Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552

Habari wataalam,

Nataka nijenge nyumba ndogo kwa mjengo wa stail ya ghorofa moja yaani floor moja kwa juu, kutokana taratibu za nchi na vibali vya ujenzi.

Naomba kwa anaejua hatua za kufanya ili kupata vibali na gharama za kupata hivo vibali, sitaki kujenga kienyeji nataka kufuata utaratibu ili wasije kuniandama.

Note: Eneo halijapimwa, ni squater tu.

BAADHI YA MASWALI YA WADAU WENGINE
======
Salaam wana jukwaa, nina kiwanja maeneo ya Mbweni nataka nianze ujenzi mdogo mdogo nyumba ya kuishi.

Kabla sijaanza chochote nimekuja humu jukwaani kuomba ufafanuzi jinsi ya kupata KIBALI CHA UJENZI.
======
======
======
======


BAADHI YA MAJIBU YA WADAU
======
======

 
Uwe na mchoro (plan) ya jengo, kama eneo lako liko katika mpango wa mji au jiji, ipeleke ofisi ya ardhi kwa ajili ya wao kuiangalia na kukupa ruhusa (approval)
 
Uwe na mchoro (plan) ya jengo, kama eneo lako liko katika mpango wa mji au jiji , ipeleke ofisi ya ardhi kwa ajili ya wao kuiangalia na kukupa ruhusa (approval)
Kama eneo halijapimwa je inawezekana?
 
Uko mkoa gani au eneo lipi ndani ya nchi ya Tanzania?

Kwanza kabisa kua na mchoro wako. Kwakua eneo siyo surveyed basi chakufanya nenda ofisi ya ardhi ya halmaahauri uliyopo wapelekee ramani yako then watakupatia kibali cha ujenzi kama eneo hilo halina longo longo.
 
Eneo lipo Tuangoma Temeke-Dar asante sana mkuu. Je, kuna malipo yeyote? Na itachukua mda gan?
 
Angalia wasikuambie eneo ni la NSSF mkuu.

Yes bro, kuna malipo japo sikumbuki ni how much. Fika tu ofisini Temeke pale nadhani utaelezwa procedures zote.
Eneo lipo Tuangoma Temeke-Dar asante sana mkuu. Je kuna malipo yeyote? Na itachukua mda gan?
 
Uwe na nakala kadhaa za michoro ya aina mbili yaani architectural drawings na pia structural drawings ambazo utazipeleka ofisi za ardhi katika halmashauri husika ili michoro ipitishwe na kisha kupata kibali cha ujenzi. Ujenzi bila kibali ni sawa na kuchezesha hela zako karibu na tanuru la moto.

Kibali kinapotolewa kinakuwa valid kwa miezi sita na inatakiwa uwe umeanza ujenzi ndani ya muda huo ila ikitokea umeshindwa kuanza ujenzi ndani ya muda huo itabidi kuomba extension ya muda.

Kupitishwa kwa maombi ya kuongezewa muda uwa hakuchukui muda mrefu kama maombi ya mwanzo.
 
Angalia wasikuambie eneo ni la NSSF mkuu.

Yes bro, kuna malipo japo sikumbuki ni how much. Fika tu ofisini Temeke pale nadhani utaelezwa procedures zote.
Asante sana mkuu, ushauri wako at least utasaidia, mengine nitajua hukohuko.
 
1. KIBALI CHA UJENZI
Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo Mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya:-
(i) Kutuma maombi kwa mamlaka ya mji
(ii) Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika
(iii) Kupata kibali kwa maandishi kinachoitwa “Kibali Cha ujenzi”

2. KIBALI CHA AWALI (Planning consent)

Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outland plan) kwa utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho.

Faida:
• Kuokoa muda na gharama iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
•Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.

3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI
Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe ifuatavyo:-
• Seti tatu za michoro ya jengo (Archectural drawing)
• Seti mbili za michoro ya vyuma/mihimili (structural drawings) kwa michoro ya ghorofa

4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI

Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-
• Namna jengo litakavyokuwa (plans, sections, elevations, foundation and roof plan)
• Namba na eneo la kiwanja kilipo
• Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
• Jina la mchoraji, ujuzi na anwani
• Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
• Ujazo wa kiwanja (Plot coverage)
• Uwiano (Plot ratio)
• Matumizi yanayokusudiwa
• Idadi ya maegesho yatakayokuwepo
• Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks)
• Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo

5. VIAMBATANISHO

• Fomu za maombi zilizojazwa kwa usahihi
• Hati ya mmiliki wa kiwanja au barua ya toleo
• Kumbumbuku nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo, makabidhiano n.k
• Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo
• Mabadiliko ya matumizi ya ardhi

6. HATUA ZINAZOFUATWA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA KIBALI
Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:-
• Uhakiki wa miliki
• Kukaguliwa usanifu wa michoro
• Kukagua kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa
• Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano
• Uchunguzi wa maofisa wa afya
• Uchunguzi wa mipango ya uondoaji maji taka
• Uchunguzi wa tahadhali za moto
• Uchunguzi wa uimara wa jingo
• Kuwasilishwa kwenye kikao cha Mipangomiji na Mazingira baada ya kukamilisha taratibu zote
• Hatimaye kuandika na kutoa kibali

7. TARATIBU ZA KUFUATA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI


Kwa mujibu wa sheria ya ujenzi mijini ujenzi wowote ambao
umepata kibali unapaswa kukaguliwa kwa kila hatua ya ujenzi. Baada ya kupata kibali cha ujenzi mambo yafuatayo yanapaswa kufanyika:-
1. Kutoa notisi ya masaa 48 kabla ya kuanza ujenzi. Fomu ya notisi hii utapatiwa unapokabidhiwa kibali cha ujenzi
2. Kujaza fomu ya ukaguzi na kuwasilisha kwenye ofisi ya ujenzi ili hatua hiyo ya ujenzi unayotaka kufanya ikaguliwe
3. Utapatiwa “Certificate of Occupation” baada ya ujenzi wako kukamilika iwapo tu hatua muhimu za ujenzi zimekaguliwa

8. FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA IKIWA NA KIBALI CHA UJENZI

1. Kuishi kwenye nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama
2. Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji uliopangwa
3. Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali ikiwa pamoja na kushitakiwa mahakamani, kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.

Hayo ndio Mambo muhimu ya kuyafahamu kuhusu 'Kibali cha Ujenzi' (Building Permit), Epuka usumbufu fuata sheria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…