Fahamu kuhusu Bullying na jinsi wazazi wanavyochangia kutokea kwa unyanyasaji huu unaowaathiri sana watoto wawapo shuleni

Fahamu kuhusu Bullying na jinsi wazazi wanavyochangia kutokea kwa unyanyasaji huu unaowaathiri sana watoto wawapo shuleni

Zawadi Mkweru

Member
Joined
Jan 11, 2017
Posts
5
Reaction score
19
Bullying ni aina ya Unyanyasaji unaoweza kufafanuliwa kama shambulio la kisaikolojia, kimwili au vitisho ambalo hulenga kusababisha woga, mawazo au kumdhuru mwathirika.

Bullying inapofanyika mashuleni huwa katika mazingira ambapo mwanafunzi hujikuta katika unyanyasaji wa kimfumo (pamoja na wigo wa jumla) kutoka kwa mwanafunzi mmoja au zaidi, kwa nia ya kumuumiza.

Tafiti mbalimbali zinahusisha Bullying na matatizo ya kisaikolojia ambayo husababishwa na matukio mengi katika maisha ya mtoto ikiwemo kukosa malezi yaliyo bora hasa kutoka kwa mzazi wa kiume au kulelewa katika familia isiyo na mahusiano mazuri baina ya wanafamilia au wazazi.

Bullying ni utesaji unaofanywa kwa kukusudia kwa lengo la kudhuru mwili, kwa maneno, au kisaikolojia. Unaweza kuanzia katika kupigwa hovyo, kuitwa majina yasiyofaa, vitisho na kejeli na hata kuporwa pesa na mali. Wengine huwanyanyasa wenzao kwa kueneza uvumi na taarifa za uongo kuhusu wenzao ili kuwadhalilisha.

Uonevu huu unaweza kutokea katika mazingira halisi au katika mtandao (Cyberbullying). Katika mtandao huweza kujitokeza katika mitandao ya kijamii, kupitia jumbe za simu, baruapepe au kwa njia yoyote ile ambayo watoto huitumia wawapo mtandaoni.

Madhara yake huweza kuwa makubwa sana kwa sababu wazazi wengi hawana desturi ya kufuatilia kinachofanywa na watoto wao pale watumiapo intaneti na hufanya mtoto kuathirika kwa kiwango kikubwa.

Utatambuaje kama mwanao anafanyiwa uonevu wa aina yoyote shuleni?
Hizi ni baadhi ya dalili zitakazokusaidia kugundua hili. Angalia kwa karibu hisia za watoto, kwa sababu watoto wengine wanaweza wasielezea wasiwasi wao kwa maneno. Ishara za kutazama ni pamoja na:

  • Mchunguze kama ana alama zozote za kuumizwa mwilini kama vile michubuko isiyoelezeka, mikwaruzo, mifupa iliyovunjika na vidonda
  • Hofu ya kwenda shule au kushiriki katika hafla za shuleni. Kuwa na wasiwasi wa mara kwa mara. Kuwa na marafiki wachache shuleni au nje ya shule au Kupoteza marafiki ghafla au kukwepa matukio ya kijamii
  • Kupoteza vitu/mali zake hovyo kama Mavazi, vifaa vya elektroniki au mali zingine za kibinafsi au kuharibiwa. Kuomba pesa mara kwa mara hasa aendapo shuleni. Utendaji mdogo kitaaluma au Utoro.
  • Kupenda kukaa karibu na watu wazima. Kupata usingizi usio na utulivu hasa kwa kuota ndoto mbaya/kutisha. Kulalamikia maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo au magonjwa mengine ya mwili
  • Kuwa na usiri isio wa kawaida, haswa linapokuja suala la kujua shughuli anazozifanya mtandaoni. Kuwa mkali au hasira za ghafla.

Ufanyeje unapogundua mwanao anapitia unyanyasaji wa aina hii.
Bullying huleta matokeo mabaya na mengine huwa ni ya muda mrefu kwa watoto. Mbali na athari za kiafya zitokanazo na uonevu, watoto wanaweza kupata shida za kihisia na kiakili, pamoja na msongo wa mawazo na wasiwasi, ambazo zinaweza kusababisha utumiaji wa dawa za kulevya na kupungua kwa utendaji shuleni.

Mtoto wako ana haki ya kuwa salama katika mazingira ya shule ambayo inaheshimu hadhi yake.
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto unasema watoto wote wana haki ya kupata elimu, na ulinzi kutoka kwa kila aina ya unyanyasaji wa kimwili au akili, jeraha. Unyanyasaji ni ubaguzi.


