Fahamu kuhusu Fao la Kukosa Ajira Tanzania (Unemployment Benefit)

Fahamu kuhusu Fao la Kukosa Ajira Tanzania (Unemployment Benefit)

Unampa mtu 33.3% ya mshahara wake wa mwisho laki 3, sasa pesa itamfikisha wapi? Huu si uhuni , mtu anateseka wakati pesa yake wamekalia NSSF wanatumia tu
Dhima na madhumuni ya kufanya hivyo yalikuwa ni mazuri tu, kumlinda mwanachama asipoteze sifa ya kuwa pensioner
 
Kama nimechangia miezi 180 plus nikafukuzwa kazi nikiwa chini ya umri wa miaka 55,,hapo stahiki zangu zitakuaje? Maelezo tafadhari.
Kama umechangia miaka 15+ (Miezi 180) kazi ikifika Ukomo na una miaka 55+ wewe utalipwa kiinua mgongo na pensheni ya Kila mwezi mpaka kufa, lakini ukiwa chini ya miaka 55 utalipwa kwanza kiinua mgongo alafu utasubiri utaratibu wa pensheni ya Kila mwezi ukifika miaka 55
 
Kama umechangia miaka 15+ (Miezi 180) kazi ikifika Ukomo na una miaka 55+ wewe utalipwa kiinua mgongo na pensheni ya Kila mwezi mpaka kufa, lakini ukiwa chini ya miaka 55 utalipwa kwanza kiinua mgongo alafu utasubiri utaratibu wa pensheni ya Kila mwezi ukifika miaka 55
Natarajia kufanya vituko Ili niachishwe kazi 2035,by that time nitakuwa below 50 lakini nitakuwa nimechangia zaidi ya miezi 180.
 
Fao la Kukosa Ajira ni faida/msaada wa kifedha unaotolewa kwa mwanachama wa mfuko wa pensheni aliyepoteza ajira kwa sababu zisizo za hiari, kama vile kufukuzwa kazi, kuisha kwa mkataba, au sababu nyingine za halali. Hata hivyo, fao hili halitolewi kwa mtu aliyeacha kazi kwa hiari, kwani kufanya hivyo humfanya apoteze sifa za kupata fao hili.

Sifa za Kupata Fao la Kukosa Ajira

Umri: Mtu anayestahili fao hili anatakiwa kuwa chini ya umri wa miaka 55, ikiwa umepoteza kazi na umri wako ni zaidi ya miaka 55 basi italazimika ulipwe fao la uzee (Old age pension)

Mchango: Fao hili ulipwa kwa Mwanachama aliye changia kwenye mfuko chini ya miezi 180, ikiwa umechangia zaidi ya miezi 180 na uko chini ya miaka 55 ukapoteza ajira, basi utalipwa pensheni iliyo cheleweshwa, (differed pension).

Sababu za Kupoteza Ajira: Ajira inatakiwa kuwa imekoma kwa sababu zisizo za hiari kama vile: kufukuzwa kazi, Mkataba kuisha, au kupunguzwa kazini (retrenchment).

Malipo ya Fao la Kukosa Ajira
Fao la kukosa ajira hulipwa kwa awamu mbili. Kwa Aliyechangia Zaidi ya Miezi 18: Malipo ya Awamu ya Kwanza: Unalipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho kwa kipindi cha miezi 6. Baada ya Malipo ya Kwanza: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (miaka miwili) cha kutafuta ajira, ukipata ajira, utaendelea kuchangia katika mfuko pale ulipoishia na ikitokea umekosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe au utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.

Kwa Aliyechangia Chini ya Miezi 18: Malipo: Utalipwa nusu ya kiasi ulichochangia kwenye mfuko. Baada ya Malipo: utakuwa na kipindi cha miezi 18 (Miaka miwili) cha kutafuta ajira. Ukipata ajira, utaendelea kuchangia pale ulipoishia, na Ukikosa ajira ndani ya kipindi hiki, utaandika barua kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko kuhama uchangiaji, toka uchangiaji wa lazima kwenda hiari, baada ya kuhama uchangiaji unaweza endelea kujichangia mwenyewe kwa mfumo wa hiari au kuchukua kiasi kilichobaki kwenye mfuko.

Pia malipo ya fao la kukosa ajira yanatofautina kwa mtu mwenye ujuzi (skilled) na Mtu asiye na ujuzi (Unskilled) kwa mtu asiye na ujuzi yeye hulipwa kiasi chote alicho changia kwenye mfuko na mwenye ujuzi yeye hulipwa kwa kufuata maelekezo hayo juu, hii ni kwasababu ni ngumu mtu asiye na ujuzi kupata ajira kwa urahisi ukilinganisha na mtu mwenye ujuzi

Kumbuka: Malipo ya fao la kukosa ajira yatakoma pale tu unapo pata ajira nyingine.

