Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

CORONA INAUSOGEZA ULIMWENGU KWENYE NADHARIA YA MWISHO WA DUNIA

VIRUSI vya Corona ni sehemu ya kundi la virusi ambavyo husababisha maradhi kwa mamalia na ndege. Virusi hivyo hushambulia njia ya upumuaji, hivyo kumsababisha mwathirika hali ya kikohozi, mafua, homa kali, upumuaji wa shida na hali ikizidi mgonjwa hupata nimonia.

Virusi vya Corona mara nyingi humsababishia mwathirika hali ya mafua ya kawaida (common cold), ila katika kesi chache, hufanya mashambulizi makali na hata kusababisha kifo.

Mpaka sasa virusi vya Corona ambavyo ni hatari sana na kusababisha kifo vipo katika aina nne; SARS, MERS, COVID-19 na NCOV.

SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome), ni homa ya mafua makali kutokana na Virusi vya Corona. SARS ilipogundulika Novemba 2002, Kusini ya China, kesi zaidi ya 8,000 ziliripotiwa na watu 774 waliripotiwa kufariki dunia kutokana na SARS. Kati ya Novemba 2003 na Julai 2003, SARS iliripotiwa kufika katika 17 duniani. Tangu mwaka 2004 hakuna mgonjwa mwingine wa SARS aliyeripotiwa.

Hata hivyo, mwaka 2017, wanasayansi waligundua virusi vya Corona vyenye kusababisha SARS kwenye popo, jimbo la Yunnan, China.

MERS (Middle East Respiratory Syndrome), au kwa umaarufu ni Homa ya Camel. Ukiita Mafua ya Mashariki ya Kati sio vibaya. MERS ni ugonjwa wenye kusababishwa na Virusi vya Corona. Uligundulika kwa mara ya kwanza Saudi Arabia mwaka 2012 na mpaka mwaka 2017, kesi takriban 2000 zilisharipotiwa. Asilimia 36 ya watu walioripotiwa kupata maambuziki ya MERS walifariki dunia.

COVID-19 (Coronavirus Disease 2019). Hili ndilo janga jipya linaloitesa dunia kwa sasa. Ni mwendelezo uleule wa mashambulizi makali ya Virusi vya Corona.

COVID-19 kama ilivyo kwa virusi vingine vyote vya Corona, asili yake ni maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

NCOV (Novel Corona Viruses), kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Januari 21, mwaka huu, mgonjwa wa kwanza mwenye NCOV aligundulika Jamhuri ya Korea (Korea Kusini). Aliyegundulika ni mwanamke raia wa China mwenye umri wa miaka 35. Mkazi wa Wuhan, Hubei, China.

Kwa kifupi, Virusi vya Corona vipo kwenye kundi la Zoonotic, asili yake ni wanyama. Zoonotic au Zoonosis ni maambuzi ya kibakteria, virusi na pasarasaiti, kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine, Virusi vya Corona hambukizwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye Corona akikohoa jirani na asiyekuwa na virusi hivyo, kisha asiyekuwa navyo akivuta hewa ndani, uwezekano wa kupata maambukizi ni mkubwa. Njia hiyo inaitwa respiratory droplets.

Njia ya pili ambayo inaelezwa na wataalamu mbalimbali duniani ni kugusana au kukaribiana kwa angalau futi sita na mwathirika wa Virusi vya Corona. Uwezekano wa maambukizi ni zaidi ya asilima 50.

CORONA INAVYOENEA

Mpaka jana (Machi 12), watu zaidi ya 125,000 walikuwa wameshaambukizwa COVID-19 katika nchi 80 duniani. Kati ya hao, watu 4,600 walishafariki dunia. Watu 68,000 wameripotiwa kupona COVID-19 duniani kote. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Kituo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha John Hopkins, kilichopo Baltimore, Maryland, Marekani.

Mpaka sasa hakuna kinga wala tiba ya COVID-19. Kwa mujibu wa madaktari wa China ambako maambukizi ni makubwa na vifo ni vingi, kupona kwa mgonjwa mwenye COVID-19, hutegemea uimara wa kinga za mwili wa mwathirika.

Kwamba idadi kubwa ya watu wanaopona COVID-19 wanabebwa na uimara wa kinga zao kuliko matibabu wanayopatiwa. Na hilo ni angalizo kuwa kwa mtu ambaye kinga za mwili wake zina shaka au anaumwa maradhi mengine, anapoambukizwa COVID-19, uwezekano wa kupona ni mdogo sana.

ATHARI YA KIUCHUMI

Taasisi ya utafiti ya Brookings ya Marekani, imetoa taarifa ya jinsi biashara ya mafuta ulimwenguni inavyopitia kwenye kipindi kigumu.

Jukwaa la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), limetoa taarifa kuwa COVID-19, imesababisha anguko la kiuchumi ulimwenguni kwa dola trilioni moja (zaidi ya ya Sh2,300 trilioni) mpaka sasa. Hiyo ni hesabu ya mwaka huu, yaani kipimo cha kuanzia Januari 2020.

UNCTD wameongeza kuwa kasi ya kutanuka kwa maambukizi ya COVID-19 na tahadhari kubwa zinazochukuliwa kati ya nchi na nchi ili kujikinga na maambukizi mapya, inaelekea kuisababishia dunia anguko la kiuchumi la dola trilioni 2 (Sh4,600 trilioni).

Kwa mujibu wa UNCTAD, anguko la uchumi duniani linalosababishwa na kasi ya kusambaa kwa COVID-19, linaulekeza ulimwengu kwenye Nadharia ya Mwisho wa Dunia (Doomsday Theory), inayoeleza kuwa dunia itakuwa ukingoni pale ukuaji wa uchumi duniani utakapofikia asilimia 0.5.

Hadi sasa, ukiachana na athari kubwa ya biashara ya mafuta, kwa jumla, biashara za uagizaji na usafirishaji (importation and exportation), imeshuka kwa kiasi kikubwa ulimwenguni.

Hata hapa Tanzania, vilio ni vingi sana. Kariakoo wafanyabiashara wenye kutegemea bidhaa kutoka China wanaumia. Bidhaa zinakwisha lakini hawawezi kuagiza.

Kampuni za usafirishaji mizigo (logistics) kati ya Tanzania na China au nchi yoyote iliyowekwa kwenye karantini kwa sababu ya COVID-19, zipo kwenye sintofahamu, kazi zimesimama. Uchumi unasimama.

Kwa vile Kariakoo imekuwa ikitumika kama kituo kikuu cha manunuzi ya jumla hasa mavazi kwa nchi karibu zote za Maziwa Makuu, na kwa vile biashara za Kariakoo zinategemea China, na kwa kuwa China hakuendeki kwa sasa, mpaka hapo unaweza kupata picha kubwa ya namna uchumi wa dunia unavyopitia kupindi kigumu.

Hali ndio ipo hivyo karibu kila nchi ya Afrika, maana biashara nyingi za bidhaa Afrika zinategemea China kwa kiasi kikubwa. Hali inaendelea hivyo duniani kote, uagizaji na usafirishaji bidhaa nje ya nchi vimesitishwa katika mataifa mengi.

Uchumi wa michezo ni zahama. Mpaka sasa ligi kubwa tano kwenye nchi tano za Ulaya zimesimamishwa. Kutoka England mpaka Hispania. Ufaransa hadi Ujeruma. Italia pia.

Kabla ya hapo, ilishashuhudiwa baadhi ya michezo ikichezwa bila mashabiki. Lengo likiwa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya COVID-19.

Baraza la Vyama vya Soka Ulaya (Uefa), limeahirisha mechi za mashindano yake ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League, lengo ni lilelile, tahadhari dhidi ya COVID-19. Wakati uamuzi huo ukitolewa, tayari baadhi ya wachezaji na makocha walikuwa wameshaambukizwa.

Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), kimeahirisha msimu wa mashindano ya NBA baada ya mchezaji Rudy Gobert, kukutwa na maambukizi. Gobert anachezea timu ya Utah Jazz ambayo ni memba wa Conference ya Magharibi.

Mapendekezo yametolewa kwa Ligi ya American Football (NFL) kusogezwa mbele, na wakati huohuo michezo ya vijana chini ya umri wa miaka 16, imefutwa na haitachezwa tena. Ni kwa sababu COVID-19 imekuwa tishio la dunia.

Nchi za Ulaya, inaelezwa maduka yanabaki tupu. Bidhaa zinakwisha, watu wananunua kwa wingi na kuhifadhi ndani kusudi wasitoke nje kukwepa COVID-19. Bahati mbaya zaidi, bidhaa hasa za chakula zimegeuka adimu. Hofu ya watu kukosa chakula ni kubwa.

Dunia inachapika mno kiuchumi. Taa nyekundu inawaka kuelekea kwenye poromoko la kiuchumi kwa thamani ya dola 2 trilioni. Tusiombee ufike wakati uchumi uwe unakua kwa kasi ya asilimia 0.5. Ikifika hapo ni kutimia kwa nadharia ya mwisho wa dunia, yaani Doomsday Theory.