Hatua ya kwanza ya kumfanya mtoto wako awe salama, kimazingira na hata mtandaoni ni kuhakikisha anajua vema kuhusu Bullying
  • Wafundishe watoto wako juu ya uonevu. Mara tu wanapofahamu Bullying ni nini, watoto wako wataweza kuutambua kwa urahisi, ikiwa unatokea kwao au kwa mtu mwingine.
  • Zungumza kwa uwazi na mara kwa mara na watoto wako. Kadiri unavyozungumza na watoto wako juu ya uonevu au unyanyasaji unaoweza kuwapata, watakuwa huru kukujulisha ikiwa wataona au kukumbana na uonevu wa aina yeyote.
  • Wafundishe kuwa na mitazamo chanya na kuwa mfano bora na wa kuigwa wawapo shuleni. Bullying huwa na sehemu 3: mwathirika, mnyanyasaji, na mtazamaj. Mfundishe mtoto wako kuwatetea wengine pale anapoona uonevu ukifanyika hata kama uonevu huo haujafanyika kwake.
  • Msaidie mtoto wako kujiamini. Mhimize kujiandikisha au ajiunge na shughuli anazozipenda katika jamii yako kule shuleni. Hii pia itasaidia kujenga ujasiri na marafiki walio na maslahi ya pamoja.
  • Mzazi Kuwa mfano wa kuigwa kwa mtoto. Onyesha mtoto wako jinsi ya kuwatendea watoto wengine na watu wazima kwa fadhila na heshima, pamoja na kuongea wakati anapoona wengine wanadhulumiwa. Watoto huangalia wazazi wao kama mifano ya jinsi ya kuishi.
  • Kuwa sehemu ya maisha yake awapo mtandaoni. Jihusishe katika majukwaa au kurasa ambazo mtoto wako huzitumia mara kwa mara, mueleza jinsi ulimwengu wa kidijitali ulivyounganisha na ulimwengu nje ya mtandao, na uwaonye juu ya hatari mbalimbali ambazo watakutana nazo katika kutumia intaneti.

Je! ufanye nini endapo mwao ndiye anayewanyanyasa wenzake?
Ikiwa unahisi au unajua kuwa mtoto wako ananyanyasa wengine, ni muhimu kutambua kuwa sio jambo la kurithi, lakini anaweza kuwa anafanya hivyo kwa sababu kadhaa.

Watoto wengi ambao ni wanyanyasaji mara nyingi wanatafuta namna ya kukabiliana na hisia mbaya ndani yao. Wengine huwa ni waathiriwa au mashuhuda wa dhuluma zinazofanyika nyumbani au katika jamii inayowazunguka.



Kuna hatua kadhaa unazopaswa kuchukua kumsaidia mtoto wako kuacha uonevu:

  • Wasiliana naye ili uweze kuelewa ni kwanini anatenda hivyo na itakusaidia kujua jinsi ya kumsaidia. Je! anahisi kukosa usalama shuleni? Anapigania na rafiki au nduguye? Ikiwa wana shida kuelezea tabia yao, unaweza kuchagua kushauriana na mshauri au mtaalamu wa afya ya akili ambaye amepewa mafunzo ya kufanya kazi na watoto.
  • Muulize mtoto wako aeleze hali ambayo inamchanganya kihisia, na mfundishe njia nzuri za kukabiliana nayo.
  • Jichunguze wewe mzazi ni mambo gani unayoyafanya ambayo yanapelekea unakuwa mfano mbaya katika kumlea mwanao. Je, wanakutana na mazingira gani ya uonevu wawapo nyumbani?
  • Mfundishe namna ya kujirekebisha. Fuatilia mienendo yake na shughuli zote anazozifanya anapokuwa mwenyewe au katika makundi ya watu wa rika lake. Mhimize kuomba msamaha kwa wenzake na kutafuta njia nzuri ya kujumuika na wenzake katika siku zijazo.
Watoto wanaokutana na mazingira ya unyanyasaji majumbani wana uwezekano mkubwa wa kuyafanya matendo wanayoyaona nyumbani wawapo shuleni.

Ni muhimu kwa wazazi kujichunguza jinsi tabia zao zinavyoweza kuwaathiri watoto wao - jinsi wanavyoongea na watoto wao, jinsi wanavyoongea na wenza wao, jinsi wanavyoshughulikia hasira
 
Kujimwambafai(kileo) ama kujifaharisha.
 
Nilisema sheria za wakoloni ziletwe afrika na kuApply ndipo tunaweza kuepukana na mambo ya bullying na nduguze, vinginevyo taasisi na wadau wa kupinga hii kitu mtakula sana misaada ya kutetea bullying na nduguze.
 
Shida ipo kwa jamii zetu. Ahsante kwa kutoa elimu maana ni njia ya muhimu sana katika mapambano dhidi ya huu unyanyasaji.
 
Back
Top Bottom