Habari zenu wanajamvi, kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wanajamvi kwa mawazo yenu chanya ya kibiashara yaliyoniwezesha kuanzisha baadhi ya miradi ambayo mpaka sasa inaendelea vizuri.
Bila kuwachosha ngoja niende kwenye mada husika Kwa sasa ninataka kupanua miradi yangu na kuingia kwenye biashara ya chakula, yani mgahawa ambapo nitabase katika vyakula vya chips, ugali na wali pamoja na mboga tofauti tofauti, kwa upande wa eneo nafahamu ni kwamba panatakiwa kuwa na mzunguko wa watu km vile chuo au biashara tofauti tofauti.
Kwa mtu nayeanza ningependa kufahamu mtaji unaohitajika ili kuweza kuanzisha biashara hii(vifaa) , mauzo kwa siku,uendeshaji pamoja na changamoto zake.
NB:nataka niweke kijana wa chipsi na mabinti wawili wa chakula cha kawaida ila nitakwepo muda wote kusimamia shughuli za uendeshaji pia sehemu nategemea itakuwa ya kawaida yani sio ya mtaji mkubwa.
Asanteni