Tuombe maambukizi yasiendelee kwa kasi iliyopo. Ni hatari mno kiuchumi. Tuombe udhibiti kwa wagonjwa wenye COVID-19, wapone bila kuambukiza wengine.

Ndimi
Luqman Maloto mwandishi
Umetia chumvi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama upo moshi ni siku kadhaa utakua Chuga. Ngoja nikusanye muvi na series kibao niwe naangalia tu karatini
mkuu chukua fash yangu nenda kona ya nairobi mwambie Murphy ai-format afu ajaze muvi mpya mpya🎥🎥🎥🎥



then tukutane karantini😂😂😂😂😅😅😅
 
Siangaliagi za kutafsiriwa mkuu. Kuna mshikaji kona nairobi juu ya ofisi yake kuna poster ta Creed II ndio hua naenda ananiwekea
ukihitaji ambazo hazijatafsiriwa pia hua zipo





tukutane karantini😷😷😷😷
 
Vipi ukipata hivyo virus unaweza kupona?. Wapo waliopitia hiyo madhira amepona?

Sent using Jamii Forums mobile app
Matibabu hufanyika kwa wenye dalili za virusi hivyo.

Dalili hizo hutibiwa kwa usaidizi maalumu katika mifumo ya mwili hususani mfumo wa upumuaji pamoja na viungo vya mwili vyenye dalili za kushindwa kufanya kazi vizuri.

Kwa lugha nyingine matibabu hayo hujulikana kama 'supportive care'.

Tiba kamili ya COVID-19 bado haijapatikana.
 
Watanzania inabidi tujielimishe kadiri tunavyoweza...

Kwa mnaowezq ifikia youtube, tafute documentaries zinazoonesha namna watu waliopo sehemu zenye maambukizi wanavyojiepusha...

Juzi nilikuwa natazama blogger mmoja Mrusi kaweka vblogg yake akiwa Wuhan, namna ambavyo mji umegeuka kuwa ghost town, watu wana hofu ya kugusa hadi buttons za elevators kiasi kwamba wanatumia vijiti vya toothpick...
 
UPDATE: Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 11 sanjari na vifo vipya 13 nchini humo.

Hubei pekee, kumeripotiwa visa vipya 7 huku vifo vyote 13 vikitokea pia mkoani humo.

Mpaka sasa, China imeripoti visa 80,824 vikiwemo vifo 3,189.

Wagonjwa wapatao 65,541 mpaka sasa wametibiwa dalili za COVID-19 na kupata ahueni.

Hivi sasa, wagonjwa wapatao 3,610 wako katika hali mbaya zaidi.
 
Vipi ukipata hivyo virus unaweza kupona?. Wapo waliopitia hiyo madhira amepona?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na exposureya virusi hivyo sio kuwa ni ugonjwa, isipokuwa dalili za magonjwa yanayofanana na hali ya mafua mtu ataanza yapata pale kinga za mwili zitapoanza kupambana na uvamizi wa virus...

Kwa watu wenye kinga nzuri, baada ya muda mfupi unarudi kuwa sawa...

Kwa walio na kinga ya chini, hawa virusi hupelekea mtu kuwa na 'nimonia' (pneumonia) na wanaofika stage hii na kuendelea ndio wanaopoteza maisha...
 
UPDATE: Iran

Visa vipya 1,365 vimeripotiwa hivi punde nchini humo sanjari na vifo vipya 97.

Ongezeko hilo linapelekea idadi ya visa vyote nchini humo kufikia 12,729 huku idadi ya vifo ikifikia 611 hadi sasa.

Waliopata ahueni wafikia 4,339 huku kukiwa na uwezekano wa visa vipya kuongezeka zaidi.
 
Kuwa na exposureya virusi hivyo sio kuwa ni ugonjwa, isipokuwa dalili za magonjwa yanayofanana na hali ya mafua mtu ataanza yapata pale kinga za mwili zitapoanza kupambana na uvamizi wa virus...

Kwa watu wenye kinga nzuri, baada ya muda mfupi unarudi kuwa sawa...

Kwa walio na kinga ya chini, hawa virusi hupelekea mtu kuwa na 'nimonia' (pneumonia) na wanaofika stage hii na kuendelea ndio wanaopoteza maisha...
Bado hujanijibu mkuu. “ukiwa na kinga nzuri baada ya muda unakuwa sawa”. Unakuwa sawa ndio kusemaje? Kupona ama kuacha mafua,lakini virus bado unavyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matibabu hufanyika kwa wenye dalili za virusi hivyo.

