Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Unaweza ukafanya hivyo na bado ukabomolewa, unalijua tingatinga mukuu?

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile app
 
Nimekuelewa ila huduma kwenye ofisi zetu ni mbovu.
 
Haya sasa jenga uje uvunjiwe mimi kama bwana afya huwa nawaambiaga watu wa kata yangu ila wanakuwa vichwa vigumu sehemu ambayo unaona haitakiwi kama hifadhi ya barabara, sehemu za wazi, mabondeni, mkondo wa umeme mkubwa, hifadhi za misitu maeneo ya shule ila bado hawasikii wavunjiwe tu

ukienda halmashauri utakuta plan na hiyo unailipia sasa watz tuache ujinga wa shoti kati na tufuate ushauri
Bwana Afya, mimi nami nimekupa hali halisi. Usiupuuze wasi wasi wangu, through me utapata kujua kwa nini watu wapo hivyo walivyo.

Kama unathubutu kutuita wajinga, unamuitaje Afisa mwenzio wa TANESCO na mwenzake wa DAWASCO wanaowawekea huduma za maji na umeme waliojenga huko huko pasiporuhusiwa? Wao nao hawajui zilipo ofisi za halmashauri wakachukue plan?

Ukitaka kuijua hii nchi tuulize wananchi.
 
Bwana Afya, mimi nami nimekupa hali halisi. Usiupuuze wasi wasi wangu, through me utapata kujua kwa nini watu wapo hivyo walivyo.

Kama unathubutu kutuita wajinga, unamuitaje Afisa mwenzio wa TANESCO na mwenzake wa DAWASCO wanaowawekea huduma za maji na umeme waliojenga huko huko pasiporuhusiwa? Wao nao hawajui zilipo ofisi za halmashauri wakachukue plan?

Ukitaka kuijua hii nchi tuulize wananchi.

Hahaha samahani lakini mkuu. Nimesema hivyo kwa sababu unaona mtu anafanya kivingine ukimleta kwenye uhalisia anajifanya anajua sasa ndo ivyo. Kuna mama alijenga maeneo ya mkondo wa maji sasa amemaliza ujenzi naja kumuambia hapa hapafai na namuonyesha na kalavati la maji ndo anapata presha.

Hii nchi bana inanifurahishaga sana ila basi ni bora tufiche taaluma zetu ila wanaichi bana wanachosha aisehhh mpaka nakuwa emotional
 
Thread nzuri.

Tatizo mipangi miji hawawashirikishi wananchi kujua ramani za miji na mipango ardhi ya eneo( wanaficha ranabi za urban/town plan utadhani ni siri za jeshi).

Gharama za mchakato wote ni kubwa ndiyo maana watu wanapenda shortcut, Pia wataalamu wa ardhi ni wachache sana yaan kuna mikoa mingine wapo mkoani( mikoa mipya mfano Katavi na Songwe) wakati wapo wahitimu wa fani hizo kutoka vyuo vikuu mf ardhi, sua etc wanaendesha bodaboda mitaani.

Ushauri mchakato ufupishwe na uwekewe time frame kutoka kuomba hadi kupata mf wiki 4, au 6 na siyo miezi mingi .
Pia, watu wa ardhi waache ubabaishaji katika kazi zao, na wao wawe mfano mzuri kwani wapo waliobomolewa nyumba zao kama wengime wasiyojua sheria za mipango miji.
 
USIJENGE KIHOLELA, TAMBUA MAMBO HAYA MUHIMU KUHUSU 'KIBALI CHA UJENZI'

1. KIBALI CHA UJENZI
Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo Mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya:-
(i) Kutuma maombi kwa mamlaka ya mji
(ii) Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika
(iii) Kupata kibali kwa maandishi kinachoitwa “Kibali Cha ujenzi”

2. KIBALI CHA AWALI (Planning consent)
Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outland plan) kwa utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho.

Faida:
• Kuokoa muda na gharama iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
•Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.

