Mr.Junior
JF-Expert Member
- Sep 8, 2013
- 12,454
- 11,029
🤣🤣🤣Hata kwa sababu ya kupigana kazini? Nataka nimchote ngwara mhindi wanitimue nikachote vi hela vyangu nssf nimechoka kutumwa tumwa kifala,,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣Hata kwa sababu ya kupigana kazini? Nataka nimchote ngwara mhindi wanitimue nikachote vi hela vyangu nssf nimechoka kutumwa tumwa kifala,,
Kumbe serikali haina pesa hadi inategemea pesa zetu.....!!?Siku mkija kugundua ya kuwa mafao yenu NSSF N.K Ndiyo yanayotumika kuendesha serikali...mtakuwa mmeshachelewa...
Serikali iliamua kuinganisha hii mifuko kwa sababu hii mahsusi kabisa...
Zama zilishabadilika, ishi,fanya mambo yako yote kwa asilimia 90 ya mshahara unaoupata....hiyo asilimia 10...fanya kama sadaka...
Pia una uwezo wa kuanza kwa mwajiri wako (hr) + benki, hr akaaprove mshahara wako ukatwe 10% nyingine iwe inaingizwa fixed account kwa muda na utaratibu maalum mtakaokubaliana.(mutual Consent/agreement)
Hili pekee ndilo linaweza kumuokoa muajiriwa pindi anapofukuzwa kazi.
Mkuu DOMINGO THOMAS naomba kuuliza je maternity benefits ya PSSSF yamesitishwa? Maana nimeomba tokea tarehe 13/11/2024 Hadi leo status inasomeka received by PSSSF. Nimefika kwenye ofisi zao wamesema wamepokea na zimewafikia watafanyia kazi, Ila kimya kingi Hadi leo. Naomba kufahamishwa kama lomesitishwaYou're Welcome
Sahihi, lakini ukipata kazi nyingine mpaka ukastaafu kile kiasi ulicho lipwa hakitotolewa kwenye malipo ya kustaafuElimu nzuri ila hapo tu kwenye "msaada" ndo mgogoro, zile hela ni za mwanachama na si msaada na ikipita miezi 18 unalipwa kiasi ulichochangia na wanatoa hiyo 33% ya mshahara wako waliokulipa miezi 6.
Jamaa kamchoka muhindi
Ni kwamba watu watumie mishahara yao kujiendeleza kimaisha, sio kusubiri mafaoSiku mkija kugundua ya kuwa mafao yenu NSSF N.K Ndiyo yanayotumika kuendesha serikali...mtakuwa mmeshachelewa...
Serikali iliamua kuinganisha hii mifuko kwa sababu hii mahsusi kabisa...
Zama zilishabadilika, ishi,fanya mambo yako yote kwa asilimia 90 ya mshahara unaoupata....hiyo asilimia 10...fanya kama sadaka...
Pia una uwezo wa kuanza kwa mwajiri wako (hr) + benki, hr akaaprove mshahara wako ukatwe 10% nyingine iwe inaingizwa fixed account kwa muda na utaratibu maalum mtakaokubaliana.(mutual Consent/agreement)
Hili pekee ndilo linaweza kumuokoa muajiriwa pindi anapofukuzwa kazi.
