Fahamu mambo mbalimbali kuhusu biashara ya bidhaa za electronics

Wakuu nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tz
Twende kwenye mada, nipo kwenye mchakato wa kuchakata na kuanzisha biashara itayoweza endesha maisha yangu kwa kipindi hiki kigumu kwangu graduate.

Nina mtaji wa 4M ambapo nina chance ya kupata mkopo wa 2M pia
Sasa wakuu naomba mnisaidie kwa uzoefu wenu hii biashara ya vifaa vya electronics ipoje? Changamoto,faida, hasara na mateso yake.

Mfano wa vitu nitavyouza ni
Taa
Extension
Switches
Pipe
Nyaya
Viradio vidogo
Phone components
Some Pc components eg keyboard and mouse etc

Nakaribisha maoni yenu wadau

Pia nawaza au nianzishe biashara ya mobile money tu? Ila naona mtaji bado mdogo

Kama una idea nzuri pia naomba uiseme kwa mtaji huo

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Mambo km haya yanachuniwa humu sana!! Sio kwamba hawapo....
 
Ukipata mahali pamechangamka nadhani huo mtaji unafaa ila tafuta frame ambayo sio ya gharama
 
Anza na bidhaa kidogo, uza bidhaa online, utaepuka kulipa kodi, umeme, licence, n.k
Tafuta maduka ya wholesale ununue, unaweza kuanza na extension wire, switches ata pisi kumi kumi.
Nafikiri hata millioni moja itatosha.
Kama unataka kufungua mlango wa vifaa hivyo chemsha bongo kidogo utapata jawabu.
1.Kodi ya mlango kwa miezi sita
2.umeme kwa muda wa miezi sita.
3. Licence kwa mwaka
3.Mshahara wa Shopkeeper kwa muda wa miezi 6,
4. Matumizi yako kwa muda ya miezi 6.
5. Fanya list ya vifaa unavyotaka kuingiza nenda wholesale shop, jumuisha bei ya vyote.
6. Fikiria kodi itakuwa kiasi gani.

Jumuisha 1-6 na vyengine ambavyo sikuviandika utapata jawabu.

Miezi ya mwanzo utatoa fedha bila kuingiza nyingi, sasa ili biashara iende, usitegemee kwamba itakulisha, inabidi wewe uipe support iyo biashara mpaka isimame.
Cha muhimu zaidi iyo biashara unayotaka kufungua utawapata wapi wateja, inabidi ufungue location nzuri ya kuwanasa wateja. Na mara nyingi milango yake ni ghali

Kama unauza online unakuwa uko sehemu zote changamoto iko kwenye delivery zaidi na uzuri wake hii inakuwa kama part time job, unaweza kuendelea na shughuli zako nyengine
 
Ubarikiwe sana mkuu..
Sema biashara ya vifaa vya umeme ukiifanya online ina changamoto sana, ila nimekuelewa sana kiongozi
 
Huo mtaji unatosha kabisa kuanzisha hiyo biashara.
Cha msingi location iwe ya watu wengi mfano karibu na vituo vya daladala au sehemu yenye population.
Pili kwa sababu ndio unaanza, nunua kibanda cha mabati bei ni Kama 700k hv alafu utafute kijieneo kilicho wazi na ukodi kuweka kibanda chako. Hii itasaidia kupunguza machungu ya Kodi wakati bado unatafuta kujulikana na wateja wako. Bei ya eneo la kuweka kibanda huwa Kati ya 15k-25k.
Tatu, Tenga muda wako nenda kariakoo (Kama unaishi dsm itakuwa rahisi) upate kuzunguka kupata machimbo ya bei za jumla za chini zaidi. Kuna wachina flan mwaka jana walikuwa wanashusha mpaka makasha 20 ya vifaa vya umeme, Bai zao zilikuwa kitonga Sana.
Kila la kheri mkuu.
 
Ahsante sana kaka

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Wakuu njoon mtoe mawazo
Halafu nina swali
Hivi viredio vidogo vya Bluetooth is connected kwa bei ya jumla vinauzwaje ?
Hususani hizi tunazonunua kwa 10k-30k

Back
Top Bottom