Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Ni jambo lenye lengo na nia njema, ila kwa Tz yetu, limeshageuzwa kikwazo kwa wenye hitaji la kujenga na njia ya kinipitia rushwa kwa waliopewa dhamana ya usimamizi.
 
Ahsante Sana kwa thread nzuri.hawa jamaaa waache Ukiritimba mf unalipa kuchorewa Ramani lakini ndani ya miaka 3 hujapata,Sasa kibali SI ndo kitachukua miaka 10?
 
Kuukamirisha huo mchakato mpaka kuanza ujenzi, mtu unakuwa ushapigwa pesa ambayo huenda ikaringana na gharama za ujenzi wa nyumba mpya

_ where ever you are remember me_
Hata Mimi nilikuwa nawaza hivyo hivyo
 
Habarini za jioni,

Hapa nilipo nimechanganyikiwa kwa kweli. Mimi ni mkazi wa Kisewe-Temeke. Nimerudi mihangaikoni nimekuta barua ya kudaiwa kibali cha ujenzi,niliponunua kiwanja nilijaribu kuuliza serikali za mitaa kama kuna utaratibu wa kua na kibali cha ujenzi kabla hujajenga wakaniambia utaratibu huo hakuna; nimejenga nimehamia mwaka huu January, leo nakuta barua niende Manispaa tena kesho bila kukosa.

Kiukweli nimevurugika kichwa ukizingatia hali zenyewe hizi zilivyo ngumu. Naomba nifahamishwe japo Mukhtasari nijiandae kukabiliana na yapi, maana sielewi elewi kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Mkuu, Hapo nenda na hati ya kiwanja au nyaraka zozote za umiliki wa ardhi yako, ambatanisha na ramani ya nyumba yako uliyojenga na ujiandae kulipia kibali cha ujenzi huo na faini juu yake maaana hukutekeleza inaweza fika laki na 20.
 
Natumai wajuzi wa haya mambo watakuja, week hii baada ya mvua nikaona kibanda kinavija nikjikusanya kuweka bati. Daaaa serikali ya kata walihamia hapo wakisema fine 1.5m.

Wakawashusha mafundi kwa lugha ya dharau shukeni shukeni haraka sana. Wakasema hata kama unapaka rangi bila kujali unapaka bati au ukuta lazima upate kibali.

Kwa kifupi waliomba rushwa.
 
Pole sana. Beba laki mbili uende ukayamalize haya mambo.
In the end of a day hakuna atayekuambia ubomoe...
 
Hapo kinatakiwa kibali cha kuhamia au kibali cha ujenzi? Walikua wapi kipindi unajenga? Hizi chuku zingine wanajitafutia tu. Kama kweli wako makini na ni utaratibu ambao uko kwa wote, walitakiwa tokea mwanzo wakuombe au kukutaka uweke kibali cha ujenzi.
 
Ni Matapeli tu hao Mkuu, wametanda karibu maeneo yote yenye Makazi mapya, iwasikuvunje nguvu wala kukukatisha tamaa.

Kwa uhakika zaidi jaribu kutembelea ofisi za Ardhi, mfano Manispaa na idara nyingine kama Serikali za Mtaa, kwa taarifa zaidi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujinga; kama umeshahamia usiwaze, hiyo barua ichane endelea na shughuli zako, vinginevyo labda kama kuna ujenzi unaendelea, lakini kama umeshahamia, na hakuna ujenzi wewe chana hiyo barua endelea na shughuli zako! Utaratibu Wa kibari cha ujenzi maeneo ya skwata ulikuwa na lengo zuri sana; ambalo lilikuwa ni kupunguza migogoro ya ardhi, lakini utekelezaji wake umekuwa kinyume na imegeuka kero!

1. Unatakiwa kuaandaa ramani architectural drawing inayoonesha view zote ikiwemo site plan zilizogongwa mihuri ya architect, hii gharama hufikia hadi 400000~600000/= kwa nyumba za kawaida
2. Utatakiwa kuwa na nakala tatu, ukiambatanisha na hati ya kiwanja na barua kutoka see/ mtaa

3. Gharama za kuwapeleka site hao jamaa bila kuwatoa hawaji, na kama wakija lazima watafte kasoro mfano; uwepo Wa njia,ushahidi wawakute majilani site yaani waache kwenda job kwa ajili yako.

4. Utapaswa ulipie kibali wanachaji kwa square meta makadirio nyumba nyingi 88000~150000/=
HIYO MILOLONGO UKICHUMLISHA INAKATISHA TAMAA! Ilitakiwa mwanachi achangie malipo yasiyozidi 20000/=
CHA AJABU KULIKO VYOTE, Gari la kuja kufanya savei wanakujibu halina mafuta, lakini ukijenga bila kibali huwa wanakuja fasta sijui huwa wanapata wapi mafuta!

USHAURI WANGU CHANA HIYO BARUA ACHANA NAO HAWANA CHA KUKUFANYA USHAJENGA IMETOKA HIYO
 
Back
Top Bottom