Maternity benefits ipo na haijafutwa, wanacho takiwa kukuambia ni nini kinasababisha wachelewe kukulipa, Ninacho fahamu kuhusu maternity benefits ni kwamba michango 12 kabla ya kujifungua unatakiwa uwe umechangia kwa mfululizo, je umeangalia statement ya michango yako ipo mpaka mwezi wa kumi na moja.....!?Mkuu DOMINGO THOMAS naomba kuuliza je maternity benefits ya PSSSF yamesitishwa? Maana nimeomba tokea tarehe 13/11/2024 Hadi leo status inasomeka received by PSSSF. Nimefika kwenye ofisi zao wamesema wamepokea na zimewafikia watafanyia kazi, Ila kimya kingi Hadi leo. Naomba kufahamishwa kama lomesitishwa
Okay ......hii ela iliniumiza aisee sintosahau yaani nilikuwa apeche alolo 2019 nikatia timu NSSF nikakutana na hii dhahama ya fao la kukosa ajira wakati mie nataka nivute yote. Mwisho wa siku ikabidi nichukue fao la kukosa ajira na nilivyomaliza nikawa napambana nilipwe zilizobaki hata kwa kujifanya mgonjwa lakini wapi, kumbuka kipindi hicho hata staffs wa NSSF hawakuwa na maelezo ya what next ukishalipwa fao la kukosa ajira miezi sita. Nimekuja kugundua kwamba baada ya miezi 18 unalipwa baada ya kusota sana ndo kuna staff akanambia maana wengine walikuwa wanarukaruka the si unajua enzi zile mzee baba Magu alikuwepo.Sahihi, lakini ukipata kazi nyingine mpaka ukastaafu kile kiasi ulicho lipwa hakitotolewa kwenye malipo ya kustaafu
Asante kwa kushare experience, pole piaOkay ......hii ela iliniumiza aisee sintosahau yaani nilikuwa apeche alolo 2019 nikatia timu NSSF nikakutana na hii dhahama ya fao la kukosa ajira wakati mie nataka nivute yote. Mwisho wa siku ikabidi nichukue fao la kukosa ajira na nilivyomaliza nikawa napambana nilipwe zilizobaki hata kwa kujifanya mgonjwa lakini wapi, kumbuka kipindi hicho hata staffs wa NSSF hawakuwa na maelezo ya what next ukishalipwa fao la kukosa ajira miezi sita. Nimekuja kugundua kwamba baada ya miezi 18 unalipwa baada ya kusota sana ndo kuna staff akanambia maana wengine walikuwa wanarukaruka the si unajua enzi zile mzee baba Magu alikuwepo.
Nikasubiri miezi 18 nikavuta mkwanja wangu nikaacuana nao
Mkuu DOMINGO THOMAS sorry miezi 18 wanahesabu baada ya kulipwa hiyo 33 ya miezi 6 au inakuaje?Asante kwa kushare experience, pole pia
HaaaahaaHesabu ngumu zaidi ya calculus!
Kwanzia upoteze ajiraMkuu DOMINGO THOMAS sorry miezi 18 wanahesabu baada ya kulipwa hiyo 33 ya miezi 6 au inakuaje?
Fao la Kukosa Ajira ni faida/msaada wa kifedha unaotolewa kwa mwanachama wa mfuko wa pensheni aliyepoteza ajira kwa sababu zisizo za hiari, kama vile kufukuzwa kazi, kuisha kwa mkataba, au sababu nyingine za halali. Hata hivyo, fao hili halitolewi kwa mtu aliyeacha kazi kwa hiari, kwani kufanya hivyo humfanya apoteze sifa za kupata fao hili.
Sifa za Kupata Fao la Kukosa Ajira
Umri: Mtu anayestahili fao hili anatakiwa kuwa chini ya umri wa miaka 55, ikiwa umepoteza kazi na umri wako ni zaidi ya miaka 55 basi italazimika ulipwe fao la uzee (Old age pension)
Mchango: Fao hili ulipwa kwa Mwanachama aliye changia kwenye mfuko chini ya miezi 180, ikiwa umechangia zaidi ya miezi 180 na uko chini ya miaka 55 ukapoteza ajira, basi utalipwa pensheni iliyo cheleweshwa, (differed pension).
Sababu za Kupoteza Ajira: Ajira inatakiwa kuwa imekoma kwa sababu zisizo za hiari kama vile: kufukuzwa kazi, Mkataba kuisha, au kupunguzwa kazini (retrenchment).
Malipo ya Fao la Kukosa Ajira
Fao la kukosa ajira hulipwa kwa awamu mbili. Kwa Aliyechangia Zaidi ya Miezi 18: Malipo ya Awamu ya Kwanza: Unalipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho kwa kipindi cha miezi 6. Baada ya Malipo ya Kwanza: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (miaka miwili) cha kutafuta ajira, ukipata ajira, utaendelea kuchangia katika mfuko pale ulipoishia na ikitokea umekosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe au utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.
Kwa Aliyechangia Chini ya Miezi 18: Malipo: Utalipwa nusu ya kiasi ulichochangia kwenye mfuko. Baada ya Malipo: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (Miaka miwili) cha kutafuta ajira. Ukipata ajira, utaendelea kuchangia pale ulipoishia, na Ukikosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe kwa mfumo wa hiari au kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.
