Habari zenu wanajamvi..
Naomba mnishauri mwenzenu nahitaji kua mnene kias(kuongeza uzito).
Nimewahi kupima uzito wangu wakaniambia uko chini ya kiwango kinachokubalika ukilinganisha na urefu wangu.
Nimewahi pia kupima magonjwa mengi ikiwepo UKIMWI lakini sina.
Je nini ambacho natakiwa nifanye nibalance kama nilivyoshauriwa?
DAWA YA KUNENEPA MWILI?
Njia zinazo weza kukusaidia kuongeza unene
1.Kula chakula cha kutosha kila unapokula halafu chenye mafuta mengi,chakula chenye wanga zaidi nk.
2.Usikae muda mrefu bila kula chakula,muda kabla ya mlo mwingine usizidi masaa 4 au 3 halafu ukipata msosi kandamiza sawasawa.
3.Achana na mazoezi hasa yale ya kukimbia.
4.Kula chakula kingi kabla ya kwenda kulala.
5.Punguza mawazo
6.Punguza kula mboga za majani na matunda badala yake kandamiza nyama,maharage
nk.Kutimia njia za kawaida ni bora kwa sababu ukiona uzito umezidi unaachana na njia
hizi lakini unene wa dawa wakati mwingine hata kama ukiacha kutumia zinakuwa
zimeathiri mfumo wa asili wa utendaji kazi wa mwili huenda ukashindwa kuzuia tena.
7. Ukitaka kunenepa kula kwa wingi Ufuta mweupe mbichi changanya kidogo na sukari au pia waweza kupika huo ufuta ikawa ndio chakula chako utanenepa mwili wako.
8.Kula mkate weka na hii (White cheese) Jubini ndani yake utongezeka mwili na kunenepa.
white cheese aka Jubini