Sababu za Malipo Kufanyika kwa Awamu

Mfumo wa malipo kwa awamu una lengo la kuhakikisha mwanachama anaendelea kuwa na sifa za kupata pensheni ya uzee. Kama kiasi chote kingetolewa mara moja, kuna hatari ya mwanachama kufika umri wa kustaafu bila kufikia michango ya miezi 180 inayotakiwa kwa ajili ya pensheni ya uzee.

Hivyo, malipo kwa awamu yanasaidia kulinda michango iliyopo ili mwanachama awe na nafasi ya kufanikisha sifa za pensheni ya uzee.

Faida ya Fao la Kukosa Ajira

Hutoa msaada wa kifedha kwa kipindi cha mpito baada ya kupoteza ajira. Hakuna kupunguzwa kwa michango ya awali kwenye mfuko, Mfano: Ulikuwa na michango 20, ukalipwa fao la kukosa ajira, lakini hukuchukua kiasi chote. Ukipata ajira mpya, utaanza kuchangia kuanzia mchango wa 21 na kuendelea.

Kumbuka: Fao hili ni haki ya mwanachama aliyepoteza ajira kwa sababu halali zilizopo kwenye sheria, Mchakato wa kudai fao hili unahitaji nyaraka zinazothibitisha hali ya kuachishwa kazi kama barua ya kusitishwa kwa ajira.
Ni somo zuri sana lakini sijaelewa kwa nini kuna watu wame-dislike!
 
Hii sheria inawaumiza watu wa Mkataba.Nimewahi fanya kazi kampuni binafsi kabla ya mambo kuvurugika awamu ya 5 ,baada ya kazi kuisha walinilipa hela zangu zote ndani ya mwezi 1 tuu ,ilikuwa PPF saizi haipo.
Kivipi inawaumiza.....!?
 
Kivipi inawaumiza.....!?
Sasa unaanzaje kulipwa mdogo mdogo harafu unasubiria miezi 18 uanze upya kutafutiza huoni huo ni usumbufu na lolote linaweza tokea hapo katikati?

PPF waliwahi nipa hela yote Kwa mkupuo na ndio ulikuwa utaratibu wa awali.

Uzembe wa mifumo kukosa hela ndio umewashishia mzigo walioko kwenye Ajira za mkataba.

Harafu Serikali imerekwbisha sheria ya kikokotoo iliyolalamikiwa na wale permanent employee,Kwa nini wasirekebishe na Kwa temporary contract employees? Hapo unaona ni sawa?
 
Serikali haina huruma kabisa wabunge wanalipana mafao zaidi ya 200M wakimaliza tu miaka yao 5, lakini Mtanzania anae lipwa laki 5 anaambiwa apewe 33.3% nyingine asubiri miezi 18, hii nchi hii ina viongozi wa hovyo sana , vitu vingine hata mtoto wa darasa la 7 anaweza kuwazidi akili
Kitu ambacho unatakiwa kufahamu wabunge, madiwani, wakuu wa mikoa na wilaya sio wanachama wa PSSSF/NSSF na hawalipwi na hiyo mifuko
 
Dhima na madhumuni ya kufanya hivyo yalikuwa ni mazuri tu, kumlinda mwanachama asipoteze sifa ya kuwa pensioner
Mwanachama yupi wakati mikataba yenyewe uko private haieleweki? mkisha kuwa serikalini mnasahu kuwa waajiri huku ni wahindi na wachina, wanakutumia wanakupa laki 3 au 4 hakuna mikopo wala bonus, mtu anapotaka pesa yake apewe acheni usumbufu wakati ni pesa yake
 
MKUU MFANO,MTU ALIKUWA ANAFANYA KAZI YA KUFUNDISHA,MKATABA UKAISHA,NA HAKUPEWA MWINGINE,BALI AKAPEWA BARUA YA KUMALIZA MKATABA NA ALIKUWA ANACHANGIA,AKIWA LABDA MKOA X.

JE,AKITAKA KUOMBA STAHIKI HIZI MPAKA AOMBEE OFISI ZA MKOA HUOHUO X AU HATA AKIWA MKOA Y ANAWEZA KUOMBEA OFISI ZA HUKO?

NA UTARATIBU WA KUOMBA HIZI STAHIKI UKOJE YAANI UNAANZIA WAPI?
Utaratibu wa kuomba mafao unaweza omba ukiwa mkoa wowote ule kwenye ofisi za mfuko husika, fika na barua yako ya ukomo wa mkataba na namba yako ya uanachama, utapewa utaratibu na fomu za kujaza.
 
Kitu ambacho unatakiwa kufahamu wabunge, madiwani, wakuu wa mikoa na wilaya sio wanachama wa PSSSF/NSSF na hawalipwi na hiyo mifuko
Kama wabunge wanalipwa kiinua mgongo chote, na mishahara yao ni mikubwa sana, sasa kona kona za nini kwa huyu mtoto wa masikini anaetaka kujikwamua kutoka kwenye kifungo cha wahindi? mnashangaa wagonjwa wa akili kuongezeka wakati nyie ndio tatizo, wapeni watu pesa zao wafanye biashara waokoe familia zao
 
Back
Top Bottom