Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakti huu;
Ni matumaini yangu kwamb mnaendelea salama na Shughuli zenu za upambanaji na utafutaji wa Riziki;
Leo nimeona nilete mada ambayo kwa wajasiriamali wengine inaweza kuwa na faida sana na kuwasaidi katika kufanya mipango kuhusu maisha yao ya sasa na ya baada.
Leo nataka kuzungumza kuhusu kitu kinaitwa Retirement Planning au kujipanga kwa maisha baada ya kustaafu.
Kwanza nianze kusema kwamba Kustaafu sio suala la umri au uwezo ni suala la uamuzi.Ninaposema ni suala la uamuzi ninamaanisha kwamba Sio kila mstaafu afikie umri wa miaka 55 au 60 hata hivyo ktika mjadala wetu wa leo tunaweka utaratibu kwamba Mstaafu atastaafu akiwa na umri wa miaka 60 kwa mujibu wa sheria zetu.
Sasa nitaomba sana andiko lolote ambalo nitaliweka hapa ambalo linazungumzia masuala ya kisheria na iwapo litakuwa na makosa basi mwenye utaalamu anaweza kuweka marekebisho nami nitajitahidi kufuatili zaidi na kufanya maboresho.
Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo kwa mifuko Rasmi ya hifadhi ya Jamii,Mstaafu anaweza kulipwa Pensheni pale tu ambapo anakua amechangia angalau michango 180 au michango ya miaka 15 mfululizo au zaidi ya hapo.Michango inakuwa mfululizo bila kujitoa wala kuruka kuchangi.HIvyo Basi iwapo wewe ni majsiriamali na unataka kujindaa kwa ajili ya kustaafu ni lazima uangali Umri wako wa sasa na umri wa kustaafu imebaki miaka mingapi.Iwapo imebaki chini ya miaka 15 basi usijaribu kushawishia na fao la kujitoa.Ila Pia inabidi uanze kuangalia kiwango chako cha mchango unachotoa uone iwapo kinaweza kuendana na mipango yako baada ya kustaafu ili auweze kujipanga
Jambo lingine ambalo unapaswa kufahamui ni kwamba Mstaafu hulipwa kiinuo mgongo(Lumpsum Pension) ambayo ni kama theluthi moja ya michango yake yote na kisha kila mwezi hulipwa mafao ya kila mwenzi amabyo ni sawa pia kama theluthi moja ya pato lake la wastani wa mwaka wake wa mwisho wa ajiraa.Hii ina maana kwamba kama Mshahara wako kwa miezi 12 kabla ya kustaafu ni Milioni 1 basi pensheni yako ya kila mwenzi itakuwa ni theluthi moja hivi aua kama laki 330,000.Hii inamaana kwamba katika mwaka wako wa mwisho wa ajira ni lazima kabisa ujiandae kwa kuongeza pato lako la mshahara ili upandishe kiwango chakeo cha Lumpsum na kiwango cha Pensheni.
Baada ya maelezo hayo sasa nieleze namna mjasiriamali anavoweza kufanya mipango ya kujiandaa kustaafu na wakti sahihi wa kuanza kufanya hivyo.Kwa kuanza tufahamu kwamba Michango ya Hifadhi ya Jamii ni Tax exempted na hivyo basi kama wewe ni Mjasiriamali ambaye unamiliki Kampuni au biashara yako uanweza kabisa kuchangia na malipo yale yakatoka kwenye Kampuni yako na kuipa nafuu ya kikodi.Ila usisahu kwamba kiwango utakachotumia Pia ndicho kitatumika katika kukotoa kodi ya Payrol Tax(Kodi ya Mshahara )Hivyo bsi unapopiga hesabu zako zingatia PIA Hilo;
Pembeni ya Hii mifuko ya hifadhi ya jamii(Kwa sasa NSSF Pekee) uanweza kuwa na Mipango mingine ya kustaafu kama vile kununua BIMA za Maisha ambazo nyingi hazina kiwango kikubwa sana cha michango.Unaweza kuchukua Bima ya Maisha ya Wafanyakazi ambayo kimsingi nayo ina faida.Inabidi uzungumze na kampuni za BIMA vizuri ili uweze kupata aina ya BIMA ambayo itawanufaisha warithi wa wafanyakazi wako iwapo watafia kazini,na Pia itwainufaisha kampuni iwapo wataishi mpaka wastaafu au kuwanufaisha wote.
Mambo ya kuzingatia unapofanya Mipango ya kustaafu ni kuhakikisha kwamba Unatumia Kiwango kidogo kabisa cha uwekezaji ili kupata faida kubwa mbeleni hasa kwa kuzingatia halihalisi ya uchumi wako binafsi na hali ya uchumi wa taifa.Usiishi maisha ya dhiki katiki kipindi unapojiandaa kustaafu ili ustaafu na mafao makubwa bali tafuta namna ya kubalance Mapato yako ya sasa yakupa maisha ya Furaa na wakti huo huo ya kupe nafasi ya kuishi maisha mazuri utakapo staafu.
Je unafikiri ni kiwango gani ni kizuri cha kuweka kama akiba kwa ajili ya kujiandaa kustaafu ambayo itakupa Kiwango kizuri cha maisha baada ya kustaafu?
Tujadili kwa pamoja huku tukiboresha mjadala huu na kuweka taarifa ambazo zitakusaidia katika kupanga kustaafu