3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI
Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe ifuatavyo:-
• Seti tatu za michoro ya jengo (Archectural drawing)
• Seti mbili za michoro ya vyuma/mihimili (structural drawings) kwa michoro ya ghorofa

4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI
Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-
• Namna jengo litakavyokuwa (plans, sections, elevations, foundation and roof plan)
• Namba na eneo la kiwanja kilipo
• Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
• Jina la mchoraji, ujuzi na anwani
• Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
• Ujazo wa kiwanja (Plot coverage)
• Uwiano (Plot ratio)
• Matumizi yanayokusudiwa
• Idadi ya maegesho yatakayokuwepo
• Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks)
• Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo

5. VIAMBATANISHO
• Fomu za maombi zilizojazwa kwa usahihi
• Hati ya mmiliki wa kiwanja au barua ya toleo
• Kumbumbuku nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo, makabidhiano n.k
• Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo
• Mabadiliko ya matumizi ya ardhi

6. HATUA ZINAZOFUATWA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA KIBALI
Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:-
• Uhakiki wa miliki
• Kukaguliwa usanifu wa michoro
• Kukagua kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa
• Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano
• Uchunguzi wa maofisa wa afya
• Uchunguzi wa mipango ya uondoaji maji taka
• Uchunguzi wa tahadhali za moto
• Uchunguzi wa uimara wa jingo
• Kuwasilishwa kwenye kikao cha Mipangomiji na Mazingira baada ya kukamilisha taratibu zote
• Hatimaye kuandika na kutoa kibali

7. TARATIBU ZA KUFUATA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI

Kwa mujibu wa sheria ya ujenzi mijini ujenzi wowote ambao
umepata kibali unapaswa kukaguliwa kwa kila hatua ya ujenzi. Baada ya kupata kibali cha ujenzi mambo yafuatayo yanapaswa kufanyika:-
1. Kutoa notisi ya masaa 48 kabla ya kuanza ujenzi. Fomu ya notisi hii utapatiwa unapokabidhiwa kibali cha ujenzi
2. Kujaza fomu ya ukaguzi na kuwasilisha kwenye ofisi ya ujenzi ili hatua hiyo ya ujenzi unayotaka kufanya ikaguliwe
3. Utapatiwa “Certificate of Occupation” baada ya ujenzi wako kukamilika iwapo tu hatua muhimu za ujenzi zimekaguliwa

8. FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA IKIWA NA KIBALI CHA UJENZI


1. Kuishi kwenye nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama
2. Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji uliopangwa
3. Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali ikiwa pamoja na kushitakiwa mahakamani, kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.

Hayo ndio Mambo muhimu ya kuyafahamu kuhusu 'Kibali cha Ujenzi' (Building Permit), Epuka usumbufu fuata sheria!.JENGA KWA RAMANI.
 
Ni vigumu hilo jambo kwa tanzania hii ya kununua kiwanja miguu 20 kwa 20 unapandisha vyumba viwili kwanza choo kwa jirani vingine utamalizia taratibu ukiwa ushaamia nikifikilia hilo na hiyo namba 7 hapo kazi kwelikweli ila sio kesi mdogomdogo tutafika ni swala kujizoesha then itakuwa kawaida tu.

TUIJENGE PAMOJA NCHI yetu
 
Duuu utafikili baada ya kufuata hatua zote unapewa mkopo wa vifaa vya ujenzi?
Nashindwa kuelewa kabisa. Kwanini isingekuwa unapeleka ramani ya nyumba,malipo ya kibali na hati tu; mlolongo namna hiyo halafu kibali unapewa baada ya miez 6 si usumbufu huu.
 
Nashindwa kuelewa kabisa. Kwanini isingekuwa unapeleka ramani ya nyumba,malipo ya kibali na hati tu, mlolongo namna hiyo halafu kibali unapewa baada ya miez 6 si usumbufu huu.

Unaonaje saivi ukitoka mwenge paka posta kwa gari binafsi km9 unaweza tumia paka masaa ma3 siku zingine si usumbufu? au maji kujaa posta nzima kwa mvua ya siku moja si usumbufu? the list could go on. Gharama ya miji mibovu na iliyojengwa kiholela ni kubwa kuliko taratibu ndogo kama hii. kwa nchi zingine taratibu zao ni strict hata kuzidi hii. japo wanaweza boresha pia na kufanya taratibu ikawa haraka zaidi na yenye ufanisi.
 
Kibali kinatolewa baada ya muda gani ukifuata taratibu zote hizo na gharama yake ikoje au ni bure?
 
Back
Top Bottom