Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Kumbe ujanja ujanja!?. Hapo sawa mwambieni basi awe mjanja mjanja japo biashara haitaki ujanja ujanja wateja wakishagundua watakukimbia wote na huko mtaani utasemwa vibaya
 
Sijaelewa hapa "wateja wa kuweka kwako"
Mteja akitoa pesa mfano shilingi 5000 commission inakua kama 160 hivi
Mteja kuweka 5000 commission ni kama 100

Hapo sasa Umepata concept Kidogo kuwa mteja akitoa pesa kuna commission kubwa kidogo kuliko akiweka
 
Na huo ndio uhalisia Wenywe naweza kumwambia mtu niazime hata laki tatu baada ya siku kadhaa mfano week narudisha hela ya watu nikiwa nmetengeneza faida
Kweli

Ila changamoto zilizopo kwa sasa utapeli umekuwa mwingi sana

Tunahitaji kuwa makini
 
Kumbe ujanja ujanja!?. Hapo sawa mwambieni basi awe mjanja mjanja japo biashara haitaki ujanja ujanja wateja wakishagundua watakukimbia wote na huko mtaani utasemwa vibaya
Ujanja ujanja sio huo unaofikiria mkuu hiyo ni nyongeza lakini kikubwa nilichoamaanisha ni mwanzo mgumu aende mdogo mdogo tu mwisho wa siku akiwa na goli inakuwa rahisi hata kukopa kwa ndugu na jamaa kwa kuwa tayari umeonyesha una shughuli mjini lakini sio lazima (ndo ujanja niliouzungumzia)...ukienda kwa watu wa hardware mfano unakuta mtu anauza tiles za aina tofauti tofauti na ameweka display, wengi wao sio kweli ana vigae vya kutosha ..mara nyingi unakuta ana box kadhaa na ukitaka mzigo mkubwa anakuambia upo stoo na wanachofanya wanakwenda kwenye duka la jumla na kuchukua mzigo lakini sie tukianza unakuta mtu anawekeza milion kadhaa na anachukua mzigo lundo kumbe wenzake wanachukua chache chache na mara nyingi wauzaji wa jumla wanawafahamu wenye duka wote akipiga simu mzigo unaletwa anapewa chache na yeye anachukua chache (ndio ujanja ujanja naouzungumzia huo ukiambatana na kauli ya kibiashara)
 
Hatuelewan kwa kusema 500,000 anaweza pata commission ya laki 6 kwa mwez voda. Ndo hapo mi nasema hayo matumaini hewa kabisa mwambien ukweli mkuu kuwa huo mtaji unatosha kuanzia na akikomaa anapata faida nzur tu ili kukuza hiyo biashara yake lkn "not to that extent"( kwa sauti ya mkuru)
 
Changamoto hizo za utapeli zipo yani mwezi wa pili tu nilikula shoti kama 90 hivi nililalamika sana ila sikufa moyo nikaanza upya leo sio tena bwege

Unawakwepaje hao matapeli maana nasikia wanatapeli kweli wanatumia mbinu gani?
 
Unawakwepaje hao matapeli maana nasikia wanatapeli kweli wanatumia mbinu gani?
Kusema ukweli natumia lugha ya biashara hapo hapo nikiwa simuamini mtu sitoi hela bila kuhakikisha sms kwenye simu yangu kama umekosea kutuma sijui nini wasiliana na makao makuu huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…