Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
IJUE NCHI YA ETHIOPIA
Ethiopia ni nchi ya pembe ya afrika, ambayo imepakana na Eritrea na Djibouti kwa upande wa Kaskazini, Somaliland kwa upande wa Kaskazini mashariki, na imepakana na Somalia kwa upande wa mashariki, imepakana na Kenya kwa upande wa kusini, imepakana na sudani kusini kwa upande wa magharibi, na imepakana na Sudan kwa upande wa Kaskazini magharibi kwa kifupi tunaweza kusema kuwa Ethiopia ni nchi ambayo haijaguswa na bahari (landlocked country) kwa sababu imezungukwa kila upande
Ethiopia ina Zaidi ya watu milion 117 na inashika namba 12 duniani kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu na kwa afrika inashika nafasi ya pili ikitanguliwa na Nigeria
Mji mkuu wa Ethiopia ni Addis Ababa na ndio yalipo makao makuu ya umoja wa Afrika
Raisi wa Ethiopia ni Sahle-Work Zewde na Waziri mkuu wake ni Abiy Ahmed
Yafuata ni Mambo machache kuihusu Ethiopia
1) ETHIOPIA NDIO CHIMBUKO LA IMANI YA RASTAFARI
Tofauti na watu wengi wanaoamini kuwa CHIMBUKO la RASTAFARI ni Jamaica ila ukweli ni kuwa imani ya kirastafari CHIMBUKO lake ni Ethiopia, japo haipingiki kuwa imani hii ya kirasi imeshika mizizi sana katika nchi ya Jamaica.
Neno Rastafari limetokana na maneno mawili nayo ni Ras na Stafari. Neno rasi maana yake ni mwana mfalme na neno Stafari ni jina la aliyekuwa mfalme wa Ethiopia Haile Selassie wa kwanza ambaye jina lake halisi aliitwa Tafari Makonnen.
Wenye imani hii ya Rastafari baadhi yao wanaakini kuwa Haile Selassie ni Mwana Wa Mungu
2) ETHIOPIA IMETAJWA KWENYE VITABU VITAKATIFU MBALIMBALI
Katika bibilia ya Mfalme James neno Ethiopia limetajwa mara 45 kama nchi ya kusini mwa Misri. Pia kuna story ya Malkia Sheba aliyemtembelea mfalme Solomon. Inaaminika kuwa Malkia Sheba alikuwa mtawala wa Ethiopia
3) MOJA YA DHEHEBU LA KALE ZAIDI LA UKRISTO LINAPATIKANA ETHIOPIA
Tewahedo ni miongoni mwa DHEHEBU la kale linapopatikana Ethiopia kanisa hilo pia hujulikana kama Ethiopian Orthodox Church, mwaka 330 baada ya kuzaliwa kwa Yesu Mfalme Ezana wa Auxime alibadili dini na kufanya UKRISTO kama dini rasmi ya nchi, kufika karne ya 4 kanisa la kwanza lilijengea Ethiopia. Hadi leo hii asilimia zaidi ya 60 ya raia wa Ethiopia ni wakristo huku asilimia 40 ni wanaoamini kwenye kanisa la Ethiopia Orthodox Church
4)ETHIOPIA NDIO NCHI YA KWANZA KUUKUBALI UISLAMU KUWA NI DINI
Ukiwa uislamu bado ni mgeni na haujulikani na hata ndani ya Maka ukiwa bado unapigwa vita. Mtume Muhammad (s.a.w) aliwaagiza baadhi ya maswahaba wake waende Negash watakutana na mfalme mtenda haki... Mfalme Armah aliupokea ugeni ule na kuwapa hifadhi, hata maadui wa uislam kwa kipindi kile walipokwenda kuwachukua kule Ethiopia ili wawarudishe Makka yule mfalme alikataa
Lakini pia muadhin wa kwanza katika historia ya uislamu ni Bilal Ibn Rabah ambaye alikuwa anatoka Ethiopia (kwa wasiojua adhana ni ule muito unaosikia wakati wa swala unapokaribia). Lakini pia msikiti wa kwanza kujengwa nje ya nchi za kiarabu ulijengwa Ethiopia
Hadi leo asilimia 31 ya raia wa Ethiopia ni waislamu
5)MWAFRIKA WA KWANZA KUSHINDA MEDALI YA DHAHABU KWENYE MASHINDANO YA OLIMPIC
Hadi Leo hii ni zaidi ya medali 120 za DHAHABU ambazo waafrika wameshinda kwenye mashindano ya olimpik..lakini medali ya kwanza ya DHAHABU kutoka kwenye mashindano ya olimpik ilipatikana mwaka 1960 katika jiji la Roma ambapo mwanariadha kutoka Ethiopia Abebe Bikila alifanikiwa KUSHINDA. Abebeb Bikila akiwa miguu peku alifaniki kukimbia na kushinda medali hiyo
Abebe Bikila alipata nafasi ya kwenda kushiriki mashindano ya olimpiki baada ya mwanariadha aliyeandaliwa kwenda kuugua ghafla
6) Mwanamke wa kwanza kuwa rubani anatokea Ethiopia. Jina lake ni Asegedech Assefa
7) Mwafrika wa kwanza kuendesha gari anatokea Ethiopia
Ikiwa hadi Leo Kasomi sijui hata kusogeza gari, lakini Mwafrika wa kwanza alifanikiwa kuendesha gari mwaka 1907
Mfalme Menelik wa pili aliletewa gari hilo kama zawadi na marafiki zake kutoka ulaya lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano
8) KALENDA YA WAETHIOPIA INA MIEZI 13
Tofauti na wengi tunaojua kuwa kuna miezi 12 lakin kwa Ethiopia kuna miezi 13
Mwezi wa una siku kati ya 5 hadi 7
Kwahyo KALENDA ya Ethiopia iko nyuma ya kalenda ambayo dunia inatumia kwa miaka 7 na miezi 8
9) WANAHESABU MUDA TOFAUTI
siku yao imegawanyika mara 2 kwa masaa 12, hakuna masaa 24 yaani saa kama tunavyoisoma kwa kiswahili
10) Inasadikiwa kuwa watu wa kale zaidi waliishi Ethiopia, wanaikolojia walipata mabaki ambayo yamewapa nguvu kuamini kuwa huenda watu walianza kuishi Ethiopia
11) ETHIOPIA NDIO NCHI YA KWANZA AFRIKA KUMILIKI NA KUENDESHA Boeing 787 Dreamliner
Kama unakataa wewe kataa ila ukweli ni kuwa Ethiopia ndio nchi ya kwanza kumiliki na kuendesha ndege aina ya Boeing 787 Dreamliner.
Mwaka 2012 walifanikiwa kununua aina hiyo ya ndege na kuipa jina la afrika one
12) Ethiopia ndio nchi mama ya zao la kahawa na umegunduliwa kupitia mbuzi
13) Eskista (dance shoulders) ndio dansi maarufu zaidi nchini Ethiopia ambassador hujumuisha wanaume, WANAWAKE na watoto
14) Injera ndio chakula maarufu zaidi nchini Ethiopia