Naambiwa ukitumia VPN network inakuwa slow sana. Limekaaje hili
VPN INAPUNGUZA KASI YA NETWORK?
Ndio na hapana - yote inategemea na mambo kadhaa. Unaweza kutumia VPN halafu network ikaenda kwa kasi ileile, au unaweza uka-connect kwenye VPN halafu ghafla ukaona network inaangukia pua. Kwa ujumla, ni vizuri kutarajia mabadiliko ya kasi ya mtandao unapotumia VPN, lakini usitarajie kila unapotumia VPN basi network inapungua kasi papo kwa papo. Wakati mwingine unaweza usigundue kama spidi imepungua.
SASA KWANINI VPN INAPUNGUZA SPEED YA NETWORK?
Nakupa sababu 7 za kwanini VPN inaivuta shati network yako;
1. Location ya Server.
Umbali halisi kati yako wewe na VPN server unayotumia unachangia sana kuamua ni kasi kiasi gani ya network utapata. Kwanini? Kwasababu inachukua muda mrefu zaidi kwa zile data packets kusafiri kati yako na VPN server. Kadiri unavyokuwa mbali na server ndivyo speed ya network inayokuwa slower.
2. Ukomo wa Server Bandwidth.
Kama VPN server unayotumia ina kitu tunaita bandwidth limitations, basi speed ya network lazima ipungue pale unapogonga limit au server ikizidiwa (Mkiwa watu wengi mnaitumia kwa wakati mmoja). Pia server kama server yenyewe ina impact kwenye speed ya network kulingana na aina yake; kama ni server ya ubora mdogo basi na kasi itaathirika kulinganisha na High quality servers.
3. Aina ya Encryption.
Inategemea aina ya encryption ya VPN protocol unayotumia - kama unatumia stronger encryption basi kasi ya network inaangukia pua. Lakini si mara zote, na wakati mwingine huwezi kugundua kabisa. Kwa ujumla encryption aina ya OpenVPN protocol ndo mara nyingi inapunguza kasi ya network, wakati PPTP ina kasi kubwa. Lakini PPTP ni hatari zaidi kwasababu haina reliable encryption. Aina zingine ni IKEv2, L2TP/IPSec na SoftEther protocol.
4. Firewall.
Firewalls mara nyingi haziathiri kasi ya VPN lakini huwa zinaweza kuharibu mambo kama imesetiwa kuingilia traffic ya VPN au performance ya CPU yako. Niongezee hapa kuwa kasi ya CPU yako pia ni sababu inayochangia mabadiliko ya kasi ya network. Kama unatumia CPU za kizamani badi ni sababu mojawapo ya kukuchelewesha.
5. Network Setup
Kuna watumiaji wa VPN wamegundua kuwa kuna utofauti ukiwa unatumia internet ambayo connection yake ni ya router ambayo ina LAN cable ukilinganisha na kutumia WiFi. Jaribu kubadilisha connection yako, hamia kwenye kutumia WiFi, utaona utofauti.
6. VPN Routing Algorithms
Kuna uwezekano VPN provider wako ana-route connection yako kati ya server nyingi, na wakati mwingine ana-route data zako pia. Hiyo safari ndo sababu mojawapo ya ku-slow down kwa VPN speed. Hii ni kawaida sana kwa FREE VPNs... vya bure vina gharama zake.
7. Kasi ya netwrok yako.
Mwisho wa siku, unatumia mtandao gani? TTCL, Halotel, Voda, Tigo au Zantel. Hakikisha unatumia mtandao ambao una kasi, tunaongelea angalau ya 3G kwenda juu. Siwezi sema mtandao gani una kasi zaidi - inategemea uko wapi.
Bila shaka nimejibu swali lako mkuu.