Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Waha tena?.Wapare na Waha sijui walitokea kwenye sayari gani
Soma tena alichoandika mleta mada, utaelewaMkuu hili linahusu wale ambao wameshalipwa pesa za michango yao kutoka NSSF na bado hawajapata kazi wanaweza kurudi NSSF wakalipwa nusu ya pesa walizolipwa awali msaada tafadhari
Hata kwa sababu ya kupigana kazini? Nataka nimchote ngwara mhindi wanitimue nikachote vi hela vyangu nssf nimechoka kutumwa tumwa kifala,,Yes, kama unabarua ya kuachishwa kazi kwasababu yoyote ile unalipwa.
Na Waha tena?
😅😅😅👋🏾Hata kwa sababu ya kupigana kazini? Nataka nimchote ngwara mhindi wanitimue nikachote vi hela vyangu nssf nimechoka kutumwa tumwa kifala,,
Nenda na barua ya ukomo wa mkataba/kazi, watakupatia fomu za kujaza na kukupa maelekezo ya viambata vinavyo hitajika... (Wanaweza kukuuliza pia mbona umechelewa kuomba mafao/ Uandike barua kwanini umechelewa kuomba mafao)Hii imekaaje kwa mtu ambae aliachishwa kazi miaka saba nyuma na kachangia kwa miaka mitano ila tangu aachishwe kazi hakuwahi kufatilia na hayuko kwenye ajira mpaka sasa
Utalipwa fao la uzee, unapata kiinua mgongo chako + pensheni ya kila mwezi mpaka kifo.Ukifukuzwa kazi ukiwa umechangia , miezi 180 na umetimiza miaka 55, utalipwa Nini na Nini?
Ninaona mifuko imechanganya watu akili.
KaribuAhsante mkuu kwa andiko hili
Kama ulilipwa malipo ya awali, na miezi 18+ imepita bado huna ajira unaweza kurudi kuchukua michango yako iliyo bakia.Mkuu hili linahusu wale ambao wameshalipwa pesa za michango yao kutoka NSSF na bado hawajapata kazi wanaweza kurudi NSSF wakalipwa nusu ya pesa walizolipwa awali msaada tafadhari
Fao la Kukosa Ajira ni faida/msaada wa kifedha unaotolewa kwa mwanachama wa mfuko wa pensheni aliyepoteza ajira kwa sababu zisizo za hiari, kama vile kufukuzwa kazi, kuisha kwa mkataba, au sababu nyingine za halali. Hata hivyo, fao hili halitolewi kwa mtu aliyeacha kazi kwa hiari, kwani kufanya hivyo humfanya apoteze sifa za kupata fao hili.
Sifa za Kupata Fao la Kukosa Ajira
Umri: Mtu anayestahili fao hili anatakiwa kuwa chini ya umri wa miaka 55, ikiwa umepoteza kazi na umri wako ni zaidi ya miaka 55 basi italazimika ulipwe fao la uzee (Old age pension)
Mchango: Fao hili ulipwa kwa Mwanachama aliye changia kwenye mfuko chini ya miezi 180, ikiwa umechangia zaidi ya miezi 180 na uko chini ya miaka 55 ukapoteza ajira, basi utalipwa pensheni iliyo cheleweshwa, (differed pension).
Sababu za Kupoteza Ajira: Ajira inatakiwa kuwa imekoma kwa sababu zisizo za hiari kama vile: kufukuzwa kazi, Mkataba kuisha, au kupunguzwa kazini (retrenchment).
Malipo ya Fao la Kukosa Ajira
Fao la kukosa ajira hulipwa kwa awamu mbili.
Kwa Aliyechangia Zaidi ya Miezi 18: Malipo ya Awamu ya Kwanza: Unalipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho kwa kipindi cha miezi 6. Baada ya Malipo ya Kwanza: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (miaka miwili) cha kutafuta ajira, ukipata ajira, utaendelea kuchangia katika mfuko pale ulipoishia. na ikitokea umekosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe au utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.
Kwa Aliyechangia Chini ya Miezi 18: Malipo: Utalipwa nusu ya kiasi ulichochangia kwenye mfuko. Baada ya Malipo: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (Miaka miwili) cha kutafuta ajira. Ukipata ajira, utaendelea kuchangia pale ulipoishia, na Ukikosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe kwa mfumo wa hiari au kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.
Pia malipo ya fao la kukosa ajira yanatofautina kwa mtu mwenye ujuzi (skilled) na Mtu asiye na ujuzi (Unskilled) kwa mtu asiye na ujuzi yeye hulipwa kiasi chote alicho changia kwenye mfuko na mwenye ujuzi yeye hulipwa kwa kufuata maelekezo hayo juu, hii ni kwasababu ni ngumu mtu asiye na ujuzi kupata ajira kwa urahisi ukilinganisha na mtu mwenye ujuzi
Kumbuka: Malipo ya fao la kukosa ajira yatakoma pale tu unapo pata ajira nyingine.
Sababu za Malipo Kufanyika kwa Awamu
Mfumo wa malipo kwa awamu una lengo la kuhakikisha mwanachama anaendelea kuwa na sifa za kupata pensheni ya uzee. Kama kiasi chote kingetolewa mara moja, kuna hatari ya mwanachama kufika umri wa kustaafu bila kufikia michango ya miezi 180 inayotakiwa kwa ajili ya pensheni ya uzee.
Hivyo, malipo kwa awamu yanasaidia kulinda michango iliyopo ili mwanachama awe na nafasi ya kufanikisha sifa za pensheni ya uzee.
Faida ya Fao la Kukosa Ajira
Hutoa msaada wa kifedha kwa kipindi cha mpito baada ya kupoteza ajira. Hakuna kupunguzwa kwa michango ya awali kwenye mfuko, Mfano: Ulikuwa na michango 20, ukalipwa fao la kukosa ajira, lakini hukuchukua kiasi chote. Ukipata ajira mpya, utaanza kuchangia kuanzia mchango wa 21 na kuendelea.
Kumbuka: Fao hili ni haki ya mwanachama aliyepoteza ajira kwa sababu halali zilizopo kwenye sheria, Mchakato wa kudai fao hili unahitaji nyaraka zinazothibitisha hali ya kuachishwa kazi kama barua ya kusitishwa kwa ajira.
Unaweza,kunitumia eneo au mahali palikoandikwa Mkuu?Utalipwa fao la uzee, unapata kiinua mgongo chako + pensheni ya kila mwezi mpaka kifo.
Miezi 18+ toka ajira ilipo komaAsante kwa ufafanuzi mzuri, swali langu ni kwamba ukipokea fao la kukosa ajira kwa miezi sita, ili uweze kutoa mafao yako yaliyobakia unasubiri miezi 18 baada ya kulipwa miezi sita au miezi 18+ toka ajira ilipokoma?