Pia malipo ya fao la kukosa ajira yanatofautina kwa mtu mwenye ujuzi (skilled) na Mtu asiye na ujuzi (Unskilled) kwa mtu asiye na ujuzi yeye hulipwa kiasi chote alicho changia kwenye mfuko na mwenye ujuzi yeye hulipwa kwa kufuata maelekezo hayo juu, hii ni kwasababu ni ngumu mtu asiye na ujuzi kupata ajira kwa urahisi ukilinganisha na mtu mwenye ujuzi
Kumbuka: Malipo ya fao la kukosa ajira yatakoma pale tu unapo pata ajira nyingine.
Sababu za Malipo Kufanyika kwa Awamu
Mfumo wa malipo kwa awamu una lengo la kuhakikisha mwanachama anaendelea kuwa na sifa za kupata pensheni ya uzee. Kama kiasi chote kingetolewa mara moja, kuna hatari ya mwanachama kufika umri wa kustaafu bila kufikia michango ya miezi 180 inayotakiwa kwa ajili ya pensheni ya uzee.
Hivyo, malipo kwa awamu yanasaidia kulinda michango iliyopo ili mwanachama awe na nafasi ya kufanikisha sifa za pensheni ya uzee.
Faida ya Fao la Kukosa Ajira
Hutoa msaada wa kifedha kwa kipindi cha mpito baada ya kupoteza ajira. Hakuna kupunguzwa kwa michango ya awali kwenye mfuko, Mfano: Ulikuwa na michango 20, ukalipwa fao la kukosa ajira, lakini hukuchukua kiasi chote. Ukipata ajira mpya, utaanza kuchangia kuanzia mchango wa 21 na kuendelea.
Kumbuka: Fao hili ni haki ya mwanachama aliyepoteza ajira kwa sababu halali zilizopo kwenye sheria, Mchakato wa kudai fao hili unahitaji nyaraka zinazothibitisha hali ya kuachishwa kazi kama barua ya kusitishwa kwa ajira.
Nilianza kulipwa hiyo 33.3% tarehe 11/12/2024 na nililipwa amount ya miezi miwili. Niliachishwa kazi tarehe 30/09/2024. Baada ya kunilipa hiyo hela ya miezi miwili inachukua muda gani kulipa malipo ya awamu nyingine kwa miezi minne iliyosalia. Nilijua labda wangelipa tena mwisho wa mwezi wa 12 lakini mpaka sasa hivi naona kimyaFao la Kukosa Ajira ni faida/msaada wa kifedha unaotolewa kwa mwanachama wa mfuko wa pensheni aliyepoteza ajira kwa sababu zisizo za hiari, kama vile kufukuzwa kazi, kuisha kwa mkataba, au sababu nyingine za halali. Hata hivyo, fao hili halitolewi kwa mtu aliyeacha kazi kwa hiari, kwani kufanya hivyo humfanya apoteze sifa za kupata fao hili.
Sifa za Kupata Fao la Kukosa Ajira
Umri: Mtu anayestahili fao hili anatakiwa kuwa chini ya umri wa miaka 55, ikiwa umepoteza kazi na umri wako ni zaidi ya miaka 55 basi italazimika ulipwe fao la uzee (Old age pension)
Mchango: Fao hili ulipwa kwa Mwanachama aliye changia kwenye mfuko chini ya miezi 180, ikiwa umechangia zaidi ya miezi 180 na uko chini ya miaka 55 ukapoteza ajira, basi utalipwa pensheni iliyo cheleweshwa, (differed pension).
Sababu za Kupoteza Ajira: Ajira inatakiwa kuwa imekoma kwa sababu zisizo za hiari kama vile: kufukuzwa kazi, Mkataba kuisha, au kupunguzwa kazini (retrenchment).
Malipo ya Fao la Kukosa Ajira
Fao la kukosa ajira hulipwa kwa awamu mbili. Kwa Aliyechangia Zaidi ya Miezi 18: Malipo ya Awamu ya Kwanza: Unalipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho kwa kipindi cha miezi 6. Baada ya Malipo ya Kwanza: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (miaka miwili) cha kutafuta ajira, ukipata ajira, utaendelea kuchangia katika mfuko pale ulipoishia na ikitokea umekosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe au utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.
