Fahamu kuhusu Utapeli kwa Njia ya Phishing Attach (links, email, attachments)

Fahamu kuhusu Utapeli kwa Njia ya Phishing Attach (links, email, attachments)

Ghost MVP

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2022
Posts
439
Reaction score
736
Habari wana jukwaa!..

Technology ikiwa inaendelea kukuwa na vijana wa hovyo hawajaachwa nyuma, kuna utapeli unafanyika leo nataka nikuelekeze kuhusu utapeli wa kutumia 'Phishing Attack'.

960x0.jpg

Phishing Attack ni njia inayotumia kuiba taarifa nyeti ambazo ni siri ya mtumiaji husika, kama Back Accounts, Neno la Siri(password), user name, na mengine mengi.

Ambapo Mdukuaji atanumia vitu kama Links, Email, Attachments, Pop Ads(matangazo ya dharura) ili kuingia katika mfumo wa Device yako na kuiba anachohitaji. Mdukuzi anakutumia Link, Email, Attachments, an Tangazo ili kukuvutia weww kufata process kadhaa ambazo zitamuwezesha yeye kuchukua umiliki wa device yako na vyote vilivyomo ndani yake.

1679588974857.jpeg


Mfano: Anakutumia Linki ya Promotion ya wewe kushinda au Tangazo la wewe kushinda iPhone 15 na wewe bila kufikiria toka lini mtu akakushindisha vitu bila kuvifanyia jitihada unagusa link hiyo, Email au Tangazo hilo ukishaenda kwenye Ukurasa inakutaka kuhakikisha taarifa zako kama Email, password na wewe bila kufikiria unalogin, inakuambia unekosea. Papo hapo anakuwa kashapata Email na Password yako na atalogin na kupata emails zako zote kwa wale wanaotumia Email katika kazi na Bank habari inakuwa imeishia hapo.

IMG_2322.jpeg

IMG_2323.jpeg


Mwingine ukishaingia kwenye ukurasa wao inaku command kuzipa Access Contacts, File & Media, Storage, Camera ambapo anauwezo wa kupata namba zako zote zilizopo katika simu, Picha video, Apps n.k. hii hupelekea wewe kuibiwa vitu vyako vya siri katika simu au computer yako bila wewe kujua. Na vilevile naweza kuona unachofanya kwenye simu, kama kuingia katika Mobile Banking, pin za miamala na atazitumia badae kukuibia bila wewe kujua.

Jihadhari na kugusa Link usizozijua, matangazo ya zawadi, attachment katika email iliyotoka kwa mtu usiyemjua au link iliyowekwa.
 
Back
Top Bottom