Cataliyya
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 781
- 371
Kichwa cha habari hapo juu chahusika, nataka kuanzisha biashara ya mama ntilie nna mtaji wa milioni moja hivi kodi hapohapo, nimefanikiwa kuzunguka na kupata fremu ya 150,000 kwa mwezi amekubali nilipie kwa miezi mitatu, fremu ipo kwenye mzunguko wa watu ni maeneo ya bunju b, nailipia jumamosi, msichana msafi na mchangamfu nnaye labda atafute msaidizi. Cha kuzingatia sijawahi kufanya biashara kabla wadau nakaribisha mawazo yenu kama kuna kitu cha kuzingatia nlichosahau hapo