Fahamu mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia ili kunenepa au kuongeza uzito wa mwili (Kilo)

Fahamu mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia ili kunenepa au kuongeza uzito wa mwili (Kilo)

Subiri utanenepa muda ukifika. Wala usiutamani.
Na ukija usije ukalia ukasema unataka kukonda.
Me kabla sijaolewa nilikuwa na kg around 48 to 50. Saivi ninakaribia kg 80. Kupunguza kg 1 tu ishu. Natamani nifike walau 60 kg lkn meshindwa. [emoji26]
Ebu nipungizie japo kilo 2 tu na mim niwe mnene kidogo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mimi ni kijana wa 24 years umbo langu ni 1GB nataka ni angalau 4GB nisha kula mayai mboga za majani nyama mpka supu ya kitimoto na mtura si nenepi
Mkuu bado upo na 1GB.!? Ingependeza kama ungeleta mrejesho..!!
 
Kama huna mwili wakunenepa beba vyuma, maana more power is equal to more muscles. .. na muscle ni bora kuliko fats.
 
Habari zenu wanajamvi,

Naomba mnishauri mwenzenu nahitaji kua mnene kias(kuongeza uzito). Nimewahi kupima uzito wangu wakaniambia uko chini ya kiwango kinachokubalika ukilinganisha na urefu wangu.

Nimewahi pia kupima magonjwa mengi ikiwepo UKIMWI lakini sina. Je, nini ambacho natakiwa nifanye nibalance kama nilivyoshauriwa?
 
Asubuhi kunywa chai maziwa na sukari, mkate uliopakwa butter na jam mayai ya kukaanga (kama utaweza). Mchana ugali nyama au wali nyama. Usiku kiepe na mirinda ya baridi. Bila kusahau matunda na Mbita mboga pamoja na kunywa maji,
 
Asubuhi kunywa chai tenure sukari, mkate uliopakwa butter na jam mayai ya kukaanga (kama utaweza). Mchana ugali nyama au wali nyama. Usiku kiwis na mirinda ya baridi. Bila kusahau matunda na Mbita mboga pamoja na kunywa maji,
Asante mkuu
 
Pamoja na vyakula hivyo jitahidi sana uwe na amani ya moyo(stress free heart) mwenyewe utajishangaa!
 
Habari zenu wanajamvi..
Naomba mnishauri mwenzenu nahitaji kua mnene kias(kuongeza uzito).
Nimewahi kupima uzito wangu wakaniambia uko chini ya kiwango kinachokubalika ukilinganisha na urefu wangu.
Nimewahi pia kupima magonjwa mengi ikiwepo UKIMWI lakini sina.
Je nini ambacho natakiwa nifanye nibalance kama nilivyoshauriwa?

DAWA YA KUNENEPA MWILI?

Njia zinazo weza kukusaidia kuongeza unene

1.Kula chakula cha kutosha kila unapokula halafu chenye mafuta mengi,chakula chenye wanga zaidi nk.

2.Usikae muda mrefu bila kula chakula,muda kabla ya mlo mwingine usizidi masaa 4 au 3 halafu ukipata msosi kandamiza sawasawa.

3.Achana na mazoezi hasa yale ya kukimbia.

4.Kula chakula kingi kabla ya kwenda kulala.

5.Punguza mawazo

6.Punguza kula mboga za majani na matunda badala yake kandamiza nyama,maharage

nk.Kutimia njia za kawaida ni bora kwa sababu ukiona uzito umezidi unaachana na njia

hizi lakini unene wa dawa wakati mwingine hata kama ukiacha kutumia zinakuwa

zimeathiri mfumo wa asili wa utendaji kazi wa mwili huenda ukashindwa kuzuia tena.

7. Ukitaka kunenepa kula kwa wingi Ufuta mweupe mbichi changanya kidogo na sukari au pia waweza kupika huo ufuta ikawa ndio chakula chako utanenepa mwili wako.

8.Kula mkate weka na hii (White cheese) Jubini ndani yake utongezeka mwili na kunenepa.


cheese.jpg

white cheese aka Jubini
 
Asubuhi kunywa chai tenure sukari, mkate uliopakwa butter na jam mayai ya kukaanga (kama utaweza). Mchana ugali nyama au wali nyama. Usiku kiwis na mirinda ya baridi. Bila kusahau matunda na Mbita mboga pamoja na kunywa maji,
Unaandika vitu gani wewe havieleweki
 
Habari zenu wanajamvi..
Naomba mnishauri mwenzenu nahitaji kua mnene kias(kuongeza uzito).
Nimewahi kupima uzito wangu wakaniambia uko chini ya kiwango kinachokubalika ukilinganisha na urefu wangu.
Nimewahi pia kupima magonjwa mengi ikiwepo UKIMWI lakini sina.
Je nini ambacho natakiwa nifanye nibalance kama nilivyoshauriwa?
Veeswt,

Kuna vitu kadha wa kadha ambavyo inabidi uzingatie kabla hujaanza kuwa na wazo la kuwa mnene.

Unafanya kazi gani, je kazi yako inahitaji uwe na pumzi? Upo kwenye ndoa?, Mwenza wako anaushauri gani kuhusu mwili wako? Anataka unenepe?

Zingatia haya mambo kwanza. Lakini naomba uwe na amani kwenye moyo wako. Ukishakuwa na amani, na uridhike na unachokipata, utaanza kunenepa.

Kumbuka lakini unene sio dalili ya afya.

Disclaimer: huu ni ushauri tu, maamuzi tunakuachia wewe. Naandika haya nikiwa napata mvinyo, naomba usinihukumu.
 
Back
Top Bottom