Fahamu kuhusu Fao la Kukosa Ajira Tanzania (Unemployment Benefit)

Ni Faida/Msaada kwa maana ya kwamba, ukipata ajira utaendelea kuchangia pale ulipo ishia, na ikitokea amestaafu kile kiasi/kiwango ulicho lipwa hakita tolewa/punguzwa kwenye malipo ya pensheni.
Msaada kwenye Tuta..mfano nimechangia miezi 180 ambayo naona Ni miaka 15 nikaachishwa kazi...Je naweza kuingia kwenye mfumo Wa pension Hadi nakufa???
 
Hapana, baada ya kulipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho, utasubiri miezi 18+ ukitafuta ajira, ukikosa ndio utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki
Je unaruhusiwa kuchukua kiasi chote baki I mean Kuchukua rumpsum
 
Kama nimechangia miezi 180 plus nikafukuzwa kazi nikiwa chini ya umri wa miaka 55,,hapo stahiki zangu zitakuaje? Maelezo tafadhari.
 
Hapana, baada ya kulipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho, utasubiri miezi 18+ ukitafuta ajira, ukikosa ndio utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki
Je naweza kuchukua hiyo 33.3% Kwa mkupuo wa miezi 6 au ni mpaka Kila mwezi ndani ya miezi hiyo 6?
 
Elimu nzuri ila hapo tu kwenye "msaada" ndo mgogoro, zile hela ni za mwanachama na si msaada na ikipita miezi 18 unalipwa kiasi ulichochangia na wanatoa hiyo 33% ya mshahara wako waliokulipa miezi 6.
Wanaita Msaada Kwa sababu ukipata Ajira hawazikati kwamba eti ulishalipwa bali itaendelea ulipoishia.
 
Hela uliyovuta baada ya miezi 18 walikata Yale malipo ya awali ya 33.3% ndio ukalipwa kilichobaki ama ilikuaje?
 
Kwa nini wasilipe ya miezi 6 yote badala ya mwezi mmja mmja manake Haina Tija
 
Hii sheria inawaumiza watu wa Mkataba.Nimewahi fanya kazi kampuni binafsi kabla ya mambo kuvurugika awamu ya 5 ,baada ya kazi kuisha walinilipa hela zangu zote ndani ya mwezi 1 tuu ,ilikuwa PPF saizi haipo.
 
Serikali haina huruma kabisa wabunge wanalipana mafao zaidi ya 200M wakimaliza tu miaka yao 5, lakini Mtanzania anae lipwa laki 5 anaambiwa apewe 33.3% nyingine asubiri miezi 18, hii nchi hii ina viongozi wa hovyo sana , vitu vingine hata mtoto wa darasa la 7 anaweza kuwazidi akili
 
MKUU MFANO,MTU ALIKUWA ANAFANYA KAZI YA KUFUNDISHA,MKATABA UKAISHA,NA HAKUPEWA MWINGINE,BALI AKAPEWA BARUA YA KUMALIZA MKATABA NA ALIKUWA ANACHANGIA,AKIWA LABDA MKOA X.

JE,AKITAKA KUOMBA STAHIKI HIZI MPAKA AOMBEE OFISI ZA MKOA HUOHUO X AU HATA AKIWA MKOA Y ANAWEZA KUOMBEA OFISI ZA HUKO?

NA UTARATIBU WA KUOMBA HIZI STAHIKI UKOJE YAANI UNAANZIA WAPI?
 
Msaada kwenye Tuta..mfano nimechangia miezi 180 ambayo naona Ni miaka 15 nikaachishwa kazi...Je naweza kuingia kwenye mfumo Wa pension Hadi nakufa???
Kama umechangia miaka 15+ (Miezi 180) kazi ikifika Ukomo na una miaka 55+ wewe utalipwa kiinua mgongo na pensheni ya Kila mwezi mpaka kufa, lakini ukiwa chini ya miaka 55 utalipwa kwanza kiinua mgongo alafu utasubiri utaratibu wa pensheni ya Kila mwezi ukifika miaka 55
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…