Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ubarikiwe sana mkuu..Anza na bidhaa kidogo, uza bidhaa online, utaepuka kulipa kodi, umeme, licence, n.k
Tafuta maduka ya wholesale ununue, unaweza kuanza na extension wire, switches ata pisi kumi kumi.
Nafikiri hata millioni moja itatosha.
Kama unataka kufungua mlango wa vifaa hivyo chemsha bongo kidogo utapata jawabu.
1.Kodi ya mlango kwa miezi sita
2.umeme kwa muda wa miezi sita.
3. Licence kwa mwaka
3.Mshahara wa Shopkeeper kwa muda wa miezi 6,
4. Matumizi yako kwa muda ya miezi 6.
5. Fanya list ya vifaa unavyotaka kuingiza nenda wholesale shop, jumuisha bei ya vyote.
6. Fikiria kodi itakuwa kiasi gani.
Jumuisha 1-6 na vyengine ambavyo sikuviandika utapata jawabu.
Miezi ya mwanzo utatoa fedha bila kuingiza nyingi, sasa ili biashara iende, usitegemee kwamba itakulisha, inabidi wewe uipe support iyo biashara mpaka isimame.
Cha muhimu zaidi iyo biashara unayotaka kufungua utawapata wapi wateja, inabidi ufungue location nzuri ya kuwanasa wateja. Na mara nyingi milango yake ni ghali
Kama unauza online unakuwa uko sehemu zote changamoto iko kwenye delivery zaidi na uzuri wake hii inakuwa kama part time job, unaweza kuendelea na shughuli zako nyengine
Ahsante sana kakaHuo mtaji unatosha kabisa kuanzisha hiyo biashara.
Cha msingi location iwe ya watu wengi mfano karibu na vituo vya daladala au sehemu yenye population.
Pili kwa sababu ndio unaanza, nunua kibanda cha mabati bei ni Kama 700k hv alafu utafute kijieneo kilicho wazi na ukodi kuweka kibanda chako. Hii itasaidia kupunguza machungu ya Kodi wakati bado unatafuta kujulikana na wateja wako. Bei ya eneo la kuweka kibanda huwa Kati ya 15k-25k.
Tatu, Tenga muda wako nenda kariakoo (Kama unaishi dsm itakuwa rahisi) upate kuzunguka kupata machimbo ya bei za jumla za chini zaidi. Kuna wachina flan mwaka jana walikuwa wanashusha mpaka makasha 20 ya vifaa vya umeme, Bai zao zilikuwa kitonga Sana.
Kila la kheri mkuu.