Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha ujinga; kama umeshahamia usiwaze, hiyo barua ichane endelea na shughuli zako, vinginevyo labda kama kuna ujenzi unaendelea, lakini kama umeshahamia, na hakuna ujenzi wewe chana hiyo barua endelea na shughuli zako!
Utaratibu Wa kibari cha ujenzi maeneo ya skwata ulikuwa na lengo zuri sana; ambalo lilikuwa ni kupunguza migogoro ya ardhi, lakini utekelezaji wake umekuwa kinyume na imegeuka kero!
1. Unatakiwa kuaandaa ramani architectural drawing inayoonesha view zote ikiwemo site plan zilizogongwa mihuri ya architect, hii gharama hufikia hadi 400000~600000/= kwa nyumba za kawaida
2. Utatakiwa kuwa na nakala tatu, ukiambatanisha na hati ya kiwanja na barua kutoka see/ mtaa
3. Gharama za kuwapeleka site hao jamaa bila kuwatoa hawaji, na kama wakija lazima watafte kasoro mfano; uwepo Wa njia,ushahidi wawakute majilani site yaani waache kwenda job kwa ajili yako.
4. Utapaswa ulipie kibali wanachaji kwa square meta makadirio nyumba nyingi 88000~150000/=
HIYO MILOLONGO UKICHUMLISHA INAKATISHA TAMAA! Ilitakiwa mwanachi achangie malipo yasiyozidi 20000/=
CHA AJABU KULIKO VYOTE, Gari la kuja kufanya savei wanakujibu halina mafuta, lakini ukijenga bila kibali huwa wanakuja fasta sijui huwa wanapata wapi mafuta!
USHAURI WANGU CHANA HIYO BARUA ACHANA NAO HAWANA CHA KUKUFANYA USHAJENGA IMETOKA HIYO
Nafahamu hii iko kwa (skwata) wanaotaka/wanaofanya ujenzi . Sio kwa waliokwisha jenga! Ila kwa planned areas hata kama umekwisha jenga, ila uko kinyume na regulations watakuja kukubomolea!
Hakina gharama kubwa sijui labda njia ulizopitia weweShida malipo ni makubwa mno. Kiwanja ununue mwenyewe kujenga ujenge mwenyewe kwa jasho lako halafu kupata ruhusa tuu ya kujenga hela kibaaooo
maelezo ndio yamechambuliwa kwa urefu lakin kiuhalisia sio mrefu mana ramani unakuwa unazo na ndio maana sisi kama kampuni tupo kusaidia kwa wale ambao watakuwa busy na majukumu mengineMlolongo ni mreefu mno!...Kusoma tu hayo maelezo yanachosha; Je kufuatilia itakuwaje?
Uaratibu wa hovyo haupo kumsaidia mwananchi Bali kumnyonya!
SITAKI KIBALI CHA HIVI MIMI; NITANUNUA KONTENA NILALE
Nadhan thread ijayo itakuwa ya kuongelea vijijin yaan mashambani kama ulivoandika ww mkuuUmeongelea miji na majiji,vipi kwa wanojenga mashambani? Yaani bush
Ukishakuwa kwenye sekta hizi lazima ujue madhara yake kwa hiyo tunafuata taratibu zoteMaofisa wa TRA huwa wakwepaji wa kodi wazuri kwenye biashara zao, na ndiyo haohao wanahamasisha wananchi kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi, hata hapa usishangae kusikia mleta mada ana nyumba alizojenga bila vibali.
Ingawa ni kosa lakin inabid nikuambie tu kuwa na kibali cha ujenzi ni lazima maeneo ya mijini hata kama hapajapimwa mana itakuondolea usumbufu wa watendaji kuja kuchafua kuta zako ni kulipishwa fainiVipi kwa yale maeneo ambayo hayajapimwa na mipango miji.? Bado wanahitaji kibali cha kujenga.?
watakuja na faini utatoaTatizo siyo kibali ila urasimu wa kukipata na rushwa ndiyo maana hatutaki kusikia huo upupu hapa
watakuja na faini utatoaView attachment 1228653