As-salamu alaykum...kauli zangu zimefanya nini? Wewe kijana mwenzangu kama huna hoja ni busara ukiwa mpole tu. Ikiwa unavyo vielelezo vyote vya muhimu kuna sababu gani iliwafanya wakupe line mwezi wa nne? Hiyo miezi mitatu ya nyuma walikuwa wanachunguza nini? Au wewe wakati unapewa hiyo line, walikwambia sababu ya kukuchelewesha? Hatukatai hizo line zinatolewa bure, lakini usumbufu ni mkubwa na mazingira ya kutumika kwa rushwa ili upate line ni makubwa mno. Sasa ukishatoa chochote kwa kukimbia usumbufu hiyo line itakuwa ya bure? Kuna faida gani kusubiri line ndani ya miezi 4; while ukinunua kwa mtu aliyemuaminifu kwa muda mfupi unaanza kuitumia kwa kufanya biashara... Eti?