Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

It should be used at highway speeds of over 55 mph(80Kph), but its OK to have it on all the time since your car wont shift into overdrive until the conditions are right (speed and RPM).
 
Nijuavyo mimi,
Ukiwa unaendesha Less than 80km/per hour let the over drive be off- Taa inawaka kwenye dashboard( OD OFF)
Over 80km/hr let the over drive be on. Wakati huo Taa yenye maandishi (OD OFF) kwenye dashboard huwa haiwaki

Kuhusu kula mafuta ni hivi.
RPM ikiwa above 2.5 gari inakula mafuta. Kama unaendesha gari iki OD OFF na uko speed above 80km/hr rpm lazima iende zaidi ya 2.5. hivyo kuashiria kula mafuta.

Ukitaka kujaribu weka OD OFF then icrease your speed to 100km/hr the look at the rpm. wakati ikiwa kwenye mwendo huo press button ya OD the look at the rpm. utaona itashuka ghafla na gari inaongeza speed. (NOT APPLICABLE FO DAR RESIDENTS).

Mlachake ndivyo nilivyofundishwa sasa inaonekana kuwa kinyume chake hebu nisaidieni hilo
 
DU...Yaani ndugu zangu mbona mnateseka sana kuelezea ama kuelewa kitu hiki kidogo namna hii? Ni hivi, OD maana yake ni Top gear, yaani gear namba 5 full stop. Hivyo basi hutumika pale tu unapotaka kwenda kwa speed kubwa kwa maana kwamba utatumia gear zote tano za automatic car. Kwa hapa mjini ambapo speed ni chini ya 80kmph huna sababu yeyote ya kutumia OD. Ni kwawale wanaokwenda zaidi ya hiyo speed.
 
Hiyo kitu utamu wake kwenye masafa marefu bana.. kuipa gari take off ya ajabu especially kama unataka kuovertake! unabonyeza hicho kidude..ukishabonyeza tu kitawasha taa ya OD/OFF kwenye dash board... hapo ujue ni mwendo mdundo na upige simu kabisa kwa Shayo akuwekee ndoo ya mbege manake ni fasta unakua migombani(natamani december ifike haraka).

Anyway ukitaka kuienjoy OD button inabidi uwe na V6 au V8! hizi baby walker na vicoroola zitakuzingua tu kinapiga kelele we wakati kipo hapo hapo tu
 
Nina Escudo yani nikiweka OD inakuwa nzito na inakimbia na kuchanganya haraka huwa mpaka naogopa, nashindwa kuelewa mnaposema ukifika ukitaka kukimbia zaidi inabidi uitoe ukifikia speed fulani.
Ni kweli... ukiweka gari inakuwa nzito na inavuta sana
Unashauriwa kuitumia ktk long safari ie unataka kuovertake ama gari inaposinzia katika milima
Kwenye tope ama mchanga unaapply d2
Humu mjini usitumie kwani itaongeza ulaji wa mafuta..yaani feature iwe ON-dashboard light itakuwa off
Ingelikuwa gari ni manual OD ONN inamaanisha kuweka gia za juu haraka na kupunguza kutumia gia kubwa(za chini) katika matumizi ya kawaida na OD OFF ni kupangua gia from higher gear ili uvute kasi na definetly utaongeza spidi ya engine RPM na kasi na pia itakula mafuta zaidi--RECOMMENDED FOR SHORT DISTANCE(INSTANCES) ONLY
 
Overdrive (OD) is a term used to describe a mechanism that allows an automobile to cruise at sustained speed with reduced engine RPM, leading to better fuel economy, lower noise and lower wear.

Use of the term is confused, as it is applied to several different, but related, meanings.The most fundamental meaning is that of an overall gear ratio between engine and wheels, such that the car is now over-geared and can no longer reach its potential top speed, i.e. the car could travel faster if it were in a lower gear, with the engine turning more quickly. In some cases this implies a second definition is also true, that the gearbox output driveshaft is rotating faster than the original engine RPM. This later definition was common in the past, but many cars no longer have a driveshaft and it is not technically correct

In the era of front-engine, rear-wheel drive layouts, the device for achieving an overdrive transmission was usually a small separate gearbox, attached to the rear of the main gearbox and controlled by its own shift lever or electrical actuation button. These were often an optional extra on some models of the same car. As popular cars became faster relative to legal limits and fuel costs became more important, particularly after the 1973 oil crisis, the use of 5-speed gearboxes became more common in mass-market cars, with the 5th gear being an overdrive, eliminating the need for a separate gearbox.

