Usafi wako, mapishi bora, kauli nzuri, boresha Huduma utofautiane na jiran zako kama sahani ya wali nyama ni elf 2 wewe uza bei hio halafu weka na tunda pemben hata kama ni ndizi unaigawa Mara mbili au chungwa moja unagawa Mara NNE kuonesha utofauti na wengine
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanzo mzuri mkuu...Kichwa cha habari hapo juu chahusika,
Nataka kuanzisha biashara ya 'Mama Ntilie' nina mtaji wa milioni moja hivi, kodi hapohapo.
Nimefanikiwa kuzunguka na kupata fremu ya 150,000 kwa mwezi amekubali nilipie kwa miezi mitatu, fremu ipo kwenye mzunguko wa watu ni maeneo ya Bunju B, nailipia jumamosi
Msichana msafi na mchangamfu ninaye labda atafute msaidizi.
Cha kuzingatia sijawahi kufanya biashara kabla wadau nakaribisha mawazo yenu kama kuna kitu cha kuzingatia nlichosahau hapo
Mwanzo mzuri mkuu...
Angalia tu binafsi kero zangu tu nikupe huenda ukazifanyia kazi.
Napenda chakuka kitamu, hasa wali hakikisha unatafta mchele mzuri na wenye ladha.
Uharaka wa huduma huwa sipendi nimefika then sisikilizwi, wahudumu wawe shapu,
Mambo ya mtu umeagiza supu then chapati za kusubili hiyo wengi hatupendi aisee.
Tafta na friji weka juisi, soda na maziwa mtindi kama kuna wapenzi nayo kama mimi.
Staha epuka maneno yanatayokushushia heshima, but tarajia maneno ya kukera kutoka kwa wateja.
Sent from my Nokia 6 using Jamii Forums mobile app
Mammbo ya kuzingatia unapoanzisha biashara ya chakula:-
1. Usafi wa watu/mtu na mahala pa kufanyia kazi (hili ni muhimu mnooo)
2. Kujua bei za bidhaa, kujihimu kudamka sokoni (masoko makuu) Nazi ya kawaida unaweza kuinunua kwa shilingi 1,500 mda wa kawaida, lakini ukidamka sokoni unaipata kwa mia saba ama elfu moja.
3. Kujua aina ya wateja waliokuzunguka na wanataka nini. Huwezi kupiga mchele kwenye eneo la wasukuma wengi.
4. Kujali maslahi ya wafanyakazi wako na kuwa na ukaribu nao
5. Kuwa na tabia ya kudamkia Feri siku za weekend, kusanya stock ya wiki nzima badala ya kununua rejareja (feri utajifunza meng)
6. Ubunifu na ucheshi kwa wateja
Unafungua Biashara wewe hata kusimamia mwezi haupo, unatkiwa mwanzo wa biashara uwepo ndo unamkabidhi mtu ili ujue muenendo mzima wa biashara, hivi unajua hata kilo moja wali unatoka sahani ngapi? ratio ya kg za nyama na wali? mimi naona biashara hii fungua ukiwepo ukishajua ndo umkabidhi huyo dada, la sivyo million inateketea au omba mtu awepo hapo badala yako.
Itakushinda kama utaanza hiv dada angu,nikwambie ukwel tuu...Ntamwachia ntapitia hesabu coz mda mwingi ntakua kibaruani
Kama ni hivi, inakupasa uwe makini sana. Tena ingekuwa ni vema kama ukaanza kwa kukaa mwenyewe, ili ufahamu biashara yako ina mzungo wa kiasi gani minimum and maximum.Ntamwachia ntapitia hesabu coz mda mwingi ntakua kibaruani
Sawa.Sawa huyo Dada namjua na utendaji kazi wake na uaminifu wake naujua pia, akinidanganya ntajua pia na akija kubadilika ntajua pia. Sio mgeni kwangu
SawaSawa huyo Dada namjua na utendaji kazi wake na uaminifu wake naujua pia, akinidanganya ntajua pia na akija kubadilika ntajua pia. Sio mgeni kwangu