HABARI,
"mahavanga,
Hujakosea kwa kipimo chako hicho nakubaliana na wewe kabisa hata ukitaka miti 20 kwa heka inawezekana ,Kama umefatilia post zangu zote nilieleza vema,Kama mkulima anafanya kilimo cha mchanganyiko na mazao mengine kama mahindi,mtama,ufuta alizeti n.k ni sawa ila kama ni zao la korosho tu ni matumizi mabaya sana ya aridhi sana mita 12 duh.Ndugu mikorosho ya kubebeshwa na ya kisasa huwa haitanuki sana nitatuna picha moja kutoka mahali mkorosho wa miaka 10 haujazidi mita 3 upana kwa kila upande na kila mwaka wanavuna zaidi ya kilo 20 kwa mti mmoja hapo ndani ya mita 12 zako umeacha mikorosho miwili inayoweza kupandwa Hapo kati na bado ungeweza kupanda mazao mafupi kama maharage N.K.Unaweza kupanda idadi kubwa ya miti kwenye heka moja baada ya mika 10 na kuendelea inapozidi kubanana ndipo unapunguza mmoja mmoja ila tayari mti unakuwa umeshakupa mavuno kwa zaidi ya miaka 10 haingii akilini uwache eneo wazi kusubiri miaka 20 ibanane Duh Tusipende kukariri lazima tujiongeze tufate maelekezo ya pembejeo ila kuna mambo mengine lazima kujiongeza,India kati ya nchi zinazoongoza kwenye kilimo hicho kwa heka moja wanapanda mpaka miti 150-200 sasa wewe ndugu ukisema miti 30 Tusibweteke na aridhi tuliyokuwanayo tuangalie kuwekeza sehemu ndogo unavuna kikubwa.TEKNOLOGIA.TECHNOLOGY
LUMUMBA