Fahamu mambo 11 ambayo huyajui kuhusu samaki

Fahamu mambo 11 ambayo huyajui kuhusu samaki

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
1) Samaki hupata huzuni/msongo wa mawazo (depression) kama apatavyo binadamu

2) Kuna Samaki wanaishi zaidi ya miaka 70 ila yupo aliyeishi miaka 112 anaitwa Bigmouth buffalo

3) Kibaolojia kuna makundi (species) 30,000 ya samaki yanayotambulika

4) Kihistoria Samaki ameanza kuwepo duniani miaka milioni 500 iliyopita

5) Samaki halii (crying) kwahiyo ule msemo wa machozi ya samaki kwenda na maji ni fasihi tu ndio imetumika

6) Samaki huwa analala... Japo sio kama binadamu lakini samaki pia huwa analala... Ulalaji wa samaki huwa ni kupunguza mizunguko yake, hupunguza uwezo wa kuhisi jambo, hupunguza metabolism... Na kwa wakati huu ndio rahisi kuwavua kwa nyavu kwan huwa Hawana ujanja ujanja

7) Unajua kuwa kuna Samaki wanabadilisha jinsia kutoka kuwa wa kiume kwenda kuwa wa kike au kike kwenda kuwa wakiume kwa kitaalumu huitwa Sequential hermaphroditism.... Mara nyingi sababu ya kubadilisha huko kwa jinsia hutokana na mazingira

8) Je unajua kuwa baadhi ya lipstick na rangi za kucha zinatokana na magamba ya samaki NA PIA shahawa/manii ya samaki aina ya nyangumi pia hutumika kutengenezea shampoo, lipstick na baadhi ya vipodozi

9) Bunju/ fugu ni miongoni mwa samaki watamu sana ila ni samaki wenye sumu kali sana inayoweza Kukuua muda mchache...Nchini Japan ili upewe idhini ya kumpika samaki huyu unatakiwa uwe na cheti maalum cha kusomea.... Lakin kwa Tanzania anapikwa tu japo sio na kila mtu ila supu yake ina balaa [emoji2][emoji2]

10) Binadamu anaweza kujua ladha 7,000 lakini kambare anauwezo wa kujua ladha 27,000

11) Horse fish ni kama kinyonga tu kwa sababu wanafanana kwa baadhi ya mambo mfano... Mwendo wao kinyonga na horse fish wote hutembea taratibu, kinyonga na horse fish wote wanauwezo wa kujibadilisha rangi kuendana na mazingira, kinyonga na horse fish wote wanauwezo wa kuona mbele na nyuma wakati wa kutembea...... Mkunga nae ni kama nyoka kwa ufanano wao mfano umbo lao, maisha yao, na pia sumu zao

FB_IMG_1628542968112.jpg

 
Kambalae siyo samaki ni chura.

Katika wale ndubwi atakayeota miguu anakua chura atakayekosa miguu anaevolve na kua kambale.

Samaki huhitaji maji kuishi ila kambale waweza mtoa kwenye maji ukamuacha kwenye beseni kwa saa mbili na ukamkuta yupo hai.

Akijifukia kwenye tope ndiyo utamsahau ila siku ukifukua tope unamkuta.

Si ndo tuanze kula vyura sasa
 
Kambale, my favourite fish.

Nikimpata fresh na apikwe tu hivyo hivyo bila viongo vya ajabu ajabu,yaani maji na chumvi ama limao kwa mbali tu na ugali wa muhogo laini, maisha yanakua matamu sana.

Kwangu kambale kisha anafuata Sato, ila watu wa kanda ya ziwa tunajua kwenye mito na ziwani kuna visamaki species nyingine vidogo vidogo vitamu balaa, vingine vina rangi rangi, mabaka mabaka, sijui ningu na majina mengine ambayo sijapata kiswahili chake fasaha.

Hiyo picha hapo huyo ni kamongo na sijui kwa kimombo anaitwaje. Ni mtamu balaa, hana mfupa. Ndugu zangu wajaluo wanasema kamongo asinda nyama, kwa maharage atoka droo, eeh yawah, omera😂. Machiegni nyasae omera.
 
Je samaki reptiles??!!sababu wana magamba??!!km nyoka au mamba!!

Kambare ni au catfish ni samaki ambae anaweza kuishi bila chakula kwa miezi kadhaaa katika kipindi hicho huyeyusha minofu yake mwenyewe ya tumboni na kujila!!

Hiyo picha umeweka huyo samaki anaitwa KAMONGO sijui kwa kizungu
 
Back
Top Bottom