Fahamu kuhusu kirusi mbaya zaidi wa kompyuta(ransomware)

Fahamu kuhusu kirusi mbaya zaidi wa kompyuta(ransomware)

Ghost MVP

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2022
Posts
439
Reaction score
736
Ransomware ni programu (Kirusi) iliyoundwa kumnyima mtumiaji au shirika ufikiaji wa faili kwenye kompyuta yake. Kwa kuloki faili hizi kwa njia amabyo huwezi fungua na kisha kudai malipo ili uweze kufungua faili zako, wavamizi (Hackers) wa mtandao huweka mashirika katika hali ambayo kulipa fidia ndiyo njia rahisi na ya bei nafuu zaidi ya kurejesha ufikiaji wa faili zao. Baadhi ya mashirika yameongeza utendaji wa ziada - kama vile wizi wa data - ili kutoa motisha zaidi kwa waathiriwa wa Kirusi hiki Ransomware kulipa fidia.
network-infection-coronavirus.jpeg


Ransomware imekuwa kwa haraka aina maarufu na mbya zaidi ya kirusi. Mashambulizi ya hivi majuzi ya ransomware yameathiri uwezo wa hospitali kutoa huduma muhimu, kulemaza huduma za umma katika miji, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa mashirika mbalimbali.

-Kiwangi cha malipo ya kufunguliwa fail zako huwa ni kwanzia $800,000(TSH. 1.8 Bilion) hadi $5,000,000(TSH.11.6 Bilion) ambayo pia haina uhakika kama ukimlipa Hacker atakufungulia au atatokomea na pesa yako, FIB na mashira makubwa ya kuzuia uhalifu wanaendelea tafuta namna ya kuumaliza uhalifu hii.

Kirusi hiki huingia katika system/Computer yako kwa njia ya Internet, Ambapo inaweza kuja kama Ad(Tangazo) Au link ya zawadi ambapo ukiigusa na kufungua ni ketendo cha dakika moja tu na computer yote inakuwa katika shambilizi

Chanzo: Checkpoint

shutterstock_1098423464.jpeg


MASHIRIKA 5 MAKUBWA AMBAYO YALIKUMBANA NA UHALIFU HUU WA MTANDAO
1.CWT Global
-Shirika la usafirishaji la America, Ililipia Dola za kimarekani $4.5Million(TSH 10.4 Bilioni), Mwezi Julai mwaka 2020.
-Shambulio hili liliathiri kompyuta 30,000 na kuaribu data za 2TB(2000 GB), Mfumo wa malipo, Data binafsi za wafanyakazi, Nyara za siri.

2.COLONIAL PIPELINE -Wasambazaji wa mafuta na gesi walilipa Dola za Kimarekani $4.4Million(TSH 9.8 Bilioni), Mwezi may mwaka 2021.
-Shambulio hili liliathiri mfumo wote wa malipo ambayo kampuni ilishindwa kufatilia malipo kwa wateja wake wala kupata data za usambazaji na uuzaji wa nishati yao.

3.BRENNTAG - Kampuni ya usambazaji wa kemikali ililipa Dola za kimarekani $4.4Million((TSH 10.4 Bilioni), Mwezi May mwaka 2020.
-Shambulio hili lilisababisha wizi wa data za 150GB ambayo iliitikisa kampuni, na kusitisha maili 5,000 za bomba la mafuta, mapka pale walipofikia muafaka wa malipo

4.TRAVELEX - Mwaka 2019 tarehe 1 siku ya mwaka mpya kampuni hii iliathiriwa na Virus huyu kwa muda wa wiki mbili, na walilipa Dola $2.3Million(TSH.5.3 Bilioni)

5.UNIVERSITY OF CALIFONIA AT SANFRANSISCO - Mwezi Juni 2020 Chuo kiliathiriwa na kirusi huyu mpaka walipolipa Dola $ 1.14Million(TSH. 2.6 Bilioni)

