Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakati huu,
Mwaka 2003 nilibahatika kuhudhuria mnada wa mtu aliyeshindwa kulipa DENI. Mnada huu ulifanyika huku familia ikiwa ndani ya nyumba kwa mkopo ambao BABA alichukua kwa ajili ya biashara na akashindwa kulipa. Kwanza tukio lile lilinishangaza sana kwani lilikuwa la kufedhehesha, kudhalilisha na lilionesha kutokujali kwa aina yoyote. Kwanza nyumba iliuzwa kwa bei ya chini kuliko thamni yake na pili uuzwaji ulifanyika bila kuzingatia utu na staha. Tukio lile lilinifanya nikajifunza mambo mengi sana. Kwanza niligundua ni vibaya sana kuingia kwenye mkopo bila kushirikisha wana familia wote. Pili nilijifunza ni vibaya sana kuingia kwenye mkopo na kuweka aseti ya familia kama nyumba wanao wanayoishi kama dhamana. Pia nilijifunza kwamba Ukikopa bila malengo ni hatari sana.
Sasa leo natka niwaeleza fursa ndogo ya kibiashara ambayo imejificha katika madeni nayo ni Biashara ya kuuza na kununua madeni. Sio biashara ya kukusanya madeni bali ni kununua na kuuza madeni. Watu wengi hufanya mchezo huu kwa kwenda kukopa sehemu moja ili kulipa sehemu nyingine huku wakiendelea kudaiwa. Hata hivyo hufanya hivi katika mazingira magumu,ya uongo na wakati mwingine wanajikuta wakijiingiza katika RISK kubwa sana za Madeni (Debt Exposure) kutokana na kuwa katika hali ngumu.
Biashara ya kununua na kuuza madeni inaweza kufanywa na watu gani? Hii inaweza kufanywa na wakopaji na wakopeshaji. Mkopeshaji anaweza kuwa amekopesha pesa nyingi kiasi kwamba ama anajikuta mikopo yake ahaifanyi kazi vizuri na akajikuta anata kupunguza mzigo wa gharama kwa kuwauza wadaiwa wake kwenda kwa mtu mwingine. Mkopaji anaweza kuwa anadaiwa ila anataka kubadili terms za malipo ili apate nafuu na aliyemkopesha hana uwezo kufanya DEBT restrucuring (Kurekebisha mkataba wa mkopo) na hivyo kujikuta anahitaji nafuu katika terms za malipo.
Soko hili la madeni anaweza kwenda yeyote, mkopaji au mkopeshaji na kuweka deni lake sokoni na terms zake. Mfano mkopo wako ni wa milioni kumi ndo unadaiwa ila uko tayari kuliuza kwa milioni 11 atakayenunua atalipa milioni kumi unakodaiwa na atakupa kipindi kingine cha ziada kulipa hio milioni 11 ambapo faida yake itakuwa milioni 1. Kama wewe ni mkopeshaji unaweza upa mkopo discount mfano una mdai mtu milioni 10 basi unauza deni kwa milioni 9 kisha yule mnunuaji anamuongezea muda yule anayedaiwa na anatengeneza faida ya milioni 1.
Soko hili la madeni litawafaa sana wafanyabiashara ambao wameelemewa na mzigo wa madeni ambao unaathiri kwa kiwango kikubwa uwezo wao kujiendesha kwa faida na hivyo wanahitaji msaada.
Jambo hili tayari linafanyika ingawa adoa halijawa maarufu kwa hapa nchini lakini ni jambo ambalo lipo na linawezekana kuwa biashara kama biashara nyingine.
Karibu tujadili kuhusu biashara hii na nama ambavyo tunaweza kuitumia kama fursa.