Fahamu kiundani kabila la Wapare na Wanawake wa kipare

Fahamu kiundani kabila la Wapare na Wanawake wa kipare

Nadhani utafiti wa DNA unaweza kufafanua zaidi uhusiano au unasaba wa matawi ya kabila la wapare na pia ukaribu wao na makabila mengine ya jirani kama wachaga na wasambaa nk.
Historia imeandikwa vizuri - shukurani mtunzi.
 
Sikuwahi kujua kama wapare wana historia nzuri hivi japo ni watani wangu .
Mara nyingi huwa tunasikia na kusikilishwa upande wa ubaya tu kumbe kuna mengi mazuri hatusikilizishwi kutoka kwao.

Nimefurahi pia kusia wapare wana majina yanayoshabihiana na Wachagga, huwenda tuna undugu wa damu baina yetu ila hatujui tu.


Miaka ya nyuma kulikua na soko au gulio maeneo ya Uchira , pale tulikua tunaenda kupeleka bidhaa kutoka uchagani kama ndizi maharagwe mahindi na vingi kwenda kubadilisha na magadi, yaani sisi tulikua tunatoa labda maharage kiasi fulani wao wanatupa magadi.

Kule uchagani magadi yalikua yanathamani sana ila kila familia haikosi magadi kwaajili ya mifugo, kiungo cha chakula au dawa haswa tumbo.
Sehemu pekee yaliyopatikana magadi ni upareni, na soko maalum ni hilo la uchira.

Nilikua naona wakina mama wa upareni wamebeba magadi karibu gunia nzima peke yake, walikuwa na nguvu sio kidogo, ingawa kwa sasa sijui kama huo mtindo wa kubadilishana bado upo.
 
Nishawahi kukaribishwa msosi na mpare, nilikuta makande yamepikwa kwa mahindi, maharage,njegere, njugumawe na mchicha😄
Nilitamani kusema sili cz huo mchanganyiko sio poa! Nikajikaza kijiko cha kwanza tu Makande matamu balaaaaaaaaaa!

Kilichofata nilipiga plate 2.
 
Back
Top Bottom