Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Ahsante mkuu, na mimi mwakani nitapanda. Tatizo la kilimo cha Tz unaweza kuta baada ya miaka 5 bei ikaporomoka sana.
 
Ahsante mkuu, na mimi mwakani nitapanda. Tatizo la kilimo cha Tz unaweza kuta baada ya miaka 5 bei ikaporomoka sana.
Ndio hvy kaka ila tusikate tamaa na kushuka kwa bei na kwa zao la korosho kama utapata kupeleka mwenywe nje ya nchi basi utakua mwenywe kufaidika sana.
 
Ndio hvy kaka ila tusikate tamaa na kushuka kwa bei na kwa zao la korosho kama utapata kupeleka mwenywe nje ya nchi basi utakua mwenywe kufaidika sana
Ila kupeleka nje ya nchi inatakiwa uwe na mzigo mkubwa sana ili uone faida. Uzuri wa Korosho ni zao la biashara pia chakula, tofauti na kitu kama Pamba ambayo mabadiliko ya teknologia yanaweza kuwapoteza kabisa.
 
Mkuu Ardhi ilikuwa inatolewa na Halmashauri ya Lindi. Sijuhi kwa sasa hivi kama bado wanatoa maana mvua ndo zinaishia labda mpk mwakani tena.

Nimefika Lindi last week na taarifa nilizopewa ni kwamba ardhi waliyoitenga kwa kilimo imeshakwisha!
 
Dah sawa kaka. ni msitu mkubwa sn wa kulimia au pori la kawaida tu kwa ajili ya kufanya usafi
 
Nna Eka 50 Ikwiriri, Rufiji aliyeko interested aje tuzungumze nimpe Eneo alime kwa makubaliano tukayobaliana.

Ova
 
Please naomba angalia sera ya kilimo kwanza na kipaumbele chake for the next five years. Na kama tuna road map yoyote

Hakuna sera ya kilimo kwanza Tanzania na haijawahi kuwepo. Labda kama unamaanisha sera ya kilimo!! Hata hivyo kwenye sera kuna issues tu na statements ambazo kwake sidhani kama zina msaada kwa sasa..labda ungemwambia asome 5 years plan ya nchi kuangalia vipaumbele hadi ifikapo 2020/21 ningekuelewa. Aidha pia unatakiwa ujue tofauti ya sera mkakati na master plan! Aidha kuna kauli mbiu na long term plans za nchi.
 
Katika pitapita zangu kwenye kata mbalimbali zilizopo Lindi, aise nimejifunza kuwa watu wengi waliochukua miche ya korosho msimu huu hakika wamekwenda kuipanda katika mashamba niseme machafu au ambayo hayakuandaliwa vizuri!

Nadhani kuna haja ya elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima juu ya maandalizi ya shamba hatua kwa hatua mpaka mche wa mkorosho unapopandwa!

Mengi ya mashamba hayo yanamilikiwa na watu waliopo mijini ambao wameweka vijana au mwanakijiji msimamizi ambae anatoa taarifa ya maendeleo ya shamba kupitia simu au picha za watsup!

Ndugu zangu ambao mna interest ya kuwekeza katika kilimo hiki napenda niwakumbushe kuwa kazi ya kilimo hata siku moja haijawai kufanywa au kusimamiwa kwa simu.

Wengi wetu tumeweka mategemeo makubwa sana tukiwa na calculator zetu mezani tuki reffer ile bei ya 3970 kwa kilo times namba ya kilo kwa mkorosho mmoja times idadi ya ekari ulizoambiwa na “mfanyakazi/msimamizi” wako kule Lindi kuwa zimepandwa msimu huu.

Changamoto ni kubwa na kinachoendelea Lindi na maeneo mengine katu hayataweza kututoa hapa tulipo kama juhudi binafsi katika kusimamia uwekezaji huu hazitachukiwa!

Naomba magwiji wa kilimo hiki ambao wamejaa tele katika jukwaa hili watufundishe hatua mbali mbali za maandalizi ili kuokoa jahazi ambalo kwa mtazamo wangu tayari limeshageuzwa lilikotoka na linakaribia kuzama!!

“”NIISHIE HAPO KWA SASA””
 
Nimeupenda ushauri wako huu and it is so technical.

Nimejifunza jambo muhimu ntakaloli apply mahali, literature zinasema hiyo 12M kwa 12M hadi 15M ila ushauri wako umeweka vizuri zaidi.
 
Based on the reference ulipewa maelezo sahihi tu ila LUMUMBA Kanyumbulika na kuinyumbulisha vizuri zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…