Dalili hizo hutibiwa kwa usaidizi maalumu katika mifumo ya mwili hususani mfumo wa upumuaji pamoja na viungo vya mwili vyenye dalili za kushindwa kufanya kazi vizuri.

Kwa lugha nyingine matibabu hayo hujulikana kama 'supportive care'.

Tiba kamili ya COVID-19 bado haijapatikana.
Kwa hiyo huo usaidizi una maana gani mkuu?. Ni sawa na kuongeza kinga mwilini tu,lakini utakufa au ikoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado hujanijibu mkuu. “ukiwa na kinga nzuri baada ya muda unakuwa sawa”. Unakuwa sawa ndio kusemaje? Kupona ama kuacha mafua,lakini virus bado unavyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa sawa/timamu maana yake kinga ya mwili imeweza kuvikabili virusi na mtu kupona kabisa...

Kuna watu ambao wanapona kabisa, maambukizi yanaondoka mwilini mwao...

Kuna kitu kimoja sijajua vizuri bado, naendelea kufuatilia. Nacho ni iwapo mtu aliyepona je mwili utatengeneza kinga ya kudumu au maambukizi yanaweza mrudia tena akiwa exposed!
 
Kuwa sawa/timamu maana yake kinga ya mwili imeweza kuvikabili virusi na mtu kupona kabisa...

Kuna watu ambao wanapona kabisa, maambukizi yanaondoka mwilini mwao...

Kuna kitu kimoja sijajua vizuri bado, naendelea kufuatilia. Nacho ni iwapo mtu aliyepona je mwili utatenheneza kinga ya kudumu au maambukizi yanaweza mrudia tena akiwa exposed!
Asante mkuu. Fuatilia mpaka mwisho nijulishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na report kamaili ni yanaweza kukurudia
Na yakikurudia ni hatari zaid
Ni kama mafua, inaweza kukurudia kama kawaida
Kuwa sawa/timamu maana yake kinga ya mwili imeweza kuvikabili virusi na mtu kupona kabisa...

Kuna watu ambao wanapona kabisa, maambukizi yanaondoka mwilini mwao...

Kuna kitu kimoja sijajua vizuri bado, naendelea kufuatilia. Nacho ni iwapo mtu aliyepona je mwili utatengeneza kinga ya kudumu au maambukizi yanaweza mrudia tena akiwa exposed!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 609 pamoja na vifo vipya 58 vimeripotiwa nchini humo hivi punde.

Mpaka sasa, idadi ya visa vyote nchini humo imefikia 5,841 huku vifo vikifikia 191.

Serikali ya nchi hiyo imepanga kufungwa kwa nchi nzima kuanzia Jumatatu asubuhi wiki ijayo ili kupunguza na kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
 
Kwa hiyo huo usaidizi una maana gani mkuu?. Ni sawa na kuongeza kinga mwilini tu,lakini utakufa au ikoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo usaidizi ama kwa kitaalamu 'Supportive care' unafanyika kwa wagonjwa wenye dalili za COVID-19 na hujumuisha mambo yafuatayo;

1. Uongezwaji wa maji ndani ya mwili ili kukabiliana na upungufu wa maji mwilini.

2. Usaidizi wa kupumua kwa kutumia vifaa maalumu (oksijeni).

3. Usaidizi katika viungo ama ogani za mwili (vital organs) zenye dalili za kushindwa kufanya kazi; mapafu, figo, ini, moyo n.k. kwa kutumia vifaa maalumu vya kitabibu.

4. Mchanganyiko wa dawa mbalimbali ili kutibu hizo dalili. Dawa zinazotumika ni zile zitumikazo kutibu maradhi mengine kama vile Ebola n.k.

Kinachotibiwa ni dalili tu ila kirusi kinaendelea kuwepo ndani ya mwili maana bado hakuna dawa ya kuweza kukiangamiza kabisa isipokuwa ni uwezo wa mwili wa mgonjwa kuweza kuvithibiti virusi hivyo ili visishambulie mwili na kuleta tena dalili.

Pia, kuna wanaopona dalili hizo lakini kwa mujibu wa tafiti zilizopo, wanaweza kubakia na matatizo mengine ya kudumu katika mifumo yao ya mwili ama ogani zao kutokana na madhara yaliyosababishwa na virusi hivyo isitoshe pia kuna visa vya watu kuambukizwa tena ama kwa mara nyingine.

Bado utafiti zaidi unaendelea kuhusiana na kirusi hiki pamoja na tabia zake maana kuna mambo mengi yahusuyo kirusi hiki bado hayajafahamika kitaalamu.
 
Back
Top Bottom