Mkuu biashara sometimes ujanja ujanja unatakiwa na kuwa na kauli ya kibiashara ...kama biashara anadhani anaweza kuifanya aifanye hivyo hivyo hata kama atahudumia wateja wa 50,000 na mteja wa 500,000, akija wa million ambao ni wachache atajua namna ya ku-deal nao maana navyojua kama mtu ni mwaminifu sometimes huwa anapokea hela na kumpa namba ya wakala mwingine ili kuweza kumuaminisha mteja siku nyingine aje maana wenye vibanda vya huduma hizi wengi level zao hizo hizo za laki moja ama mbili inategemea na location.
Kwahiyo apige mdogo mdogo tu kama ana nia ya kweli ya hiyo biashara maana ukisema kuongeza mtaji wakati mwingine muda sio rafiki kwani ukiwa na goli (kibanda) ni mwanzo mzuri hata kama mtaji ni mdogo lakini pia ni rahisi kupiga hata mzinga mtu laki moja na nusu hata ndugu zako 10 kwa ahadi ya utawarudishia baada ya siku kadhaa unaongezea mtaji (mjini humu wengine tukiwa na shida ya laki 2 tunatumia mbinu ya kuomba watu tofauti tofauti hata kama ni 20,000 ama 40,000 mpaka itafika laki 2)