Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Laki 4 kwa maisha ya kijana mtanzania wa siku hizi hapo niparefu jamaa yangu
Sidhan kama upo serious. Vijana unaowatetea wanasmartphone za hadi laki tano,wananunua bando kila siku. Kwa kufupi inawezekana kuanza na mtaji mdogo. Mfano mimi nilifungua mgahawa kwa sh laki tisa tu na hapo nikiwa nmelipa kodi ya chumba miez 3 na kununua kila kitu. Na mgahawa huo ulinipatia sh. Elfu kumi kila siku ambayo nachukua sh 70,000/ kila jumapili hii ni sawa na sh. 280,000/ kwa mwezi hapo utashindwaje kulipa ada za shule kwa watoto? Shida ni kwamba wengi wetu hasa tuliajiriwa hizi biashara ndogo ndogo tunaziona ujinga.
Nikupe mfano mwingne kilo moja ya unga sh 1,400/ inatoa chapati za sh. 5,000/ zile chapati za 2 miatano so ukiuza supu na chai asubuh,mchana wali na ugali na ukakomaa mwenyewe baada ya miaka miwil unafungua hotel
 
Hapo unazungumzia mazingira ya uswahilini,huku ushuani watu wanahitaj kula kwenye mandhari nzuri,sehemu safi na iliyotulia,meza na viti safi,luninga na kamziki kidg,hapo bei ya frem ujipange,Anyway wazo zuri kutekelezeka USWAZI
 
ommy15,
Kweli hayupo serious, simu anayotunia utakuta S8 ya mil 1 na,..... Mtu anasimu ya mil2 analalamika kupa mtaji wa laki 5 tu???...... Alafu simu haainguzi kitu....
 
Hakuna suppliers watakaokuambia hili
Inabidi wewe mwenyewe uende kwenye mahoteli na kuonana na wenye mali



Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom