Fahamu kuhusu vicoba na namna ya kupata usajili wa vikundi hivi vidogovidogo

Kuuliza siyo ujinga
1- Tengenezeni katiba ya kikundi chenu ndio iwe sheria Mama. Kisha ipitisheni rasimu ya katiba
2 - Andikeni barau ya kujitambulisha katika ofisi ya serikali ya mtaa ambapo shuhuli zenu zitafanyika. Kikao cha ulinzi na usalama katika serikali ya mtaa kitakaa na kuwajadili.
3 - mkisha pitishwa na mtaa mnaandika tena barua ya kutambulika ofisi ya kata mliyopo. Apo mtaambatanisha katiba, CV za viongozi wenu hasa 3. Mwenyekiti, katibu na mweka hazina.
4 - Baada ya kupitishwa na kata, mtaandika barua wilayani ili kuweza kutambilika kiwilaya
5 - mwisho mtaandika barua kwa msajili wizara ya mambo ya ndani.
Msajili akifanyia kazi na kukuta hamna kasoro hasa katika katiba hapo mtakuwa mmefanikiwa.
 
Ndugu zangu mwenye mfano wa katiba ya kikundi naomba anitumie kupitia ushokola2002@gmail.com maana nipo kwenye harakati za kuunda kikundi cha ujasiriamali ili tupate fursa ya kupata mikopo.
 
Mnaunda kikundi ili mfanye shughuri zipi? au ni kwa sababu ya mikopo tu? Ok nitakutumia baadae

ndugu yangu nimeamua kuwasaidia vijana kuunda kikundi ili waweze kukopesheka kitajihusisha sana na kilimo(mahindi,mtama na alizeti) na ufugaji(kuku na ngombe wa maziwa) nakuomba unitumie kupitia hii email ushokola2002@gmail.com
 
Wana jf nami naomba msaada namna nzuri ya kuandaa/kuboresha katiba ya kikundi.tayari tuna mtaji wa milioni sita na tunahitaji kufanya usajiri wa kikundi chetu ni cha kuweka na kukopa kwa mfumo wa kununua hisa kila wiki.Naomba msaada wa mfano wa katiba na ushauri wa kuboresha kikundi.Email yangu:miltonjacob909@yahoo.com
 
fafanua ni NGO au SACCOS? nijue nikusaidieje
 
Kikundi hiki msingi wake ni kama Vikundi vya Vikoba.tunakutana wanakikundi wote kila wiki mara moja,kila mwanachama anakuwa ametengewa hisa 5 @hisa 2000.na tukisha nunua hisa,pesa hiyo wanakikundi wanaokuwa wameomba mkopo tunawapatia.kwa riba 5 asilimia.kila m/chama hupatiwa mkopo mara tano ya hisa zake.marejesho ni kila wiki hadi kumaliza muda wa mkopo uliokopa. Kwa ufupi ni hivyo,mfumo wetu ni Vikoba au tunaita villagge saving & loans association bank.ni loccally as mutual groups.
 
Mnaunda kikundi ili mfanye shughuri zipi? au ni kwa sababu ya mikopo tu? Ok nitakutumia baadae


Namomba na mimi ndugu unisaidie kwa EMAIL ndondolej@gmail.com
 
aisee wakuu mi niko mwanza na hapa mtaani kwetu tupo wafanyabiashara 10 amabao tuna kitu tunaita mchezo ila mi nadhani ni upatu kwani kila jumamosi mwanachama anatoa 50,000 na kuna mtu atakabidhiwa ambapo atapewa cash 500,000 tupo mzunguko wa pili mwishoni na kila member anatii mashariti na vigezo vizuri mno!
ningempata mtaalamu aje atukalishe na katupa darasa la VICOBA ingekuwa safi kweli kwani hiyo upatu wetu ni pesa ile ile haikuwi.
ila kwa uzoefu wangu kila member ana uhakika wa kupata 50,000 @ week
 

Mkuu Marire, Habari za Jiji la "Rock City"?

Pamoja na baadhi ya michango iliyopo kwenye uzi huu, jaribu kutafuta Uzi wenye Kichwa cha Habari
"Ifahamu VSLa (Village Saving and Loan Association)/VICOBA". Uzi huo uko kwenye Jukwaa la Ujasiriamali na ulianzishwa tarehe 18/04/2012. Uzi huo utakuelewesha baadhi ya mambo muhimu unayotakiwa kuyafahamu kuhusu Mfumo wa Hisa (VICOBA).

Naomba sasa nikusemeshe machache. Kwanza ni vizuri kuwa tayari wewe na Wafanyabiashara wenzako mmeanzisha, kwa nia nzuri kabisa, "mchezo". Huo ni mwanzo mzuri. Hata hivyo ninadhani kuo "mchezo" wenu haustahili kuitwa "upatu". "Upatu" ni kitu hatari, na kukitekeleza ni kuvunja Sheria za Nchi (usiniulize Sheria namba ngapi, ya mwaka gani, n.k. - sijui). Ila ukiona kitu kinaitwa "Upatu" kimbia mbio kama Bolt - ni janga!

"Mchezo", kama huo wa kwenu, una mazuri kadhaa. Hata hivyo wingi wa mapungufu yake unazidi hayo wazuri machache. Kuokoa muda, sitataja mazuri. Ninakutajia baadhi tu ya mapungufu ya "mchezo" wenu: 1. Pesa yenu (mitaji) itabaki pale pale, haitakuwa wala kuongezeka, kama ulivyosema. Leo ni tarehe 20/03/2014. Tuseme "mcheze" kwa miaka mitatu mfululizo, tarehe kama ya leo baada ya miaka hiyo mitatu, mchango wako kwenye Kikundi chenu utakuwa palepale, yaani Sh. 50,000/= bila kujali anguko/ongezeko la thamani ya Shilingi ndani ya muda huo 2. "Mchezo" hauna dhamana. Kwa mfano, mmecheza hadi mtu wa saba halafu inatokea mmoja anapata tatizo
linalopelekea kushindwa kuchanga kama kifo, ajari, kuugua, n.k., inakula pande yenu hasa pande ya wale ambao zamu yao inakuwa haijafika 3. "Mchezo" kama huo wenu unamfanya Mwanakikundi atarajie kiasi fulani cha pesa kwa muda fulani, hakuna mabadiliko 4. "Mchezo" unamlazimisha Mwanakikundi achukue/apokee fedha, Sh. 500,000/=, zamu ikifika hata kama haihitaji kiasi hicho siku hiyo 5. "Mchezo" ni jela ya aina yake. Yaani mnapoanza mzunguko, Mwanakikundi anakuwa hana uhuru wa kutoa mchango pungufu, au kutotoa kabisa, hata kama mambo yake ni magumu. Sio kila siku zinalingana. Hii inaweza kumsababishia Mwanakikundi huyo Msongo wa Mawazo na hivyo kusababisha matatizo makubwa zaidi 6. "Mchezo" mara nyingi hauna fungu la pembeni la kusaidiana inapotokea Mwanakikundi amepata dharura kama kuugua, kuuguliwa, kufiwa, kufa, kupeleka mtoto Shule, n.k.

Nia yako ya kubadilika kutoka kwenye "mchezo" kwenda kwenye Mfumo wa Hisa/VICOBA ni nia endelevu. Ni kweli, mngepata Mtaalamu hapo Mwanza atakayewapa Darasa na kisha kuwasimamia kwa kipindi hadi mtakapo komaa, ni wazo zuri sana. Miaka kama minne iliyopita nilishuhudia Vikundi vya Mwanza vinalipa Wataalamu wa Hisa/VICOBA kati ya Sh. 50,000/= - 100,000/= kwa kila siku anayokuja kufundisha Kikundi! Sifahamu kama hilo bado lipo. Jaribuni kuongea na Mashirika mbalimbali kama CARE na CRS, wako Isamilo, ili waweze kuwasaidia. Jaribu vilevile kwenye Halmashauri ya Jiji, Idara ya Maendeleo ya Jamii, unaweza pata msaada wa Wataalamu, lakini sio kwa bei hiyo niliyoitaja - huo ni wizi!

Hebu sasa tupige hesabu ya kawaida tu ya Kikundi chenu kama kitabadilika kutoka "analogia" (Mchezo) kwenda "dijitali" (Mfumo wa Hisa/VICOBA)

Tuseme: 1. Hisa moja iwe Sh. 10,000/= 2. Ratiba ya kukutana Kikundi chenu, ili kununua Hisa (kuweka Akiba) ibaki siku moja kwa Wiki kama mnavyofanya sasa hivi 3. Kila Mwanakikundi akaendelea kujiwekea kiasi kilekile kama sasa yaani Sh. 50,000/= kwa wiki, yaani Hisa 5 (Sh. 10,000/= X Hisa 5 = Sh. 50,000/=) 4. Idadi ya Wanachama ikabaki ile ile ya Watu 10 mliopo; Ina maana jumla ya Mtaji wenu kama Kikundi kwa Wiki, utakaotokana na Akiba/Hisa zenu, utakuwa: Sh. 50,000/= x Wanachama 10 = Sh. 500,000/=. Kwa mwezi itakuwa: Sh. 500,000/= x Wiki 4 = Sh. 2,000,000/=. Kwa Mwaka mtakuwa na Mtaji wa: Sh. 2,000,000/= x Miezi 12 = Sh. 24,000,000/=. Katika kiasi hicho, wewe Mkuu Marire, kama utakuwa na nidhamu ya kujiwekea Akiba/Kununua Hisa 5 (yaani Sh. 50,000/=) kila wiki kwa Mwaka mzima, Jumla ya Sh. 2,400,000/= taslimu zitakuwa ni za kwako - mgawo wako bila chenga!

Mwaka ukifikia mwisho, yaani mkifikia mwisho wa Mzunguko, mnaweza kufanya maamuzi ama 1. kugawa Akiba/Hisa kwa kadri ya kila Mwanakikundi alivyoweza kujiwekea 2. kugawana sehemu ya Akiba/Hisa hiyo ili kinachobaki kiweze kuendeleza Mtaji wa kukopeshana au 3. kutogawana kabisa na fedha hiyo ikaendelea kukopeshana kwa Wanakikundi.

Uzoefu wangu kwa Jiji la "Rock City", Jiji Safi kuzidi yote hapa Afrika ya Mashariki, Jiji la Sato, Sangara na Mumi, kiasi cha Sh. 2,400,000/= unaweza kulipia Karo za Watoto wawili wa Shule ya Msingi katika Shule za "International - Bongo" zinazofundisha kwa "yes" na "no", unaweza kununua bonge la kiwanja Luchelele, Igoma, Kiseke, n.k. au hata kulipia Mahari toto zuri kabisa la Kisukuma (na bado chenji ikabaki)! Unaweza vile vile kuirudisha kwenye Biashara yako ili kupanua Mtaji! N.k.

Hesabu iliyoko hapo juu imeongelea Akiba/Hisa zenu tu mlizojiwekea kwenye Kikundi. Kikundi cha Hisa/VICOBA ni Kikundi cha Kuweka (Akiba) na Kukopeshana. Fedha ya kukopeshana, kwa masharti nafuu, inatokana na Akiba/Hisa zenu Wanakikundi mnazojiwekea kwenye Kikundi chenu. Tunaposema "kukopeshana kwa masharti nafuu" ni pamoja na Rida/Ziada ya Mkopo unaotolewa kwa Mwanakikundi kuwa kidogo ikilinganishwa na viwango vinavyotozwa na Taasisi za Fedha yaani Mabenki, SACCOS, n.k. na Wakopeshaji wa Mitaani (Loan Sharks). Vilevile Masharti nafuu ni pamoja na muda unaotolewa kwa Mwanakikundi "kuzungusha" huo Mkopo kwenye Biashara/Shughuli yake kabla ya kurejesha. Kiwango cha Riba/Ziada ya Mkopo inayopendekezwa, mara nyingi, ni 10% na muda ambao Mwanakikundi anaruhusiwa "kuzungusha" Mkopo wake kwenye Biashara zake mara nyingi ni miezi mitatu.

Ina maana, Mkuu Marire, ukikopeshwa leo, tarehe 21/03/2014, Sh. 1,000,000/= unaruhusiwa kurejesha Mkopo huo tarehe 21/06/2014! Kati ya leo, unapokopeshwa na Kikundi, hadi siku ya kurejesha, utatakiwa uwe unalipa Riba/Ziada ya Mkopo kila Mwezi kutegemea na Katiba yenu. Mfano kama Katiba yenu inasema Riba/Ziada ya Mkopo ni 10%. Hivyo tarehe 21/04/2014 utalipa Riba/Ziada ya Mkopo ya Sh. 100,000/=, utalipa tena Riba/Ziada ya Mkopo ya sh. 100,000/= tarehe 21/05/2014 na tarehe 21/06/2014 utalipa Mkopo yaani Sh. 1,000,000/= kujumlisha Riba/Ziada ya Mkopo ya mwezi huo wa tatu ya Sh. 100,000/=.

Fahamu kuwa Riba/Ziada ya Mikopo kwa Mikopo yote inayotolewa na Kikundi kwa Wanakikundi, inapolipwa inalipwa kwenye Kikundi na inachanganywa na Hisa/Akiba za Wanakikundi na hivyo kupanua Mtaji wa kikundi kukopesha mikopo zaidi kwa Wanakikundi.

Hivyo kiasi cha fedha kinachogawanwa na Wanakikundi mwishoni mwa mwaka ni = (Hisa/Akiba za Wanakikundi + Riba/Ziada ya Mikopo + mapato mengine kama faini, n.k.) Kama Kikundi kikiendesha shughuli zake kwa ufanisi, yaani 1. Wanakikundi wakanunua Hisa/Kuweka Akiba ipasavyo 2. Wanakikundi wakakopa kwa bidii; na 3. Wanakikundi wakarejesha kwa ufanisi na kwa wakati, basi Faida/Ziada itakayopatikana kwa Mwaka mzima ni kati ya 30% - 40%, yaani kila Sh. 1 itazaa kati ya senti 30 hadi senti 40!

Mkuu Marire, tukirudi kwenye hesabu zako hapo juu, yaani Hisa/Akiba yako ya Sh. 2,400,000/= itakuwa "imezaa" kati ya Sh. 720,000/= hadi Sh. 960,000/=! Ina maana, kama mtaamua kugawana na kuanza upya, Mkuu Marire, siku ya kugawana utaondoka na "fuko" la kati ya Sh. 3,120,000/= hadi Sh. 3,360,000/=!

Ni benki gani hapa Duniani inaweza kukukopesha kwa masharti hayo na kisha mwishoni mwa Mwaka kukulipa faida ya Akiba yako kwa kiasi hicho?

Mtu anaweza kuuliza mapungufu ya Mfumo wa Hisa/VICOBA ni yapi. Kusema kweli, kwenye mapungufu ya Mfumo huo mimi huwa ninakuwa kipofu! Ndio, mara moja, katika Kikundi chetu tulichokivunja baada ya kuwa tumekuwa nacho kwa miaka mitatu, tumewahi kupunguza kiasi cha kugawana baada ya baadhi ya Wanakikundi kutokomea na mikopo. Kwa kuwa Kikundi cha Mfumo wa Hisa/VICOBA mara nyingi ni Kikundi kisicho rasmi, yaani hakijaandikishwa popote Kisheria, kuchukua hatua za Kisheria kwa Wanakikundi kama hao ni ngumu sana. Tulipata "hasara" hiyo baada ya kuwa sisi Wanakikundi 1. Tumeacha kusimamia shughuli za kila siku za Kikundi baada ya kuwa tumebweteka na mafanikio makubwa ya miaka miwili mfululizo 2. Tumekaribisha Wanakikundi wasio waaminifu 3. Kikundi kimekuwa kikubwa sana cha Wanachama zaidi ya 35 na hivyo usimamizi ukawa mgumu 4. Mtaji wa Kikundi umekuwa mkubwa sana na hivyo kupelekea Wanakikundi kukopa Mikopo mikubwa iliyowazidi uwezo wa kuisimamia na hivyo kushindwa kurejesha na 5. Kikundi kutokuwa na mbinu za kuwapa Elimu zaidi Wanakikundi ili waweze kumudu Mikopo mikubwa na biashara kubwa zaidi!

Ni hayo tu kwa sasa. Naachia na wengine wenye ufahamu zaidi kwa kuwa ufahamu wangu unatokana na uzoefu zaidi! Wasalimie Jiji la "Rock City", Jiji la Sato, Sangara, Mumi, Nembe na Totoz za Kisukuma! Ciao!
 
mkuu. MahinaVeterani mchanganuo wako nitawapa wanakikundi watatu amabao pia wanaingia huku ili na wao watoe mawazo yao.
nashukuru sana kwa mchango wako!
 
Last edited by a moderator:
mkuu. MahinaVeterani mchanganuo wako nitawapa wanakikundi watatu amabao pia wanaingia huku ili na wao watoe mawazo yao.
nashukuru sana kwa mchango wako!

Tuko pamoja Kaka.

Najua maelezo hayajajitosheleza. Kuna mambo mengi sana ambayo siyo rahisi kuyaweka yote hapa. Kwa mfano, namna ya utunzaji wa Kumbukumbuku za Kikundi - za Kifedha, nk.; sikuongelea suala la Mfuko wa Jamii ambao vilevile ni wa muhimu sana hasa Mwanachama anapopata dharura, Katiba ya Kikundi ambayo vilevile ni muhimu sana, namna ya kukokotoa fedha mwishoni mwa Mwaka iki Wanakikundi mgawane; namna ya kukotoa mahesabu endapo Mwanachama anapotaka kutoka kwenye Kikundi, n.k.

Ushauri wangu, tafuteni Mtaalamu mkae naye awape darasa la kutosha ili muweze kufanya maamuzi stahiki. Hili mngelifanya kabla ya kuanza mzunguko mwingine wa "mchezo" wenu.

Mkifikia maamuzi, tutaarifiane ili kama nitakuwa nimepata Mtu wa kuwaelimisha hapo Mwanza niwaunganishe!

Usiku mwema!
 
Marire nitafute kwenye sim no 0783544889 ntakupa maelekezo hata mm nimo kwenye vikoba
 
somo zuri, hatuwezi kuanzisha VICOBA ya JF
vicoba inabdi watu wawe wanaish sehemu au kuwe na umbali mfupi baina ya wanachama. hivyo vicoba ya jf itakuwa ngumu sababu watu wanaish mikoa au nchi tofauti , labda organize ulipo ufahamu ni watu wangapi wapo tayari na labda hao watu wanatumia jf au lah.
 
Marire nitafute kwenye sim no 0783544889 ntakupa maelekezo hata mm nimo kwenye vikoba

Marire, changamkia hii ofa na hasa kama yuko Mwanza itawarahisishia sana. Cha msingi pateni Elimu juu ya Mfumo wa Hisa/VICOBA ndio mfanye maamuzi. Lakini, nianzidi kukuhakikishia Mfumo huu ni "the best"!
 

nimekuelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…