasa hifadhi pesa yako mkuu izungushe kwenye biashara za hapahapa hasa zinazohusu biashara za vyakura ndo deal now
7bu sasa hv watu wengi hawatumii pesa hovyo kwa vitu vya anasa wanaficha kuhofia corona
mfn ni mm matumizi nimepunguza ya siku toka elf 20 25
mpk elf 10 to 15 na kila siku najibana nahifadhi elf 15 ambappo hapo awali sikuweza kabisa
nafanya hivi hata likivoromoka hilo gonjwa nijue cha kufanya nahani umesikia wenye mamlaka hawana uwezo

matumizi ya vitu visivyo na ulazima nimeacha hivyo si mm tu hata watu wengi ambao ili tupate pesa lazima tutoke kila siku tumekuwa makini na matumizi ya pesa hvyo ushauri wangu tulia kwanza uangalie upepo unavyokwenda 7bu hata kuagiza mzigo kuupata itakuchukua muda au usiupate kabisa kazi kwako mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Uingereza

Idadi ya visa vyote nchini humo imefikia 273 hadi sasa huku wagonjwa wapatao 12 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) vilivyothibitika nchini Uingereza ni vifo viwili (2) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Iran

Idadi ya visa vyote imefikia 6,566 hadi sasa nchini humo huku wagonjwa wapatao 2,134 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) vilivyothibitika nchini Iran ni 194 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Korea Kusini

Idadi ya visa vyote imefikia 7,313 hadi sasa nchini humo huku wagonjwa wapatao 130 wakiripotiwa kupata nafuu na wengine 36 wakiwa mahututi.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) vilivyothibitika nchini Korea Kusini ni 50 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Barani Afrika

Afrika Kusini imeripoti kisa kipya kimoja (1) cha COVID-19 nchini humo. Nchi hiyo imekwisha ripoti visa vitatu (3) hadi hivi sasa.
 
Hali ni mbaya Italy
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vyote nchini humo vimefikia 847 hadi sasa ambapo wagonjwa wawili (2) wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 17 wakipata ahueni.

Hadi sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kile kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
Dogo wa hapo juu chenga ndio maana nimempa jibu kulingana na uwezo wake wa kufikir, anauliza nimepataje mil 5 jibu ni kubet aende akabeti aone

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana jamaa hukumuelewa alimaanisha yakwamba unge endelea nabiashara hio hio uloanza nayo ambayo imekupelekea kuipata Hio Million Tano Jamaa Nilivyomuelewa Mimi Hakua Namaana Mbaya Ila Alikusudia Uifanze Biashara Ilokupatia Awali M5

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Italia

Visa vipya 1,492 pamoja na vifo vipya saba 133 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 7,375 huku wagonjwa wapatao 462 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 622 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia 366 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Barani Afrika

1. Kisa kipya kimoja (1) kimebainika nchini Tunisia. Watu takribani 1000 wamewekwa karantini nchini humo wakihofiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

2. Misri imethibitisha kisa kipya kimoja (1) ambacho pia ni kifo cha kwanza kabisa kinachohusishwa na COVID-19 nchini humo na barani Afrika kwa ujumla.

3. Algeria imeripoti kisa kipya kimoja (1). Mpaka sasa nchi hiyo imekwisha ripoti visa vipatavyo 20 huku visa 17 kati ya hivyo ni ndugu wa familia moja walioambukizana.
 
UPDATE: Kifo cha kwanza nchini Misri na Afrika

Kisa hicho katika umri wa miaka 60, raia wa Ujerumani, aliingia nchini Misri mnamo Machi 1. Alilazwa hospitalini kutokana na homa mnamo Ijumaa kisha hali yake kuridhisha lakini mnamo Jumamosi aliripotiwa kuugua Nimonia kisha kufariki dunia mnamo Jumapili, Wizara ya afya imeeleza.
 
UPDATE: Italia

Visa vipya 1,492 pamoja na vifo vipya saba 133 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 7,375 huku wagonjwa wapatao 462 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 622 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia 366 hadi hivi sasa.
mh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Italia

Visa vipya 1,492 pamoja na vifo vipya saba 133 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 7,375 huku wagonjwa wapatao 462 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 622 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia 366 hadi hivi sasa.

Italy hali mbaya, wajifunze kwa wachina wanacontrol vipi kasi ya maambukizi, Wachina population yao 1.4B lakini maambukizi yao Hayakuwahi kufika kwenye 4digit kwa siku.
Sasa Italy yenye population 60.4M wanapata maambukizi makubwa kiasi hiki kwa siku hii ni Hatari sana.
 
Back
Top Bottom