Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HABARI,PatriceLumumba naweza kuwaangamiza kwa mbinu ipi wadudu wanaoshambulia mashina ya mikorosho hadi kukausha mti?
Wadudu hao hutoboa mti na kupekecha ganda la nje kuzunguka mti wote na wanamuonekano kama funza.
Asante sana Mkuu, Nashukuru mnoHABARI,
Pole sana kwa hiyo changamoto,
Mdudu huyo anaitwa stream borrel au Kifauongo kwa kiswahil ni jamii ya wadudu funza..
huwa analeta hatari zaidi kwenye stage ya bull kama anavyoonekana Funza, Uzuri wao akianza kushambulia mkorosho ahami kwenda mwingine mpaka haumalize huo. Hutoboa na kuingia ndani na kufyonza ute wa ndani wa mkorosho na kuharibu mfumo wa ustawishaji wa virutubisho rishe(Nutrients) na maji kutoka kwenye mizizi na kupelekea mkorosho kukauka kwa kukosa mawasiliano kati ya mizizi na sehem ya juu y mti, kwa kuharibu xylem & phloem(sehem za kati ya mmea za kuptisha maji)..
Kwa sasa hakuna dawa maalum ya kuondoa tatizo halo zilizothibitishwa na mamlaka ya viuatilifu na sumu dawa(TPRI). Hivyo ukiona dalili za hili tatizo kama viungaunga mfano wa maranda kwenye mkorosho, kama ni hatua ndogo yaani
iametoboa kidogo waweza kukata kiasi eneo lililoathilika kwa lengo la kumtoa ama chukua waya kama spoku kuingiza kwenye tobo kw lengo la kumchoma ili afe, na kama ametoboatoboa sana na maendeleo ya mkorosho si mazuri basi, unashauliwa mkorosho kuukata tu na kuuchoma moto mkorosho kwa lengo la kuzuia tatizo lisihame kwe mikorosho mingine..
Chakuzingatia: ni kutembelea shamba mala kwa mala, kufanya palizi kwa wakati, shamba lisiwe kando na miti mingi.
LUMUMBA
Inategemea mkuu ..ila haizidi week 3.Mnada ukifanyika hela inakaa mda gan ndoitoke..
Inategemea mkuu ..ila haizidi week 3.
Mfano Mnada wa kwanza ulifanyika tar 10 hadi tar 18 watu walishaanza kulipwa .
Anayependa kupata Miche Bora ya mikorosho awasiliane nami no 0784474935 nipo masasi, nasambaza Miche popote ulipo. Mwaka Jana nilisambaza Miche 4000 singida
Inategemea na maeneo unayotaka kununua ardhi.Mashamba kwa.ajili.ya kupanda korosho yanapatikana kwa bei gan ?
Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Kwa uelewa wangu mdogo, suala la nafasi kati ya mti na mti lina mambo mengi sana ya kuangalia kabla hujaamua kufuata ushauri wa wataalamu.
Wataalamu wa chuo cha maendeleo ya korosho pale naliendele mtwara wanasisitiza umbali kati ya mti na mti kuwa mita 12 na mstari na mstari pia kuwa mita 12.
Ukifuata utaratibu huu, utaona katika ekari moja unapa miche 25 mpaka 27.
Ila kiuhalisia, na kwakuzingatia majanga mengine yanayoendelea katika mashamba yetu kati ya kipindi ambacho mkorosho umepandwa mpaka kuanza uzalishaji yaani wadudu, magonjwa, wanyama waharibifu, ukame, mvua zilizozidi kipimo, majanga ya moto n.k, unaweza ukakuta unaishia kuwa na miche michache sana katika ekari moja.
Na kama msemaji mmoja alivyosema hapo juu, mikorosho ya sasa haitanuki saaaana kiasi cha kuanza kugusana katika umri mdogo wa miaka 3 mpaka mi5. Mimi nimepanda miche 45 mpaka 50 kwa ekari moja kwakuwa sipandi mazao mengine shambani kwangu. So far inakwenda vizuri sana na ninaamini ntavuna kwa miaka kadhaa kabla sijaanza kuipunguza ile ntakayoona inaanza kugusana.
Changamoto mashambani ni nyingi ila akili za kujiongeza pia zinaruhusiwa.. siyo kila kitu ni vitabu tu.. [emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu eneo ulipatia wapi..?Mkuu ni kweli kabisa uliyoandika hata mimi nimefuata ushauri wa wataalamu ila nimepanda miche 28 kila ekari moja
Kwa sasa nina shamba la ekari 40 ila nimepanda ekari 11 tu na lililobaki nategemea kulisafisha mwakani 2021 ili nipande lote na baadhi ya ekari nitapanda matunda ya aina zingine kama maembe, machungwa na malimao
Naendelea kufuatilia kwa ukaribu humu
Zinastawi vzr huko..?vipi ishaanza uzalishaji?Mkoa wa Tabora
Zinastawi vzr huko..?vipi ishaanza uzalishaji?
#MaendeleoHayanaChama
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Yaah..kichanga zinakua vzr sana..Nimepanda kwenye kichanga na zinastawi vizuri sana ila bado uzalishaji kwani ni mda mfupi tu nimeanza
Ila kuna watu wana mwaka wa 3 na uzalishaji ni mzuri sana na kuna Chuo cha kilimo ambapo wanatoa msaada mzuri sana
Kwenye kusafisha shamba unaweza tumia herbicides/kiuagugu?Njia ya Muheza Pangani tulianza kulima kitambo
Je unaweza tumia herbicides kiuagugu kusafisha shamba lenye mikoroshoYaah..kichanga zinakua vzr sana..
#MaendeleoHayanaChama
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app