Hii itakua unpopular opinion ila nitasema ninachofikiri.
Pasi na chembe ya shaka Covid-19 ni ugonjwa hatari ila, kwa mawazo yangu, dunia nzima ime overact na jinsi ya kukabiliana na huu mlipuko.
Kinachoendelea sasa ni mashindano ya kutoa takwimu za waathirika na kutishana. Bado death rate ya corona sio ya kutisha sana kiasi cha kufanya shughuli zingine zote zisimame. Ikumbukwe watu walikua wanakufa kabla ya corona na wataendelea hata baada ya corona, it's the circle of life. Sasa kila anayefariki ni corona magonjwa mengine yote yamepotea ghafla. Hata mimi nikifa kwa corona hakuna sababu ya maisha ya wengine kusimama.
Nadhani kuchukua tahadhari tu ingetosha ila sio kusimamisha maisha ya watu juhudi ambazo hazionekani kuzaa matunda yoyote, mwishoe watu watasema potelea mbali na kurudi makazini. Dawa au chanjo ya corona isipopatikana hadi mwakani watu wataendelea kukaa ndani mwaka mzima?
Sasa bongo nao watu wanataka kila kitu kisimame sababu corona imeua watu watano toka ianze, really? I can assure you malaria imeua wengi zaidi ya hao in the last 24hrs.
According to Wikipedia,
Mortality rate - Wikipedia, inakadiriwa watu laki moja na nusu hufa kila siku kwa sababu mbali mbali duniani. Sasa iweje corona iliyoua watu karibu watu laki moja na nusu kwa miezi mitatu isimamishe dunia.
www.worldometers.info/coronavirus/
Confirmed
2,173,432 | Recovered
554,786 | Deaths
146,291 |
Media nyingi zinatoa idadi ya vifo na waathrika wapya tu hawasemi wangapi wamepona. Nia ni kujazana hofu.
Come June maisha yataendelea aidha chanjo imepatikana au lah, vinginevyo we're facing economy Crashdown beyond repair. Kilichofanyika so far ni kuua sisimizi kwa nyundo.