With the popularity of front wheel drive cars, the separate gearbox and final drive have merged into a single transaxle. However the fundamental meaning, that of an overall ratio higher than the ratio for maximum speed, still applies. Although the deliberate labeling of an overdrive is now rare, the underlying feature is now found across all cars.

Source: Overdrive (mechanics) - Wikipedia, the free encyclopedia
 
you are right ... there is a confusion somewhere on when should overdrive supposed to be

ukiangalia gear lever ... button ya overdrive ikiwa chini basi OD ipo on na button ikiwa juu basi OD is off na dashboard itawaka taa ya "overdrive off"

hivyo basi kutokana na maelezo ya wadau nina assume kwamba normal use ya gari ni wakati OD ipo on .... yaani wakati taa ya overdrive haiwaki



Thanx LAT, pamoja na kuwepo maelezo mengine, maelezo ya LAT yazingatiwe
 
Nijuavyo mimi,
Ukiwa unaendesha Less than 80km/per hour let the over drive be off- Taa inawaka kwenye dashboard( OD OFF)
Over 80km/hr let the over drive be on. Wakati huo Taa yenye maandishi (OD OFF) kwenye dashboard huwa haiwaki

Kuhusu kula mafuta ni hivi.
RPM ikiwa above 2.5 gari inakula mafuta. Kama unaendesha gari iki OD OFF na uko speed above 80km/hr rpm lazima iende zaidi ya 2.5. hivyo kuashiria kula mafuta.

Ukitaka kujaribu weka OD OFF then icrease your speed to 100km/hr the look at the rpm. wakati ikiwa kwenye mwendo huo press button ya OD the look at the rpm. utaona itashuka ghafla na gari inaongeza speed. (NOT APPLICABLE FO DAR RESIDENTS).
BINGO......!!!:censored:

Mlachake ndivyo nilivyofundishwa sasa inaonekana kuwa kinyume chake hebu nisaidieni hilo
So Do I!! Ngoja tuwasubirie kina Michael Schumecher wengine labda sisi ndo hamnazo kwenye haya makitu.:high5:
 
BINGO......!!!:censored:

So Do I!! Ngoja tuwasubirie kina Michael Schumecher wengine labda sisi ndo hamnazo kwenye haya makitu.:high5:

kaka nilishadanganywa eti wakati nina overtake halafu niko kwenye overdrive then nikaona hatari mbele, i.e una overtake labda semi then mbele ukaona basi ku avoid face to face crush eti unaturn overdrive off hapo hapo unarudisha gear kwenye drive 2 eti gari inapata nguvu na speed ya ajabu!!!

My God someone tried this technique gari ikapaa ikawa mwisho wa maisha yake.
 
Kwa ninavyofahamu mimi, overdrive ni kama walivyoeleza waliotangulia ila, kama iko off maana yake unaifanya gari iweze isiweze kwenda mpaka gear ya mwisho. Kama ina 7 speed itaishia 6. Kama ni 4 speed itaishia 3. Ukiangalia kweye gear lever yako kutegemea na gari lako utagundua yafuatayo. P R D 4 3 2 L AU 1. Mengine P R D 2 L AU

1. Ukiweka kwenye L means gari itakuwa kwenye gear ya 1 na haitaruka hapo. Hapo ni kama unavuta gari au unashuka mteremko mkali sana ili kupata engine braking au kupanda mlima mkali sana au kutoka kwenye matope kama umezama. Ukiweka 2 inakuwja inaishia hapo kwenye gear ya pili na haiendi zaidi.

Hapo ni kama upo kwenye barabara mbaya sana na unajua huhitaji gear zaidi ya hiyo. Hapa unaipunguzia kazi gear box yako na hata kuiongezea maisha. Ukiweka 3 the same inaishia hapo. Wameweka hivi makusudi kwa kuwa ikiwa D itakuwa inajaribu kufanya kazi sana ya kutafuta gear kutokana na motion ya gari.

Hapa sasa kuna makundi mawili. Hilo la P R D 2 L ndiyo common hapa na ndiyo zenye kidude cha kubonyeza. Kikiwa OFF taa itakuwa inawaka kwenye dash na kikiwa ON Haitowaka. Kama iko OFF maana yake gari haitokuwa inapata support ya engine kwenye kusimama kama vile kupangua kwa wale wenye manual transmission.

