Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

USIJENGE KIHOLELA, TAMBUA MAMBO HAYA MUHIMU KUHUSU 'KIBALI CHA UJENZI'

1. KIBALI CHA UJENZI

Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo Mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya:-
(i) Kutuma maombi kwa mamlaka ya mji
(ii) Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika
(iii) Kupata kibali kwa maandishi kinachoitwa “Kibali Cha ujenzi”

2. KIBALI CHA AWALI (Planning consent)
Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outland plan) kwa utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho.
Faida:
• Kuokoa muda na gharama iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
•Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.

3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI
Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe ifuatavyo:-
• Seti tatu za michoro ya jengo (Archectural drawing)
• Seti mbili za michoro ya vyuma/mihimili (structural drawings) kwa michoro ya ghorofa

4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI
Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-
• Namna jengo litakavyokuwa (plans, sections, elevations, foundation and roof plan)
• Namba na eneo la kiwanja kilipo
• Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
• Jina la mchoraji, ujuzi na anwani
• Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
• Ujazo wa kiwanja (Plot coverage)
• Uwiano (Plot ratio)
• Matumizi yanayokusudiwa
• Idadi ya maegesho yatakayokuwepo
• Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks)
• Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo

5. VIAMBATANISHO

• Fomu za maombi zilizojazwa kwa usahihi
• Hati ya mmiliki wa kiwanja au barua ya toleo
• Kumbumbuku nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo, makabidhiano n.k
• Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo
• Mabadiliko ya matumizi ya ardhi

6. HATUA ZINAZOFUATWA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA KIBALI

Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:-
• Uhakiki wa miliki
• Kukaguliwa usanifu wa michoro
• Kukagua kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa
• Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano
• Uchunguzi wa maofisa wa afya
• Uchunguzi wa mipango ya uondoaji maji taka
• Uchunguzi wa tahadhali za moto
• Uchunguzi wa uimara wa jingo
• Kuwasilishwa kwenye kikao cha Mipangomiji na Mazingira baada ya kukamilisha taratibu zote
• Hatimaye kuandika na kutoa kibali

7. TARATIBU ZA KUFUATA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI

Kwa mujibu wa sheria ya ujenzi mijini ujenzi wowote ambao
umepata kibali unapaswa kukaguliwa kwa kila hatua ya ujenzi. Baada ya kupata kibali cha ujenzi mambo yafuatayo yanapaswa kufanyika:-
1. Kutoa notisi ya masaa 48 kabla ya kuanza ujenzi. Fomu ya notisi hii utapatiwa unapokabidhiwa kibali cha ujenzi
2. Kujaza fomu ya ukaguzi na kuwasilisha kwenye ofisi ya ujenzi ili hatua hiyo ya ujenzi unayotaka kufanya ikaguliwe
3. Utapatiwa “Certificate of Occupation” baada ya ujenzi wako kukamilika iwapo tu hatua muhimu za ujenzi zimekaguliwa

8. FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA IKIWA NA KIBALI CHA UJENZI

1. Kuishi kwenye nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama
2. Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji uliopangwa
3. Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali ikiwa pamoja na kushitakiwa mahakamani, kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.

Hayo ndio Mambo muhimu ya kuyafahamu kuhusu 'Kibali cha Ujenzi' (Building Permit), Epuka usumbufu fuata sheria!.JENGA KWA RAMANI.
 
Kwa utaratibu huo mbona ni kama hati ya mashitaka ya ufisadi ya kina lugemalila na sethy wa IPTL, maana kwa jinsi manispaa zetu zilivyo hizo hatua kufatwa na mtanzania wa kawaida inakuwa ni mtihani aisee.

Usithubutu kujenga bila kupatiwa kibali na halmashauri, usipofanya hivyo utawekewa x nakupigwa fain, nakupewa stop Oder.
 
zumbemkuu aaaah yote hayo hayana umuhimu Sana,wangapi wanajenga bila vibali na mambo yapo mukide tu.
 
Salaam wana jukwaa, nina kiwanja maeneo ya Mbweni nataka nianze ujenzi mdogo mdogo nyumba ya kuishi.
Kabla sijaanza chochote nimekuja humu jukwaani kuomba ufafanuzi jinsi ya kupata KIBALI CHA UJENZI.
Kiwanja kimepimwa? Kama kimepimwa unaweza fuatilia kibali.
 
Kwa utaratibu huo mbona ni kama hati ya mashitaka ya ufisadi ya kina lugemalila na sethy wa IPTL, maana kwa jinsi manispaa zetu zilivyo hizo hatua kufatwa na mtanzania wa kawaida inakuwa ni mtihani aisee.
Procedure ndefu na ukijumlisha na ukiritimba wa nenda rudi nenda rudi kama harawa pesa yote imeisha ndio maana watu wanajenga tu.
 
Kama uko busy nipe hiyo kazi ya kufuatilia kwa sharti la kupewa tender ya kukujengea hiyo nyumba. Malipo yote ya hicho kibali ni juu yako
Kinachukua muda gani kukipata na gharama zake?
 
Kupitishwa na enginer wa manispaa na kulipia bank hata week haifiki kama document zote unazo. Kibali kinachelewa lkn ukishalipia bank unaweza endelea na ujenzi kwani tayari enginer ameshapitisha
 
Kurzweil,

Asante sana kwa uzi huu wa kuelimisha umma.

Nami naomba nichangie japo kidogo kuhusu swala la kibali cha ujenzi. Nianze na swala la Planning Consent,hii ni ridhaa ya awali inayotakiwa kuombwa kwenye mamlaka husika kama Manispaa na Halmshauri za miji,majiji, mamlaka za utawala nk.

Planning Consent ni kwa ajili hasa kwa ajili ya miradi mikubwa ya ujenzi wa majengo na si kwa miradi midogo kama ya nyumba moja ndogo ya kama vyuma vitatu vya kuishi mtu au familia moja. Lakini angalizo,nyumba hiyo hiyo moja hata kama ni ndogo kiasi gani,zikiwa kama elfu moja kwenye eneo moja zitachukuliwa kuwa ni mradi mkubwa wa makazi.Mfano wa Nyumba zinazojengwa na shirika la nyumba.

Lengo mojawapo la kuomba Planning Consent ridhaa ya awali ni kwa ajili ya kujiridhisha na maswala kama ya ardhi husika kulingana na mipango ya matumizi ya ardhi inayokusudiwa na pia maswala ya mazingira. Ikumbukwe siyo kila mradi wa ujenzi wa majengo utakubaliwa na kupewa kibali.

Hivyo,kabla ya muendelezaji hajafanya au kuingia gharama kubwa za kuandaa michoro ya ujenzi kwa ajili ya kuomba kibali cha ujenzi na kusudi asije kukataliwa, anatakiwa awasilishe michoro ya awali ambayo kitaalamu inaitwa outline/sketch proposal pamoja na maelezo ya awali ya mradi anaokusudia kuombea kibali kwa mamlaka husika ili tathmini na kumpa ridhaa ya awali Planning consent ifanyike na ndipo apewe na kuendelea na hatua ya kutayarisha michoro kwa ajili ya kuombea kibali cha ujenzi.

Nawasilisha,

Wasalaam,

Mwenzetu
 
Back
Top Bottom