Okay. Hapo kuna vitu vya kufix katika mlo wako.
Pia acha kuskip meal , umesema hapo wakati mwingine hauli usiku, jitahidi upate angalau milo mitatu yenye uwiano sawa wa vyakula kutoka kwenye makundi muhimu matano ya chakula nitayataja hapo chini
Nimeangalia vizuri diet yako ni ya kawaida sana . Sijajua kuhusu ujazo mfano chapati ngapi?, Samaki kiasi gani?? Wali kiasi gani.??
Pia katika mlo wako jitahidi kuchanganya makundi ya vyakula ili upate mlo kamili katika kila mlo iwe kifungua kinywa, chakula cha mchana au usiku.
Mlo wako hauna protini ya kutosha yani unakula protini kidogo tu ilimradi, katika zoezi la kuongeza uzito unatakiwa kuongeza vyakula vya protini zaidi.
Kutokana na uzito wako wa 52kg, inabidi upate kiasi cha protini kisichopungua 41g kwa siku ,hiki ni kiwango cha protini kinacho shauriwa kiafya kabisa na hakitaweza kukuletea madhara hasi katika afya yako.
UTAWEZAJE KUTIMIZA 41g PROTEIN INTAKE KWA SIKU (KUTOKANA NA CASE YAKO)
- Ongeza vyakula vya protini aina kwa aina katika milo yako. Kama vile nyama, mayai, maziwa, samaki, karanga, shayiri, maharage,
-Ongeza matunda yenye kiwango kikubwa cha protini kama vile apples, maparachichi,ndizi,
_ vidokezo zaidi utavipata chini mwishoni mwa andiko kwenye makundi
KIASI NA CHA PROTINI KATIKA BAADHI YA VYAKULA (PENDEKEZO YA VYAKULA NA KIASI ELEKEZI KUTOKANA NA CASE YAKO)
yai 1 ~ 6g
Maziwa glass/kikombe (mils 250) ~ 8g
Nyama kipande ya 100g ~ 27g
Ndizi 1 kubwa ~ 1.1g
Parachichi . 2 - 3g
Apple ~ 0.4g
Peanuts butter vijiko 2 ~ 8g
Kwa vyakula hivyo hapo juu kwa kiwango hicho nilichoelekeza unaweza pata zaidi ya 45g za protein kwa siku
NAMNA UNAVYOWEZA KUONGEZA PROTINI KATIKA MLO WAKO (KUTOKANA NA CASE YAKO)
Kwenye Breakfast yako ya chai na chapati unaweza kuongezea yai ,ukatoa chai ya rangi ukaweka maziwa kikombe kimoja hapo utakuwa na 14 ~15g za protini
Masaa kadhaa baada ya breakfast unaweza kupata hasusa (snatch) ya apple au ndizi ( ~ 1g protini)
Mchana unaweza kula ugali na nyama au samaki, dagaa, mboga mboga ukiongeza na tunda (haukosi protini ~ 25 - 30g)
Usiku ukipiga zako wali angalau ujazo wa kikombe cha 250g + mboga mboga, matunda, au maharage ( unaweza kupata protini kiasi cha 15g hadi 20g )
Ukizingatia hiyo menyu hapo juu haukosi 50g ya protini ambayo ni nyingi zaidi lazima utaona effect yake ukijenga habit ya kula milo hiyo kwa kipindi sikichopungua mwezi mmoja.
Usisahau maji safi ya kunywa katika kila mlo wako ( angalau lita 3 kwa siku), usinywe maji karibia na mlo au wakati wa kula
NYONGEZA: ILI KUPATA CHAKULA KATIKA UWIANO ULIO SAWA ZINGATIA VYAKULA KATIKA MAKUNDI HAYA HAPA KATIKA MLO WAKO
Matunda
Matunda kama vile pome apple (tufaa) na peasi
Matunda jamii ya machungwa kama vile machungwa, mandarins na zabibu
matunda jiwe kama vile mapera, cherries, persikor, nektariner na squash
matunda hari kama vile ndizi, papai, maembe, mananasi na tikiti
Matunda mengine kama vile matunda ya passion
Mboga mboga
Kundi hili la mboga limegawanyika katika makundi madogomadogo yenye virutubisho sawa,ikiwa ni pamoja na mboga za majani kijani, nyekundu na rangi ya machungwa, mboga zenye wanga, mboga za maharage na mbaazi. Madhumuni ya makundi haya madogo ni kukuongezea kula aina mbalimbali za mboga kutokana na virutubisho vyake.
Vyakula vyenye protini
Nyama, kuku, samaki, dagaa, mayai, karanga, mbegu, bidhaa za soya na maharage, mbaazi huunda kundi la chakula chenye cha kundi la protini . Ingawa kunde na maharage zipo katika kundi la vyakula vyenye nyuzinyuzi vyakula hivi huwa ni chanzo cha vyakula vyenye protini. Inashauriwa kula nyama ya kuku na nyama kutoka kwenye samaki na vyakula vingine kama vinavyopatikana kwenye mimea ili kuongeza afya ya mwili wako kwa kutokula nyama nyekundu kama za wanyama wa kufugwa au wa polini.
Nafaka
Vyakula vya nafaka ni vingi vilivyotengenezwa kutokana na ngano, shayiri, mchele, mtama na mahindi. Nafaka mbalimbali zinaweza kupikwa na kuliwa nzima,kusagwa kuwa mfumo wa unga na kupika aina mbalimbali ya vyakula kama mkate, ugali, uji, vitumbua, ama maandazi kwa ajili ya kifungua kinywa.
vyakula vya nafaka vinaweza kuvunjwa katika makundi manne madogomadogo. Kama vile
Mikate
vifungua vinywa Tayari kula, high fiber (wholegrain) oats, uji, muesli, wholewheatbiskuti
Nafaka - Mchele, shayiri, mahindi, mtama, uwele n.k
Bidhaa nyingine – kama Pasta, keki, popcorn, unga n.k
Maziwa
Kundi la maziwa ni kundi lenye vyakula na mazao yake zikiwemo bidhaa za maziwa na huwa na kiwango kikubwa cha madini ya kalsiamu. Maziwa ya ya mgando, jibini zaidi na bidhaa zote zenye maziwa ni sehemu ya kundi la chakula cha maziwa, . Ingawa USDA makosa calcium maboma soymilk kama sehemu ya kundi maziwa, haina ni pamoja na cream cheese, cream na siagi, kwa sababu wao siyo vyanzo muhimu ya kalsiamu. Inashauriwa kutumia maziwa au bidhaa za maziwa zenye mafuta kidogo kuzuia kupata kiwango kikubwa cha mafuta yenye lehemu mbaya. Watu wa makamo ya kati na wanaofanya kazi wanashauriwa kutumia vikombe vitatu vya chai vya maziwa kwa siku
Sent using
Jamii Forums mobile app