Ni brake tu itatumika. Advantage ya kutumia overdrive ni kwamba gari inatumia mafuta kidogo kwa kuwa ukiachia mafuta gari litakuwa neutral. Kama lingekuwa kwenye OD OFF litakuwa kwenye gear likijipangua lenyewe na hapo maana yake mafuta yatatumika mengi. Kundi hili mara nyingi transmission zake hazizidi 4 speed na kama itazidi ni 5 but ni chache sana. Zenye P R D 4 3 2 L AU 1 ni zenye hadi 7 speed. Nyingi ni za kisasa na zenye mambio mengi.

Hizi wamekurahisishia. Badala ya kile kiswitch cha OD wamekuwekea hizo 4 3 nk. Hazina hako kadude tena. Na sina uhakika kama hiyo button ina mahusiano na kuongeza nguvu ya gari zaidi ya haya maelezo niliyotoa. Ila kwenye magari baadhi kuna buttons kwa ajiri ya kazi hiyo na imeandikwa Power/ Normal.

Ukiibofya itaaeika kwenye dash pia. Power kwa maana ya kwamba, kama gear ya kwanza ingechange katika speed 10 kwa mfano, then itachange katika speed 30. Hapa ni kwamba unataka mbio. Bei ya mafuta tunaifahamu kwa sasa nadhani. Hayo ni maelezo kwa jinsi mimi nijuavyo jamani.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kwenye harrier mpangilio wa gear kuna P R D then M ambayo ipo kwa ndani kidogo, ukiweka kwenye M inadisplay manual kwenye dash board na mlio unabadilika, mwenye kujua matumizi yake tafadhali.
 
Ushauri wa bure kwa wale wanaotaka kusave mafuta. Kwanza uhakikishe gari lako lina service nzuri na kwa wakati. Air cleaner isiwe chafu. Spark plugs ziwe nzuri, upepo wa matairi uwe ni ule unaotakiwa na ucheck mara kwa mara. Hakikisha RPM isizidi namba 2. Gari yako utaipenda na itatumia mafuta vizuri.

Tumekuwa pia tukinunua magari yetu mapya na kwa kuwa tunayapenda tunafanya kubadili wheel rims na wakati mwingine kuweka kubwa zaidi. Mfano unanunua gari yenye wheel rims inch 14 unazitoa na kuweka 15 au 16.

Hakika litapendeza but kuna disadvantages zake. Utakuwa umeliongezea uzito na halitoweza kuwa normal tena kwenye vitu vingi sana ikiwemo matumizi ya mafuta kuongezeka pia vitu kama wheel bearings nk.

Ila kama mambo ya mafuta hayakupi shida then hakuna tatizo. Mimi ninalo gari langu ambalo linakula lita 1 kms 10 mjini na highway hufika hadi 13. Wenzangu hulalamikia ya kwao the same model kuwa yanatumia lt 1 kms 6 mjinh na hata wakiwa kwenye highway haizidi lt 1 km 8 to 9. Mara nyingi sababu ni hizo hapo juu. Na mufindi ni jadi yangu ati.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
wakuu

ni nini hasa matumizi ya Over Drive kwenye gari yenye automatic gear (transmition), je hutumika wakati gani haswa yaani ni wakati gani na speed gani inatakiwa iwe on au off ..... what are the pros and cons
Gari inaweza kwenda 140km/ph ikawa na gear 1-4 lakini speed ikawa imeisha hivyo ukipress button ya OD inaongeza kasi zaidi!Na gari yenye 5speed ikwa kwenye speed ya 160km/ph unaweza kuweka OD
ahsanteni
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Dah. Hili somo bado nitasupple. Kwenye premio kuna maneno huwa yanaonekana kwa rangi ya kijani 'economy' maana yake nini. Pia kuna vidude viwili kimoja ukibonyeza kinaleta alama ktk db 'manu' kingine'power'. Msaada angalu nifaidike na haya maana hili somo la od limenishinda
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Ukiwa od off taa ya njano huwaka na mara zote taa za njano na nyekundu huwa ni za taadhali kwa njano na hatari kwa nyekundu. Ni vema taa zote huhakikishe zimezima za taadhali na hatari. Hivo basi hakuna cha kuwa mjini au highway. Kitu kingine ni kwamba kuna spesho gia kama rivas na gia ya mwisho au overdrive. Hizi hata kwenye manual wakt wa kuingiza kuna spring yaani kukutaadhalisha kuwa hiyo ni spesho na hiyo button ni taadhali tu. ukiangalia vema kwenye auto huwezi kuweka R bila kubonyeza kitufe
 
Back
Top Bottom