Fahamu kuhusu Kitabu Cha Malleus Maleficarum Maarufu kama Nyundo ya Wachawi

Fahamu kuhusu Kitabu Cha Malleus Maleficarum Maarufu kama Nyundo ya Wachawi

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
FB_IMG_1636949810024.jpg

FAHAMU KUHUSU KITABU CHA MALLEUS MALEFICARUM MAARUFU KAMA NYUNDO YA WACHAWI

Hiki ni kitabu ambacho kiliandikwa na Heinrich Kramer na kuchapishwa kwa mara ya kwanza katika mji wa Speyer nchini Ujerumani mnamo mwaka 1486.

Kitabu hicho kimebeba ujumbe kuhusu wachawi ambapo ndani yake kuna maandishi yenye mapendekezo ya adhabu kwa mtu aliyebainika kuwa ni mchawi kwa wakati huo.

Adhabu iliyokuwa imepandekezwa ilikuwa ni kuteswa vikali na pili ni adhabu ya kifo ambapo walifikiri hilo ndilo suluhisho kwa mtu aliyetenda dhambi ya uchawi.

Kitabu hicho kilitumika sana katika karne ya 16 na 17 ambapo katika kipindi hicho inaelezwa kuwa zaidi ya watu millioni 5 waliteketezwa kwa moto wakiwa hai.

Pia inasemekana kuwa wakati huo kuzungumzia masuala yaliyohusu uchawi ilikuwa ni mwiko, kwa wale waliokuwa wanabainika kwa kosa hilo adhabu yake ilikuwa ni kifo.

Matumizi ya kitabu hicho yaliamuriwa na Papa Innocent VIII mwaka 1486.
Mwaka 1922 nchini Sweden ilitoka filamu ya kichawi iliyopewa jina la Häxan, filamu hiyo ilichezwa kwa mujibu wa kitabu hicho yaani yote yaliyoelezewa ndani ya kitabu yapo ndani ya filamu hiyo.
 
Ooh mambo ya kanda ya ziwa kumbe huko ni longtime kitambo tena msimamia shoo ni papa
 
Kuna watu wana bisha kua uchawi hakuna ila lengo nikutaka kuhakika au ushuuda .wanataka kuona kwa macho ya nyama.
 
Kuna watu wana bisha kua uchawi hakuna ila lengo nikutaka kuhakika au ushuuda .wanataka kuona kwa macho ya nyama.
Wanao sema hivyo baadhi yao nao ni wakali wa hizo kazi
 
Back
Top Bottom