Chanzo:IT-GOVERNANCE
 
Ni balaa, Akishaloki izo Files hivyo ndo ieisha hiyo, kibongo bongo ni kupiga windows tu
Ipo decryptor tool moja ambayo niliitumia nikafanikisha ku recover audio

Ila changamoto yake ni kuwa wimbo unakuwa mbele sekunde kadhaa, hauanzii mwanzo
 
Ipo decryptor tool moja ambayo niliitumia nikafanikisha ku recover audio

Ila changamoto yake ni kuwa wimbo unakuwa mbele sekunde kadhaa, hauanzii mwanzo
Kwa Ripoti mpaka sasa hakuna hacker wala developer aliefanikiwa ku Encrypt files zilizoathirika na Ransomware. kama ulifanikiwa ku recover bc ilikuwa online
 
Kwa Ripoti mpaka sasa hakuna hacker wala developer aliefanikiwa ku Encrypt files zilizoathirika na Ransomware. kama ulifanikiwa ku recover bc ilikuwa online
Ipo decryptor ambayo inaweza recover audio inaitwa MSISOFT Decryptor tool au stop DJVU
 
Wacha niifatilie nijue zaid kuhusu hiyo
Hii hapa ndio iliyofanya kazi kwangu

Nilifanikisa ku recover audio ila kipengele ni kwamba zilikua zimekatwa sekunde kadhaa za mwanzo

Kwenye swala la media hi inaweza kuwa hope ila kama una files za Rar au documents zingine hii haiwezi
1659122398735.png



Ila hii hapa chini kwangu haikufanya kazi kabisa

1659122532760.png
 
Walipita na vifaili vyangu, dah nikakosa pozi.
Walikuwa ransomware wa extension gani?

Mimi nimepoteza data nyingi za msingi kila siku natamani nizifute lakini nimeamua kuziacha nikiamini kuna siku huyu mdudu atapatiwa ufumbuzi na mimi nitaweza access tena files zangu

1659122719192.png
 
Hii hapa ndio iliyofanya kazi kwangu

Nilifanikisa ku recover audio ila kipengele ni kwamba zilikua zimekatwa sekunde kadhaa za mwanzo

Kwenye swala la media hi inaweza kuwa hope ila kama una files za Rar au documents zingine hii haiwezi
View attachment 2308299


Ila hii hapa chini kwangu haikufanya kazi kabisa

View attachment 2308305
Hii ni free?
 
Wacha niangalie how inaweza function
kwa media hasa audio ambayo nishawahi test, nakuhakikishia unaweza ku retrieve audio zako fresh, ila hapo kwenye video nabashiri utakutana na changamoto labda kama wamefanyia maboresho app yao maana kipindi natumia ilikuwa ni mwaka jana
 
Ransomware mwenye extension ya QSCX ni msala mazee, mwaka jana alipita na data zangu nyingi sana

View attachment 2307927


Wajinga wanani approach niwape 980$

View attachment 2307929
Kwetu sisi shida ni kupenda vitoga kwa kupakua Cracked software jamaa wanatunasia huko!!!
Mimi nilipotea data muhimu sana na kupata fundisho la kutosha.
Now nikiona site au file zisizoeleweka sigusi kabisa pia nina backup zaidi ya moja nisipoteze mazima
 
Kwetu sisi shida ni kupenda vitoga kwa kupakua Cracked software jamaa wanatunasia huko!!!
Mimi nilipotea data muhimu sana na kupata fundisho la kutosha.
Now nikiona site au file zisizoeleweka sigusi kabisa pia nina backup zaidi ya moja nisipoteze mazima
Swala la crack bado nitaendelea nalo huo ndio ulimwengu wangu

Ila hicho kirusi kinaweza kumpata yeyote na ndio maana hapo juu kuna visa vya makampuni makubwa walio kuwa wahanga na hiki kirusi
 
Back
Top Bottom