Kwa Aliyechangia Chini ya Miezi 18: Malipo: Utalipwa nusu ya kiasi ulichochangia kwenye mfuko. Baada ya Malipo: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (Miaka miwili) cha kutafuta ajira. Ukipata ajira, utaendelea kuchangia pale ulipoishia, na Ukikosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe kwa mfumo wa hiari au kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.
Pia malipo ya fao la kukosa ajira yanatofautina kwa mtu mwenye ujuzi (skilled) na Mtu asiye na ujuzi (Unskilled) kwa mtu asiye na ujuzi yeye hulipwa kiasi chote alicho changia kwenye mfuko na mwenye ujuzi yeye hulipwa kwa kufuata maelekezo hayo juu, hii ni kwasababu ni ngumu mtu asiye na ujuzi kupata ajira kwa urahisi ukilinganisha na mtu mwenye ujuzi
Kumbuka: Malipo ya fao la kukosa ajira yatakoma pale tu unapo pata ajira nyingine.
Sababu za Malipo Kufanyika kwa Awamu
Mfumo wa malipo kwa awamu una lengo la kuhakikisha mwanachama anaendelea kuwa na sifa za kupata pensheni ya uzee. Kama kiasi chote kingetolewa mara moja, kuna hatari ya mwanachama kufika umri wa kustaafu bila kufikia michango ya miezi 180 inayotakiwa kwa ajili ya pensheni ya uzee.
Hivyo, malipo kwa awamu yanasaidia kulinda michango iliyopo ili mwanachama awe na nafasi ya kufanikisha sifa za pensheni ya uzee.
Faida ya Fao la Kukosa Ajira
Hutoa msaada wa kifedha kwa kipindi cha mpito baada ya kupoteza ajira. Hakuna kupunguzwa kwa michango ya awali kwenye mfuko, Mfano: Ulikuwa na michango 20, ukalipwa fao la kukosa ajira, lakini hukuchukua kiasi chote. Ukipata ajira mpya, utaanza kuchangia kuanzia mchango wa 21 na kuendelea.
Kumbuka: Fao hili ni haki ya mwanachama aliyepoteza ajira kwa sababu halali zilizopo kwenye sheria, Mchakato wa kudai fao hili unahitaji nyaraka zinazothibitisha hali ya kuachishwa kazi kama barua ya kusitishwa kwa ajira.
Hapo watakuwa wamekupa ya mwezi wa 11 na 12, I guess walichelewa kuchakata maana kama uliondoka kazini tarehe 30 Sept maana yake huwa inachukua mwezi process yote kukamilika....hivyo kifuatapo hapo utakuwa unalipwa mwezi mmoja mmoja mpaka hiyo miezi 6 iisheNilianza kulipwa hiyo 33.3% tarehe 11/12/2024 na nililipwa amount ya miezi miwili. Niliachishwa kazi tarehe 30/09/2024. Baada ya kunilipa hiyo hela ya miezi miwili inachukua muda gani kulipa malipo ya awamu nyingine kwa miezi minne iliyosalia. Nilijua labda wangelipa tena mwisho wa mwezi wa 12 lakini mpaka sasa hivi naona kimya
Thanks mkuu.Kwanzia upoteze ajira
Ila PSSSF wao hawafanyi hivyo hawalipi kila mwezi wanakulipa mzigo wote wa miezi 6 kwa pamoja. Kitu nachoona ni kizuri pia.Nilianza kulipwa hiyo 33.3% tarehe 11/12/2024 na nililipwa amount ya miezi miwili. Niliachishwa kazi tarehe 30/09/2024. Baada ya kunilipa hiyo hela ya miezi miwili inachukua muda gani kulipa malipo ya awamu nyingine kwa miezi minne iliyosalia. Nilijua labda wangelipa tena mwisho wa mwezi wa 12 lakini mpaka sasa hivi naona kimya
Mkuu DOMINGO THOMAS sorry miezi 18 wanahesabu baada ya kulipwa hiyo 33 ya miezi 6 au inakuaje?
Wanahesabu miezi 18 baada ya tarehe ya mwisho kumaliza kulipwa fao la kukosa ajira (mie walihesabu yaani ukifika tu counter anaangalia mwisho ulilipwa lini alafu ana count miezi 18 baada ya kumaliza kulipwa kisha anakupa maelekezo ya kuandika barua pamoja na kuchukua kiapo mahakamani / mwanasheria kudhibitisha huna ajira)Kwanzia upoteze ajira