Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Comment #4 ya jolya02 imemaliza kila kitu hivyo fuata ushauri wake maana eneo hata kama halijapimwa huwa kuna master plan ambayo inaonyesha kama eneo hilo ni la makazi ama shughuli zingine za kijamii. Ikionekana kama ni la makazi basi ni rukhsa kujenga ila kama alivyoshauri jolya02 nenda Manispaa kitengo cha ardhi kwa mwongozo zaidi (lakini si vibaya kama ukipita ofisi ya kata ambapo kiwanja kipo kabla ya kwenda Manispaa huenda wakakupa utaratibu wa awali wa kufuata kabla ya kwenda Manispaa)
 
Baadhi ya serikali za mitaa zina ramani ya kijiji chao. Kwa huku kwetu hata ukienda kwa mjumbe ana ramani na ana kupointia kabisa maeneo ya makazi na maeneo mengineyo.

Vinginevyo nenda ofisi za ardhi.
 
Salaam wana jukwaa, nina kiwanja maeneo ya Mbweni nataka nianze ujenzi mdogo mdogo nyumba ya kuishi.

Kabla sijaanza chochote nimekuja humu jukwaani kuomba ufafanuzi jinsi ya kupata KIBALI CHA UJENZI.
 
Kama unajenga ghorofa inbd uwe na michoro ya architect, pamoja na michoro ya structural engineer, kama ni jengo la kawaida ambalo sio ghorofa inabd uwe na mchoro wa architect, baada ya hapo unapeleka copy tatu za mchoro wa architect manispaa, kumbuka huo mchoro lazma uwe na mhuri wa registered Arch. firm. ama ni ghorofa lazma upeleke nakala tatu za mchoro wa architect, pia nakala mbili za mchoro wa structure eng. Ukiwa na mhuri.

Kama huna mchoro wowote unaweza kunifata PM tutaweza fanya kazi na kukufuatlia kibali manispaa.
 
Weee muache atafute vibali mwenzio huko mbweni kwa wazito hakuna nyumba za hovyo hovyo
 
Kama unauhakika kiwanja chako kipo mahari pazuri, we anza kujenga acha bwebwe manispaa watakufuata wenyewe km kuna shida.
 
Maeneo haya ukianza tu....jamaa hawa...........!
Kuna kaka yangu alinunua kiwanja kisicho pimwa akataka akipime bei ya kupima ilikuwa kama wanakukomoa na bado unawalipa lakini kazi hawataki kufanya.
 
Haya mazoea ndio baadae yanatugharimu.
Unaweza kujenga hata ukiwa na hiko kibali ila nchi hii ikifika wakati hao wanaokupa kibali kuamka kutoka usingizini unakuwa sawa na sisi ambao tulijenga bila vibali,unadhani lile jengo la Tanesco lilijengwa bila kibali?
 
Kwahio wewe unamshauri mtu ajengr bila kibali kisa tanesco wamebomolewa? Kwanini lele jengo limebomolewa? Kwasababu liko ndani ya hifadhi ya barabara.

Fyi kama umejanga au umeuziwa kiwanja sehemu isiostahili ukafanya mipango ukapata kibali cha ujenzi jua kuwa ipo siku watabomoa.
 
Kama unajenga ghorofa inbd uwe na michoro ya architect, pamoja na michoro ya structural engineer, kama ni jengo la kawaida ambalo sio ghorofa inabd uwe na mchoro wa architect, baada ya hapo unapeleka copy tatu za mchoro wa architect manispaa, kumbuka huo mchoro lazma uwe na mhuri wa registered arch. Firm.. Kama ni ghorofa lazma upeleke nakala tatu za mchoro wa architect, pia nakala mbili za mchoro wa structure eng. Ukiwa na mhuri...

*kama huna mchoro wowote unaweza kunifata pm tutaweza fanya kazi na kukufuatlia kibali manispaa*
Vipi mkuu, hata servant quarter inahitaji kibali?
 
Vipi mkuu, hata servant quarter inahitaji kibali?
Kisheria kila ktu kinachojengwa kinahtaji kibali, ila kulingana na ukiritmba uliopo huko manispaa wengi huwa hawafati huo utaratbu..
Unaweza jenga ila wakikudaka lazma wakupige fine, cha kukushauri tu kama unataka kujenga unaweza enda ofisi ya serikali ya mtaa wale huwa ndo wanawatonya watu wa manispaa, wale ukienda nao sawa ujenzi wako utakamilika bila bugudha yoyote
 
Shukrani sana mkuu.
 
Back
Top Bottom