Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Ningependa kujua kama nimefuata hatua zote zinazostahili ila wakati wa kuanza kujenga nikataka kubadilisha/kuongeza idadi ya madilisha. Je, itabidi nianze upya kuomba kibali dhidi ya mabadiliko au imekaaje wakuu?
 
Ningependa kujua kama nimefuata hatua zote zinazostahili ila wakati wa kuanza kujenga nikataka kubadilisha/kuongeza idadi ya madilisha.je itabidi nianze upya kuomba kibali dhidi ya mabadiliko au imekaaje wakuu?

frami42, salamu kwako. Swala la kubadilisha madirisha na uhitaji wa kuomba kibali kuna mitazamo miwili. Mtazamo wa Kwanza ni kwa jengo kubwa mfano wa ghorofa kumi,inaweza ikakulazimu kuomba marejeo ya kibali cha ujenzi. Elewa kuwa madirisha kwenye majengo yanaweza kuathiri muhimili wa jengo. Chukulia uzito wa dirisha moja mara madirisha elfu moja ya mbao alafu ulinganishe na ya aluminium. Kwenye majnego kuna kitu kinaitwa specifications, isitoshe kibali cha ujenzi huwa kina toa conditions ambazo unastahili uzifuata,Ila utakubaliana nami kwa jengo dogo sidhani kama utakuwa na sababu hiyo zaidi ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

Mwenzetu
 
kote umepuyanga mkuu ungetaja gharama ya hivyo vibali hata mwenyewe ungeukimbia uzi wako

Jembekillo naomba nikufahamishe kuwa kila mamlaka ina bei tofauti ya tozo ya kibali cha ujenzi kulingana na mazingira, mfumo iliyopo na hata kwa kuzinagtia historia ya sehemu husika. Mfano iliyokuwa mamlaka ya Ustawi wa Mji wa Dodoma ina gharama tofauti na Mamlaka ya uendelezaji wa Mji mkongwe Zanzibar au halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Ushingae kusikia kuwa Mamlaka ya Viwanja vya ndege nayo inatoa vibali vya ujenzi wa matangazo ya biashara katika maeneo yake na ina tozo zake tofauti kulingana na mazingira yake. Kumbuka kuwa vibali ya Ujenzi hutolewa kwa lengo la kuthibiti ujenzi (utaalamu na ukandarasi), ardhi (umiliki wa viwanja), afya, mazingira pamoja na mipango miji.Vile vile ni chanzo cha mapato kwa Mamlaka husika,tena kinaweza kuwa chanzo kikuu. Hebu jiulize makusanyo ya fedha za vibali vya ujenzi katika Mkoa wa Dar es Salaam ni kiasi gani kwa kuzingatia Manispaa zake za Kinondoni,Ilala na Temeke)
 
Kupata tu huo mchoro ni ujenzi tosha.....
Afu hizo taratibu mbona lukuki. Naamini zingefuatwa pasingekuwa na slums wala uswazi.
Wameweka tu njia za kula hela hakuna chochote kinachokaguliwa labda kwa wajenga magorofa.
Chumba na sebule bwana afya wa kazi gani.
 
Afu hizo taratibu mbona lukuki. Naamini zingefuatwa pasingekuwa na slums wala uswazi.
Wameweka tu njia za kula hela hakuna chochote kinachokaguliwa labda kwa wajenga magorofa.
Chumba na sebule bwana afya wa kazi gani.
Si ndo hapo na ukjichanganya na hiko chumba chako na sebule hawakuachi wanafyeka pesa yako
 
Mlolongo mpk uje upate kibali mwenzako jirani yako atakuwa ameshahamia.
 
Kuna mtu kafanikiwa kujenga kwa kufuata huo.utaratiibu atupe mrejesho
 
Kurzweil,

Mkuu vipi kwa sie tulio vijijini sheria inasemaje kuhusu taratibu za ujenzi?
 
Kama nataka kujenga fence ya ukuta; nayo inahitaji kibali?
Fence pia inahitaji kibali ila mlolongo wake ni mfupi. Unaandika barua ya maombi ukiambatanisha nakala ya hati, risiti za malipo ya kodi ya ardhi pamoja na mchoro wa fence. Baada ya uhakiki wa umiliki na ukaguzi wa eneo husika unalipia kibali na unapata
 
Kurzweil,

Ni jambo vuri ila mlolongo mrefu sana hasa mwenye kunilimbikizia vihela kwa ujenzi! Ndio maana watu wanjenga baadae wanakuja kupigwa fine maisha yanaenda.

Ila kiukweli ni jambo jema kufata utaratibu huo ila ni ukweli pia kwamba mchakato huo ni mgumu sana kuutimiliza hasa watanzania wa kawaida anayejenga chumba kimoja kimoja na baadae nyumba kukamilika!

Na uwepo wa mchakato mrefu namna hiyo unatoa mianya ya kutoa rushwa!
 
Back
Top Bottom